MultiChoice-Tanzania waadhimisha siku ya Afrika

Baadhi ya Wafanyakazi wa  MultiChoice-Tanzania wakiwa katika vazi la kiafrika siku ya kuazimisha Africa day.

Jinsi Chaneli za TV za Barani Afrika zilivyofanikiwa kuelezea habari za Afrika katika mtazamo wa Kiafrika. 

Haukasiriki unapoangalia onyesho katika televisheni au filamu ya kutoka Afrika au kumhusu muafrika na kisha ukatahamaki, “ Hii haina chochote kinachofanana na Afrika ninayoijua?”. Kwa miongo kadhaa, tasnia ya burudani ya filamu na televisheni imetawaliwa na simulizi zenye maudhui ya nchi za Magharibi- hata pale zinapokuwa za kutoka Afrika na kwa ajili ya Waafrika. Kwa bahati nzuri, ndani ya miaka kadhaa iliyopita, tumeona mabadiliko japo ya taratibu lakini ya uhakika, ya simulizi zenye uhalisia kuhusu Waafrika zikisimuliwa kuhusu bara letu.

MultiChoice tunajisikia fahari kutokana na ushiriki wetu katika mabadiliko na maendeleo haya tangu kuanzishwa kwetu barani Afrika miaka 20 iliyopita. Mojawapo ya malengo yetu ya msingi ni pamoja na kuhakikisha kwamba huduma zetu zinawaendeleza wateja wetu kwa kuwaletea maudhui ambayo wanaweza kuyahusisha nayo na maisha yao ya kila siku. 

Lengo hili linatukumbusha dhamira yetu ya kuendelea kuunga mkono na kuendelea kuwekeza katika tasnia ya burudani barani Afrika na kuonyesha vipaji vya waafrika kupitia chaneli za hapa barani Afrika za MNet. Kutoka Nollywood mpaka Riverwood, tunaamini katika kusimulia na kuelezea habari au simulizi za Ki-Afrika ambazo watazamaji wetu wanaweza kuzihusisha nazo na maisha yao ya kila siku. Siku ya Afrika inapokaribia tarehe 25 May mwezi huu, tunasheherekea wasimulizi mbalimbali kutoka Afrika ambao wanachangia katika ukuaji wa tasnia ya filamu na televisheni ya Afrika.

Watazamaji wetu wametuamini kuwa waangalizi na wahifadhi wa simulizi za kiafrika na kuhakikisha panakuwa na simulizi zenye uwiano kuhusu Afrika. Kimsingi hakuna simulizi moja ambayo inafafanua au kuelezea kila kitu kuhusu bara letu na ndio maana chaneli zetu za zinazolenga bara la Afrika ambazo zinajumuisha Africa Magic, Maisha Magic Bongo, Maisha Magic East (E36) na Zambezi Magic, Mzansi Music na Mzansi Bioskop- zimeahidi na kujizatiti katika kuelezea simulizi za Afrika kama zilivyo. Chaneli hizi zinaleta mtazamo tofauti kuhusu maisha ya Afrika ambayo watazamaji wake wanaweza kuyahusisha na maisha yao ya kila siku.

Kama alivyowahi kusema katika mahojiano mtangazaji/mwanahabari mmoja kutoka Ghana wa BBC’s Focus On Africa ambaye sasa ni marehemu:
“ Hadhira ya ki-Afrika inabadilika. Watazamaji ni wa kisasa zaidi. Njia za zamani za kuelezea simulizi mbalimbali haziwezi kutimiza matakwa ya leo. Ninasikia fahari kwamba tunaweza kuelezea simulizi zaidi ya moja kuhusu bara letu. 

Kitu ambacho tumefanikiwa kufanya ni kubadili namna ya kusimulia. Lakini bado kuna nafasi ya kuwa na simulizi zaidi ya moja”Ningependa kukupa nafasi ya kufanya mahojiano na baadhi ya wasemaji wa chaneli za hapa nyumbani barani Afrika ambao wamejizatiti katika kubadili jinsi bara letu linavyoonekana au kutafsiriwa. Tafadhali usisite kuwasiliana nami endapo ungependa kujadili mada hii zaidi.I will also facilitate interviews between yourself and any of the following spokespeople:

Nitawezesha mahojiano baina yako na yeyote kati ya wasemaji wafuatao;


Wasemaji Wa MultiChoice
• CEO of M-Net, Yolisa Phahle
• Regional Director of M-Net West Africa Wangi Mba-Uzoukwu
• Head of Maisha Magic East, Margaret Mathore
• Head of Maisha Magic Bongo, Barbara Kambogi
• Head of Zambezi Magic, Addiel Dzonireva
• Director of Local Interest Channels, Nkateko Mabaso
Vipaji:
• Kunle Afolayan: Muigizaji na mshindi wa tuzo kutoka Nigeria, muandaaji wa filamu na muongozaji wa October 1, The Figurine, The CEO (itatoka July 2016) na zinginezo.
• Terry Pheto: Muigizaji na mshindi wa tuzo ya Oscar kwa filamu za Actress: Oscar-Award- Tsotsi and The Bold na The Beautiful soapie, muandaaji mwenza wa Ayanda & the Mechanic.
Tafadhali zingatia kwamba kutokana na tofauti za masaa kijiographia, mahojiano yanaweza kufanyika aidha kwa simu au uso-kwa-uso.
Asante kwa ushishirikiano wako na nasubiri kwa hamu kusikia kutoka kwako.

Wako mwaminifu,
Furaha Samalu

No comments:

Post a Comment

Pages