Mkurugenzi wa rasilimali watu wa Airtel, bwana Patrick Foya akiitambulisha kwa blogger VSOMO mfumo mpya unaomwezesha kijana wa kitanzania ,kupakua masomo ya ufundi stadi yanayotolewa na VETA kupitia simu yake ya Airtel.
Mmiliki wa 8020Fashions Blog Shamim Mwasha akiuliza swali mara baada ya kupata ufafanuzi juu ya mpango wa VSOMO ushirikiano kati Airtel na VETA kwenye mkutano ulifatiwa na Futari.
Baadhi ya Bloggers wakijaribu kupakua masomo ya ufundi stadi yanayotolewa na VETA kupitia simu zao na ipad zao.
Baadhi ya wafanyakazi wa Airtel wakiwa kwenye Futari baada ya mkutano wa VSOMO.
Mzee John kitime (katikati) wakijadili jambo pamoja na shamimu mmiliki wa blog ya 80/20 na Josephat Lukaza mmlimiki wa lukaza blog, wakati wa mkutano wa kuitambulisha VSOMO mfumo mpya unaomwezesha kijana wa kitanzania ,kupakua masomo ya ufundi stadi yanayotolewa na VETA kupitia simu yake ya Airtel
Baadhi ya bloggers wakipata futari
Airtel yafuturu na Bloggers
Katika mpango wake wa kukutana na kuendelea na mfungo wa mwezi Ramadhani leo Airtel kupitia Airtel FURSA imekutana bloggers na kuzungumzia mambo mbalimbali ikiwemo VSOMO mfumo mpya unaomwezesha kijana wa kitanzania ,kupakua masomo ya ufundi stadi na kupata cheti kupitia simu yake ya Airtel.
Akielezea VSOMO Mkurugenzi wa rasilimali watu bwana Patrick Foya alisema, ana anamatumaini kuwa VSOMO masomo ya Ufundi yanayotolewa na VETA kupitia simu za mkononi za Airtel, yatakua suluhisho kwa vijana wengi wenye ujuzi na ari ya kujifunza kufanya shughuli kwa uhakika kwani watakua wamejifunza mbinu zitakazowawezesha kuto bahatisha na kuongeza ufanisi katika kazi zao.
Nao bloggers walio hudhuria walikua na haya ya kusema, mfumo huu utaleta tija sana kwa vijana wengi ambao wako katika shughuli mbalimbali kupata muda wa kujifunza na kupata taaluma zitakazowawezesha kujiajiri, tunawapongeza Airtel kwa kuanzia mfumo huu wa masomo kupitia simu.
Aidha waliongeza kwa kusema wao watakuwa mstari wa mbele kushirikiana na Airtel kwa kuwafikia makundi mbalimbali ya vijana katika maeneo yao ya kazi ili kuhakikisha wanaitumia vyema fursa hii katika kujiendeleza kitaaluma.
0 Comments