Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza(kulia) akifanyiwa mahojiano na
Mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha ITV, IssaKwissa
Mwaifuge baada ya kuongea na waandishi wa habari kuhusiana na mwelekeo
na malengo ya kampuni ambapo alitoa takwimu za malipo ya kodi
serikalini 2014/2015 ambapo alibainisha kuwa Kodi ya malipo iliyolpwa
ni kiasi cha shilingi bilioni 46.4 na kukusanya kodi ya mapato, kwa
niaba ya serikali kodi ya ongezeko la thamani (VAT) zaidi ya shilingi
bilioni 108.6 na Kodi ya zuio inayofikia kiasi cha shilingi bilioni
81.5. kwa mwaka wa fedha uliomalizika mwezi Machi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza,akifafanua jambo kwa waandishi
wa habari wakati wa mkutano na waandishi hao kuhusiana na mwelekeo wa
kampuni ambapo pia alitoa takwimu za malipo ya kodi serikalini
2014/2015,Vodacom imelipa kodi ya mapato inayofikia shilingi bilioni
46.4 na kukusanya kodi ya mapato, kwa niaba ya serikali kodi ya ongezeko
la thamani (VAT) zaidi ya shilingi bilioni 108.6 na Kodi ya zuio
inayofikia kiasi cha shilingi bilioni 81.5. kwa mwaka wa fedha
uliomalizika mwezi Machi.
Baadhi
ya wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali Nchini wakimfatilia kwa
makini Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza(hayupo
pichani)wakati wa mkutano na vyombo vya habari kuhusiana na mwelekeo wa
kampuni ambapo pia alitoa takwimu za malipo ya kodi serikalini
2014/2015,Vodacom imelipa kodi ya mapato inayofikia shilingi bilioni
46.4 na kukusanya kodi ya mapato, kwa niaba ya serikali kodi ya ongezeko
la thamani (VAT) zaidi ya shilingi bilioni 108.6 na Kodi ya zuio
inayofikia kiasi cha shilingi bilioni 81.5. kwa mwaka wa fedha
uliomalizika mwezi Machi.
Kampuni
ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imelipa kodi serikalini kiasi cha
shilingi bilioni 46.4 kwa mwaka wa fedha wa 2014/15 ambao ulimalizika
mwezi Machi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza amesema jijini Dar es Salaam leo
kuwa mbali na kodi ya mapato,Vodacom imekusanya kwa niaba ya serikali
kodi ya ongezeko la thamani (VAT) zaidi ya shilingi bilioni 108.6 na
Kodi ya zuio inayofikia kiasi cha shilingi bilioni 81.5.
Kiasi
cha kodi ya mapato iliyolipwa kwa mwaka wa fedha wa 2014/2014 ni zaidi
ya shilingi bilioni 47.1 ambazo ililipa katika mwaka wa fedha wa
2013/2014 na kutangazwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania kama kampuni ya
pili kwa kulipa kodi nchini na ikiwa ni kampuni ya kwanza kchania maato
ya serikali katika sekta ya mawasiliano.Makampuni yaliyotangazwa kuwa ni
vinara wa kulipa kodi na kukusanya kodi za serikali nchini mwaka jana
ni Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Vodacom Tanzania na kampuni ya Sigara
Tanzania .
Meza
ambaye alikuwa anato taarifa ya utendaji na mwelekeo wa kampuni kwa
mwaka 2014/2015 alisema “Vodacom bado imeendeleza dhamira yake ya
kuendeleza sekta ya mawasiliano nchini na mpaka sasa tumewekeza kiasi
cha shilingi 1.8 trilioni na katika pindi cha mwaka huu tumelenga
kuwekeza zaidi shilingi bilioni 200 kwa aili ya kubresha mtandao wetu na
kuboresha zaidi bidhaa na huduma zetu tunazotoa”alisema.
Aliongeza
kuwa mtandao wa Vodacom umewafikia asilimia 99 ya watanzania kupitia
minara yake 3300 iliyopo sehemu mbalimbali nchini inayowawezesha
wananchi kunufaika na huduma kutoka mtandao huu bora nchini.
Meza
alisema pia kuwa kampuni inajivunia huduma yake ya M-Pesa ambayo imeleta
mapinduzi makubwa katika sekta ya kifedha nchini “Huduma hii inatumiwa
na zaidi ya watanzania katika kutuma ,kupokea fedha na kufanya mihamala
ya malipo mbalimbali na inazidi kuwarahishia maisha katika shughuli
zao za ujenzi wa Taifa”alisema Meza na kuongeza kuwa M-Pesa ina mawakala
zaidi ya 85,000 na imeunganshwa na mabenki 26 nchini na taasisi zaidi
ya 500 zimeunganishwa na huduma hii katika kufanya malipo na kukusanya
fedha.
Katika
kukuza teknolojia nchini Meza alisema Vodacom inaendelea kubuni huduma
za kuwarahisishia maisha na kupata taarifa,maarifa na burudani mbalimali
kupitia mtandao wa internet.
Ili
kukamilisha malengo na mikakati ya kuboresha sekta ya mawasiliano nchini
kwa mwaka 2015 ameitaka serikali kutoongeza kodi kwenye sekta ya
mawasiliano katika bajeti yake ya mwaka huu.Watanzania kwa sasa wanalipa
asilimia 33 (kodi ya zuio na ongezeko la thamani kwa muda wa maongezi
ambacho ni kiwango kikubwa katika ukanda huu wa Afrika. “Kupata
mawasiliano ni moja ya haki ya msingi hivyo kuna umuhimu yanapatikana
kwa kila mmoja kwa gharama nafuu”.Alisema
0 Comments