Baadhi
ya Mabalozi wa Vodacom Tanzania wanaoenda kutoa elimu kwa wateja wa
kampuni hiyo na wananchi kwa ujumla kuhusiana na huduma ya M-Pawa
wakimsikiliza Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa kampuni hiyo,Kelvin
Twissa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘M-Pawa Tumekufikia’ yenye lengo
la kuwaelimisha wateja wake nchi nzima kuhusiana na manufaa ya huduma
ya M Pawa inayowawezesha kujiwekea akiba na kujipatia mikopo nafuu kwa
urahisi zaidi.Uzinduzi huo ulifanyika makao makuu ya kampuni hiyo
Mlimani City jijini Dar e Salaam leo.
Mkuu
wa Mawasiliano na Masoko wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa(wakwanza
kushoto)na Ofisa Mkuu wa Idara ya M-Pesa,Jacques Voogt wakizindua
kampeni ya ‘M-Pawa Tumekufikia’ yenye lengo la kuwaelimisha wateja wake
nchi nzima kuhusiana na manufaa ya huduma ya M Pawa inayowawezesha
kujiwekea akiba na kujipatia mikopo nafuu kwa urahisi zaidi.Uzinduzi huo
ulifanyika makao makuu ya kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar e Salaam
leo.
Wateja
wa Vodacom Tanzania na wananchi kwa ujumla wanaonufaika na huduma ya
M-Pawa inayotolewa na kampuni hiyo kwa kushirikiana na benki ya CBA
itawafikia watanzania wengi zaidi baada ya kampuni hiyo kuzindua kampeni
ya kabambe ya ‘M-Pawa Tumekufikia’ yenye lengo la kuwaelimisha wateja
wake kuhusiana na faida na jinsi ya kunufaika na huduma hii
inayowawezesha kujiwekea akiba na kujipatia mikopo nafuu kwa urahisi
zaidi.
Kampeni
ya M-Pawa tumekufikia ambayo imezinduliwa leo jijini Dar es Saaam
itafanyika nchini nzima ambapo wataalamu wa huduma watapita kila mkoa
kutoa elimu juu ya matumizi na manufaa yake kwa ajili ya kujikwamua
kimaisha. Wanachi wanaoishi mijini na vijijini watapata fursa ya
kuelimishwa kuhusu M-Pawa na huduma nyingine za Vodacom Tanzania. Mbali
na elimu, wateja watajipatia zawadi mbalimbali na kupata burudani
kabambe kutoka kwa wasanii nguli wa hapa nchini.
M-Pawa
ni huduma inayowawezesha wateja wa Vodacom M-Pesa kuweka akiba na
kupata mikopo kupitia simu zao ambapo sasa imeboreshwa ili kuwawezesha
wateja wengi zaidi kupata mikopo. Tangu ilipozinduliwa mwaka jana,
huduma hii inazidi kupata mafanikio makubwa ambapo idadi kubwa ya
watanzania wanazidi kuichangamkia na kuboresha maisha yao kupitia mikopo
yenye masharti nafuu zaidi.
Mkuu
wa Mawasiliano na Masoko wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa amesema
katika kipindi cha mwaka mmoja tangu huduma hii ianzishwe imeonyesha
kuwa na mafanikio makubwa kwa kuwa tayari wananchi wengi wanazidi
kujiwekea akiba na kujipatia mikopo inayowawezesha kukabiliana na
dharura na kujikwamua kiuchumi kwa njia rahisi ya kupitia simu zao za
mkononi.
"Kadri
siku zinavyozidi kusonga mbele, wananchi wengi wamezidi kuipokea huduma
hii zaidi ya matarajio yetu. Watu wengi wamshafungua akaunti za M-Pawa,
wengi wanazidi kujiunga kila kukicha na wengi wanafurahia mikopo
kupitia huduma hii. Mpaka sasa zaidi ya wateja milioni mbili wanatumia
M-Pawa na tunawakaribisha wote kujitokeza katika kipindi cha kampeni hii
kupata ufahamu zaidi. Ratiba za misafara ya watoa elimu hii kwenye
maeneo mbalimbali zitakuwa zikitolewa kwenye vyombo vya habari hususani
redio kwenye maeneo husika”.
Alisema
teknolojia hii ya M-Pawa au “kibubu” ni mkombozi kwa wananchi wengi wa
Tanzania ambao walikuwa hawajafungua akaunti za benki “Kuna wananchi
wengi wamekuwa na utaratibu wa kukaa na fedha nje ya mabenki, ambako
hazileti riba zinawekwa kwenye magodoro,wengine kuzichimbia ardhini na
darini,fedha hizi haziko salama ni bora kuziweka M-Pawa” anasema Twissa.
Kuhusu
jinsi gani ya kutumia huduma hii mpya ya M-pawa, Twissa, alisema ni
rahisi, mteja haitaji kutuma wala kujaza fomu za maombi. Kila mmoja sasa
anaweza kufungua akaunti ya benki kwenye benki ya CBA kwa urahisi zaidi
kiasi tu cha kuchagua M-Pawa kutoka simu yake ya mkononi katika menu ya
huduma ya M-Pesa. Zaidi, haina gharama zozote wala ukomo wa kutoa ama
kuhamisha fedha kutoka M-pesa kwenda M-pawa na kinyume chake.
Aliwataka
watanzania kuchangamkia fursa hii na kupata elimu ya mikopo, akiba na
riba kutoka M-Pawa “Watanzania wengi bado hawana akaunti za benki na
sifa za kukopesheka kutoka taasisi za fedha. M-Pawa ni mkombozi kwa
wanyonge na wajasiriamali kwani inawawezesha kujiwekea akiba na kupata
mikopo isiyo na masharti magumu”.Alisisitiza.
0 Comments