Posts

Showing posts from January, 2017

DCB YAWASOGEZEA WANANCHI HUDUMA ZA DCB JIRANI NA DCB PESA

Image
Na Zainab Nyamka, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamin Sitta amewapongeza uongozi wa benki ya DCB kwa kuweza kuwasogezea huduma ya kipesa ya "DCB Jirani" na "DCB Pesa" kwani kwa hatua hiyo ni wanakuwa miongoni mwa benki zinazoanzisha huduma zinazoendana na teknolojia za kisasa. Akizungumza katika uzinduzi huo, Mstahiki Meya Sitta amesema kuwa kwa kuanzisha huduma hiyo ni moja ya maendeleo yanayohitajika katika tasnia ya kibenki na zaidi anautaka uongozi wa bodi ya DCB kuongeza juhudi na ubunifu katika kuileteta mafanikio zaidi siku zijazo na kuendelza sifa nzuri iliyopatikana. Ameongeza na kusema kuwa, kuna changamoto ,mbalimbali katika sekta za kibenki zinakabiliana nazo ila ametoa ushauri kwa manispaa za Dar es salaam kutumia benki hiyo katika shughuli zao za kibenki ili kuiwezesha kupata amana za kudumu na zaidi amesisitiza kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni wataendelea kuwa mstari wa mbele kutumia DCB kwani wameweza kufaidika na

TTCL YAZINDUA HUDUMA YA 4G ZANZIBAR

Image
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti w Baraza la Mapinduzi Issa Haji Gavu akiwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Waziri Waziri Kindamba wakinyanyua mabango ya matangazo kuashiria kuzinduliwa kwa huduma ya 4G ya Kmpuni hiyo Zanzibar (kushoto) Mkuu wa Kanda ya Zanzibar Franscis Mabula. Na Khadija Khamis, MAELEZO Zanzibar. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Issa Haji Ussi Gavu amewataka wananchi kujiunga na huduma ya mawasiliano ya 4G LTE Zanzibar ambayo inauwezo mkubwa wa mawasiliano ya haraka . Akizundua huduma za 4G LTE katika ofisi za Kampuni ya simu Tanzania (TTCL) , Waziri Gavu alisema kwamba ukuaji wa teknolojia unawalazimu watumiaji wa simu za mkononi kuwa na mawasiliano ya uhakika. Waziri Gavu alisema kwamba huduma hiyo itawarahisishia wananchi wa Zanzibar mawasiliano katika kazi zao za kilimo, biashara ufugaji pamoja na wafanyakazi wa serikalini na sekta binafsi. “Teknolojia inaendelea kukua na kuja na ugun

BENKI YA POSTA TAWI LA MBEYA WASHEREHEKEA MAPINDUZI KWA KUFANYA USAFI

Image
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Posta Tanzania Tawi la Mbeya wakishiriki zoezi la usafi katika kituo cha Afya kiwanja Mpaka jijini Mbeya ikiwa ni sehemu ya kusherekea miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar . Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Posta Tanzania Tawi la Mbeya wakishiriki zoezi la usafi katika kituo cha Afya kiwanja Mpaka jijini Mbeya ikiwa ni sehemu ya kusherekea miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo pia wakabidhi vifaa vya usafi katika kituo hicho cha Afya . Zoezi la usafi likiendelea Erick Mwaigomole Mfanyakazi Benki ya Posta Tanzania Tawi la Mbeya akishiriki kikamilifu shughuli za usafi katika kituo cha Afya Kiwanja Mpaka jijini Mbeya kama sehemu ya kusherekea Miaka 53 ya Mapinduzi Zanzibar. Zoezi la Usafi likiendelea........ Meneja Msaidizi Benki ya Posta Tanzania Tawi la Mbeya Joseph Nzilla akizungumza na waandishi wa habari kuhusu zoezi la usafi ambalo limehusisha wafanyakazi wote wa benki ya posta tawi la mbeya kama sehemu ya kusherekea miaka 53 ya Mapinduzi Za

UZINDUZI WA KIWANDA CHA AZAM DAIRY PRODUCTS LIMITED FUMBA

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) na Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa wakikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Mradi wa kiwanda cha uzalishaji wa Maziwa (Azam Dairy Products Ltd.) huko Fumba wilaya ya Magharibi "A" Unguja, ikiwa ni katika shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kushoto) Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifungua pazia kuashiria Uzinduzi wa Mradi wa kiwanda cha uzalishaji wa Maziwa (Azam Dairy Products Ltd.) huko Fumba wilaya ya Magharibi "A" Unguja, ikiwa ni katika shamra shamra za maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kushoto) Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Azam Group Bw.Said Salim Bakhresa mara alipowasil