Posts

Showing posts from 2024

Tanzania Yashinda Tuzo Ya Umoja Wa Mataifa Ya Ubunifu Bora Katika Huduma Za Umma Kupitia Mfumo Wa E-Mrejesho.

Image
  Tuzo za Umoja wa Mataifa za Ubunifu katika Huduma za Umma 'UN Public Service Innovation Awards' zimetolewa leo Juni 26 mwaka huu, nchini Korea Kusini kwenye Kilele cha Wiki ya Utumishi wa Umma ya Umoja wa Mataifa 'UN Public Service Week 2024'. Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa 72 zimeshiriki ambapo mifumo 400 iliwasilishwa na mifumo 15 ukiwemo wa e-Mrejesho ilishinda tuzo mbalimbali ambapo, kutoka Afrika nchi zilizoshiriki na kushinda tuzo hizo ni Tanzania na Afrika Kusini pekee. Mfumo wa e-Mrejesho unawawezesha wananchi kutuma kero au malalamiko, maoni, maswali, na pongezi kidijiti kwenda katika taasisi yoyote ya umma na kisha kupata mrejesho wa utekelezaji wake kidijiti mahali walipo. Mfumo huu umetengenezwa na Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Mfumo wa e-Mrejesho unapatikana kwa njia tatu ambazo ni kupitia simu ya mkononi kwa kubofya *152*00# na kisha kuchagua namba 9 na kisha nam