MCB YASHIRIKI BONANZA LA MICHEZO LA WALIMU WA MICHEZO DAR




NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
TIMU ya soka ya wafanyakazi wa Mwalimu Commercial Bank,(MCB), plc, imefungwa mabao 3-1 na kikosi mchanganyiko cha walimu wa jijini dar es salaam, katika pambano la kirafiki ikiwa ni sehemu ya mafunzo ya wiki moja ya walimu wa michezo yaliyofanyika chuo kikuu cha dar es salaam.
Pambano hilo lililopigwa kwenye uwanja wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, leo Oktoba 21, 2017, haikuwa kazi rahisi kwa kombaini ya walimu kushinda mchezo huo dhidi ya “mabenker” hao wa MCB, kwani hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, timu zote zilitoka sare ya bao 1-1.
Katika kipindi cha pili tena dakika za lala salama, wafanyakazi wa MCB walielemewa na kujikuta wanatundikwa mabao mawili ya haraka haraka.
Hata hivyo kocha wa MCB, Lufingo Mwakilasa, aliwasifu wachezaji wake kuwa wamejitahidi kucheza vizuri licha ya hali ya hewa kuwa mbaya (joto kali), lakini pia asili ya kazi yao ambayo muda mwingi huwa wanautumia wakiwa maofisini kuhudumia wateja ukilinganisha na wenzao ambao ni walimu wa michezo na muda mwingi huwa wanafanya mazoezi.
Akizungumzia pambano hilo la kirafiki, Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko cha benki hiyo, Valence Luteganya alisema, kwa takriban wiki moja walimu hao wa michezo walikuwa wakishiriki semina ya mafunzo chuo kikuu ambayo MCB ilidhamini semina hiyo.
“Mchezo huu ni wakujenga ushirikiano wa karibu na wenzetu walimu, ambao nao ni wateja wetu wakubwa.”alisema Lutenganya.

Kombania ya walimu wa michezo wa jiji la Dar es Salaam, ambao walimenyana na wafanyakazi wa MCB katika pambano la soka la kirafiki.

Mchezaji wa MCB, (Kulia), akimenyana na mwenzake wa kombania ya Walimu.

Priva Audax wa MCB, akijikunjua kufumua shuti.




Kocha mkuu wa MCB, Lufingo Mwakilasa

Wachezajiwa MCB (kulia), wakisalimiana na wwenzao wa Kombania ya walimu wa Dar es Salaam tayari kuanza mchezo huo.

Kipa wa MCB, akiruka kuokoa mpira

Kipa wa MCB, akipangua mpira

Priva Audax wa MCB

No comments:

Post a Comment

Pages