Meneja
wa Benki ya CRDB tawi la Kasulu mkoani Kigoma Paul Chacha akizungumza
wakati wa hafla ya kumkabidhi Mkuu wa Wilaya Kakonko madawati 100 yenye
thamani ya Sh. Mil 5 yaliyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya kukabiliana
na upungufu wa madawati katika Shule za Msingi wilayani humo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kakonko mkoani Kigoma
Lusubilo Mwakabibi (aliyesimama kati kati) akizungumza muda mfupi kabla
ya benki ya CRDB haijakabidhi madawati 100 yenye thamani ya Sh. Mil 5
kwa ajili ya shule za msingi wilayani humo.
Mkuu
wa wilaya Kakonko mkoani Kigoma Kanali Hosea Ndagala akizungumza kabla
hajapokea madawati 100 yaliyotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya Shule
za Msingi wilayani humo.
Mkuu
wa wilaya Kakonko mkoani Kigoma Kanali Hosea Ndagala (kulia) akipokea
kutoka kwa Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Kasulu mkoani Kigoma moja ya
madawati 100 yaliyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya wanafunzi wa Shule
za Msingi wilayani humo.
Mkuu
wa Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma, Kanali Hosea Ndagaa (kulia) akipokea
sehemu ya msaada wa madawati 100 kutoka kwa Meneja wa CRDB Tawi la
Kasuu, Paul Chacha. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi wa Hamashauri ya Wilaya
ya Kakonko, Lusubilo Mwakibibi (katikati) na ofisa wa CRDB.
Mkuu wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma, Kanali Hosea Ndagala (walioka
kulia) akiwa na Meneja wa CRDB Tawi la Kasulu, Paul Chacha (katikati) na
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kakonko, Lusubilo Mwakibibi. Kushoto
waliosimama ni Katibu Tawala wa Kakonko, Zainab Mbunda.
Mkuu
wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma, Kanali Hosea Ndagala (kulia)
akimshukuru Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Kasulu, Paul Chacha baada ya
kupokea msaada wa madawati 100 kwa ajili ya Shule za Msingi Wilayani
humo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko,
Lusubilo Mwakibibi.
Mkuu
wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala (katikati) akiwa na Meneja wa
CRDB Tawi la Kasulu, Paul Chacha (wa pili kulia), Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Kakonko, Lusubilo Mwakibibi (kushoto) na Katibu Tawala wa
Kakonko, Zainab Mbunda.
0 Comments