Watanzania warahisishiwa upatikanaji wa huduma za teknolojia


Pamoja na kuwepo kwa maendeleo ya kasi katika nyanja mbalimbali lakini sekta ya teknolojia inabaki kuwa moja ya njia ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa mafanikio hayo kwa kurahisisha kazi nyingi kufanyika kwa haraka.

Kwa kutambua hilo, kampuni inayohusika na utoaji wa huduma zinazohusiana na teknolojia ya EnGenius imeingia katika makubaliano na kampuni ya usambazaji wa vifaa vya kiteknolojia ya Red Dot ili iweze kusambaziwa vifaa na huduma mbalimbali ambazo zinafanywa na Red Dot katika nchi za Afrika Mashariki.
Mkuu wa Kanda wa EnGenius, Van Hsiao akizungumzia kazi ambazo wanazifanya na mipango ya kutoa bidhaa bora kwa nchi za Afrika Mashariki.

Kampuni ya EnGenius ambayo inatoa huduma kama za internet wireless, radio frequency (RF) technology na kusambaza bidhaa mbalimbali kama kompyuta imesema kuwa imefanya maamuzi ya kuingi katika makubaliano na Red Dot ikiamini kuwa ni moja ya njia sahihi ambayo itawawezesha kuwafikia wateja kwa karibu zaidi.

Akizungumzia makubaliano hayo, Mkuu wa Kanda wa EnGenius, Van Hsiao alisema kampuni ao kwa sasa inahitaji kujitanua katika nchi za Afrika Mashariki kama Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Ethiopia hivyo wameungana na Red Dot ili waweze kukuza biashara yao zaidi.

"Tumeingia makubaliano na moja ya wasambazaji wakubwa wa Red Dot na tunaamini watatusaidia EnGenius kufikia malengo yetu ya kuwa wauzaji wakubwa wa bidhaa za kiteknolojia kwa Afrika Mashariki, tunafahamu kuwa ni wasambazaji wakubwa na atatusaidia kukuza biashara yetu," alisema Hsiao.


Na Rabi Hume, modewjiblog.com
Mkurugenzi Mtendaji wa Red Dot Distribution akielezea jinsi ambavyo wamejipanga kufanya kazi na EnGenius. (Picha zote na Na Rabi Hume, modewjiblog.com)

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Red Dot Distribution, Munir Bharwani alisema kuwa ni ushirikiano mzuri ambao wameanza kuufanya na EnGenious na wana mipango mingi kuhakikisha malengo ambayo yamewekwa yanafikiwa.

"Tuna taraji mafanikio makubwa, Red Dot ni kampuni ya kitanzania ambayo inafanya kazi katika nchi za Afrika Mashariki kwahiyo tunatazamia ushirikiano huu utakuwa na faida," alisema Bharwani.
Meneja Mkuu wa Red Dot Distribution Tanzania, Rajesh Adiani akifungua halfa ya uzinduzi wa makubaliano kati ya Red Dot na EnGenius kwa kuelezea shughuli ambazo wanazifanya.
Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa EnGenius, Alishan Zaidi akilelezea huduma ambazo wanazitoa za kiteknolojia na usambazaji wa vifaa vya kiteknolojia kama kompyuta na kamera za usalama.
Mkurugenzi Mtendaji wa Red Dot Distribution, Munir Bharwani na Mkuu wa Kanda wa EnGenius, Van Hsiao wakipongezana baada ya kuingia rasmi katika makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja.

Baadhi ya wageni waalikwa wakiangalia bidhaa ambazo zinatolewa na EnGenius.
Baadhi ya wageni waaliakwa waliohudhuria halfa ya makubaliano ya Red Dot Distribution na EnGenius.

No comments:

Post a Comment

Pages