Katika
kilio chake hicho, Millen kimemfanya Mama Samia kumfuta machozi na
kumpa kitambaa, mwanamitindo huyo huku akimweleza kuwa, Serikali
itaendelea kushirikiana naye kwani tatizo hilo si la Millen pekee bali
ni kwa wanawake wengi hapa Tanzania.
Mama
Samia alimwambia kuwa, tatizo alilonalo la kuziba kwa mirija ya uzazi
lipata ufumbuzi na kutaka asilie kwani Serikali inania njema kwa watu
wake hivyo wataendeleza juhudi Zaidi huku akifungua milango na mwanadada
huyo.
Suluhu
alisema kuwa hata yeye tatizo kama hilo lipo katika familia yake,
lakini ana amini kwa ushirikiano wa mwanamitindo huyo tatizo hilo
linapewa uzito. Alisema kuwa ni kitu kilichokuwa kikimuumiza sana
kichwa, ana amini kupitia Millen hata binti yake atapata nafuu.
"Nimefurahi
kukutana nawe na Serikali haitakuangusha tutakuunga mkono katika
kuhakikisha gonjwa hili linapata ufumbuzi na kutoa elimu kwa kila
mtanzania kulitambua"alisema.
Akizungumza
kwa upande wake Magese alisema amekuwa akifanya semina mbalimbali kwa
kushirikiana na madaktari bingwa wa Hospitali ya Taifa, Muhimbili,
kuwaelimisha wanawake kuhusu endometriosis.
Alisema
Machi 30, mwaka huu Taasisi ya Millen Magese ilikusanya vijana
(hususani wa kike) wapatao mia tano kutoka shule za Mugabe, Manzese,
Salma Kikwete na Turiani, kuwafundisha, kuwatahadharisha na kuwatanabahi
kuhusu Afya, Uenendo, Maisha yao ya kila siku na Changamoto zilizo
mbele yao na hususani ikilenga zaidi watoto wa kike ambao wao ndio
wahanga wa ugonjwa wa Endometriosis.
Magese alisema watoto hao wakiwafikia hata wenzao 20 tu kila mmoja basi takribani watu elfu kumi watakuwa wamefikiwa.
Alisema
ni mwanzo tu angependa kupata ushirikiano na msaada wa Serikali ili
afike kila pembe ya nchi yetu hii na kufikia wengi iwezekanavyo.
"Ninaamini
-Nikiokoa hata nafsi moja kuna wakati ambao inatosha kwani nafsi hiyo
yaweza kuokoa walio wengi zaidi,shabaha yake ni kuona wanawake wenye
ugonjwa huo wanapata tiba mapema ili waweze kubaki na uwezo wao wa
kushika mimba na kuzaa kwa njia ya kawaida" alisema Magese.
"
Mimi nilichelewa na nimejikuta nikipoteza uwezo wa kushika mimba, kwa
hiyo siwezi tena kupata mtoto kwa njia ya kawaida, Kibaiolojia.
Nimeshafanyiwa
oparesheni mara 13 kati ya Afrika Kusini na Marekani. Na sasa mirija
yangu yote ya uzazi imeziba, vilevile upande mmoja wa ovari haufanyi
kazi".
Naahidi
kupambana na ugonjwa huu mpaka mwisho. Pamoja na jitihada zote, lengo
langu la juu ni kuhakikisha napata uwezo wa kujenga hospitali kubwa
kupitia taasisi yangu ya Millen Magese (Millen Magese Foundation) ambayo
itajishughulisha zaidi na utoaji wa tiba ya endometriosis kwa wanawake.
Namuomba sana Mungu anisaidie.
Alisema lengo lake kuu na Taasisi yangu ni kujenga hospitali maalum ya magonjwa ya wanawake hapa nchini.
"Nitashukuru
sana iwapo Serikali yako tukufu itatusaidia kupata eneo la kutosha na
kutupa muongozo na uwezeshaji mwingine utakaohitajika kadri harakati
zitakapokuwa zikiendelea".
Alisema
tayari Taasisi ya Millen Magese kwa kushirikiana na ProjectCure ya
Marekani imeweza kukusanya vifaa vinavyohusu afya ya mwanamke vyenye
thamani ya takribani dola laki moja , ningeomba sana Serikali yako
Tukufu kutusaidia kuweza kusafirisha na kuviingiza vifaa hivyo nchini
(kwa maana ya taratibu, gharama za usafirishaji na kodi husika).
Kwa
namna moja ama nyingi napenda kuishukuru Wizara ya Afya kupitia kwa
Waziri wake Ummy Mwalim na Naibu Waziri Hamis Kingwangwalah, pamoja na
Mkuu wa Mkoa Paul Makonda, kwa uhirikiano wao na taasisi yangu ya Millen
Magese, katika kuhakikisha tunafanikisha suala la ujenzi wa kituo cha
Hospitali.
Tuko
katika maengezi na Hospitali ya Kairuki, ambao wamejitolea kuungana
name katika ksaidia tatizo hili, ikiwa ni pamoja na kushirikiana na
Hospitali za Serikali katika kusaidia wanawake wenye tatizo hilo.
Hospitali
ya Kairuki imejitolea kusaidia wanawake wenye matatizo hayo, nina amini
kwa ushirikiano wake Mhe. Makamu wa Rais, tatizo hili litapewa uzito
unaostahili.
Mheshimiwa
Makamu wa Rais,Elimu ya masuala ya uzazi na afya ya mwanamke
zifundishwe kwa wadogo zetu, tusichelewe na baadhi yao yakawafik
madhlahaya yasiyomithilika kama yangu, wakati mwingine huwa nahisi kama
visu vinapit tumboni mwangu, natapika, nazimia, nashindwa hata kufanya
kazi zangu, ni hivi karibuni tu katika onesho kubwa la mavazi, nilizimia
niliporudi nyuma ya jukwaa (Namshukuru Mungu kwa YOTE)
Naendelea
pia na kujitoa katika shughuli za kijamii, kama ambavyo nimeshafanya
kama kujenga madarasa na uchangiaji wa madawati, kama ambavyo nimewahi
kufanya mkoani Mtwara.
Nataka pia niwe balozi mzuri wa elimu yetu.
Mheshimiwa
Makamu wa Rais, Sitaki kulia, nimeamua kuwa SAUTI. Sitaki kumuuliza
Mungu kwa nini, nimeamua kupokea na kutimiza mapenzi yake. Mheshimiwa
Makamu wa Rais, #UpasuajiMara13Umetosha
#TunahitajiUtafitiZaidiKupataTIBA. Daima
najivunia nyumbani na popote nilipo duniani ..Tanzania imebaki kuwa tunu ya uwepo na maisha yangu.
Mwisho nakushukuru mheshimiwa makamu wa rais kwa mkutano huu, nawashukuru wote tuliokutana hapa. Mungu AWABARIKI.
Naomba
unipe ruhusa kama ishara kukukabidhi Tuzo na Tunu mbalimbali
nilizozitaja kwa Heshima ya Taifa, Nchi yangu ya Tanzania, Serikali
yangu na ndugu zangu Watanzania
#NawapendaSANA.
Kule kwetu Usukumani kwa heshima huwa tunapiga goti kama Heshima, Mheshimi wa Makamu wa Rais, Mama, nasema Wabeja SANA.
Mwandada Millen akiwa pamoja na Mama Samia wakati wa tuki hulo. Kushoto ni Katibu wa Makamu wa Rais.Millen akimuonyesha Mama Samia eneo linalomsumbua katika tatizo lake hilo
Mama
Samia akieleza namna walivyopokea tatizo hilo la Millen ambapo
amemweleza kuwa Serikali itaendelea kupambana nalo tatizo hilo hivyo
kumuakikishia Millen na taasisi yake kumuunga mkono.
Mama
Samia akimfuta machozi Millen ambapo alimwelezea kuwa kwa sasa asiie
tena kwani Serikali itahakikisha inapambana na ugonjwa huo ilikusaidia
wanawake wengi hapa nchini.
Mama Samia akiangalia moja ya tuzo hiyo..
Millen Magese akimkabidhi tuzo yake hiyo Mama Samia wakati wa tukio hilo
Mama Samia akiwa katika picha pamoja na rafiki wa Magese na wageni wengine waliojumuika katika tukio hilo..
Mama Samia akipata picha ya pamoja na familia ya Millen Magese
Mama Samia Suluhu akiwa na Millen Magese na rafiki zake wakati wa tukio hilo..
Mustafa akiwa pamoja na Mama Samia na Millen
Baadhi
ya Madaktari ambao ni wataalam wa kushughulikia tatizo la Endometriosis
akiwemo Dkr. Kiiruki wakiwa katika picha ya pamoja na Mama Samia na
Millen Magese.
Kaka wa Millen Magese akiwa akipata picha pamoja na Mama Samia na marafiki wengine wakiweo kutoka
Baadhi ya waandishi wa Habari wanawake wakiwa katika picha ya pamoja na Mama Samia pamoja na Millen wakati wa tukio hilo
Baadhi
ya wanahabari wa kiume wakiwa katika picha ya pamoja na Mama Samia
pamoja na Millen wakati wa tukio hilo lililofanyika jijini Dar es Salaam
katika makazi Makamu wa Rais. (Picha zote na Andrew Chale,
Modewjiblog).
0 Comments