FM ACADEMIA "WAZEE WA GWASUMA" KUWASHA MTO WILAYANI HAI KATIKA UZINDUZI WA FLOMENA BAR USIKU WA JUMATATU YA PASAKA


Na Woinde Shizza,Arusha

Bendi ya FM Academia 'Wazee wa Ngwasuma wanatarajiwa kuwasha moto  ndani ya ukumbi mpya wa kisasa  ujulikanao kwa jina la Flomena uliopo  wilayani hai mkoani Kilimanjaro usiku wa jumatatu ya pasaka .

Akizungumza na waandishi wa habari muandaaji wa onyesho hilo  Swaum kileo alisema kuwa ameamua kuwaleta bendi hiyo katika uzinduzi huo ili kuweza kuwafurahisha wananchi wa mkoa wa kilimanjaro na mikoa jirani katika sikukuu hiii ya pasaka.
Alisema kuwa  bendi hii inamda mrefu sana aijafika wilayani hai ivyo wameamu kuileta ili wakazi wa wilaya hiyo nao wafurahie mziki wa dance unaofanywa na bendi hiyo.


Alitaja kiingilio cha onyesho hiyo kuwa ni shilingi 10000 za kitanzania huku akiwataja wathamini wa onyesho hilo kuwa ni Swaum fashion ,Tbl , libeneke la kaskazini blog pamoja , faraja saloon  pamoja na Radio five.



Kwa upande wa meneja wa bendi ya FM Academia kelvin  mkinga aliema kuwa wamejipanga vyema kuwapa burudani ya kutosha wakazi wa wilaya ya hai mkoa mzima wa Kilimanjaro pamoja na mikoa jirani  na kwa upendeleo watawatambulisha nyimbo zao mbalimbali mpya ambazo wameziandaa na wanatarajia kuzi zindua hivi karibuni.



Alisema kuwa pia wapenzi wake watakuwa na bahati zaidi kwani   show hii ndio itakuwa ya kwanza mara baada ya kutoka katika  shindano lao na bendi ya twanga pepeta

kwa upande wa Rais wa bendi hiyo Nyoshi El-Sadat   alisema kuwa timu  yake yote imejipanga vyema kuwapa burudani ya nguvu wakazi wa wilaya ya hai na mkoa mzima huku akisema  kuwa atawapa staili zote za gwasuma ikiwemo ile ya   vundesa  ambapo alisema kuwa wameiboresha na imekuwa ya kiufasaha  zaidi  na ina vinjonjo vingi zaidi ,staili tamu  pamoja na maneno matamu.



“tunatarajia kufanya show  ya kihistoria ambayo aijawai kufanyika  mkoani Kilimanjaro nah iii yote ni kwa ajili ya kuwaburudisha wapenzi wetu wa mziki wa dance wapenzi wetu wa bendi yetu ya fm academia”alisema nyoshi



Aidha alisema kuwa amewaandalia zawadi kubwa wapenzi wake wa mkoa wa huo  pamoja na mikoa jirani kwani watamuoana akiwa na muonekano mpya ambao hawajawai kuuona.





 ni pamoja na kuwaelewesha wapenzi wao nyimbo mpya na kuakikisha wapenzi wao wanajua staili zao zote za  nyimbo hizo na  sio ivyo tu pia alisema kuwa kwa kipindi  hiki wanataka kuwa wakazi wa arusha zawadi ya kuwaletea wasanii wote wa bendi hiyo ambapo alisema wapo 32  na wote watafika jijini Arusha chanzo :libeneke la kaskazini blog

No comments:

Post a Comment

Pages