Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BENKI
 ya NMB, imezindua Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani kwa kuahidi 
muendelezo wa huduma bora kwa wateja na kupokea ushauri kutoka kwa 
wateja na wadau, huku ikisisitiza utayari katika kuelekea Tanzania ya 
Viwanda.
Akizungumza
 wakati wa uzinduzi huo uliofanyika NMB Tawi la Msasani, Mkurugenzi 
Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker, amesema licha ya kuwa huduma bora ni 
kipaumbele cha kila siku, lakini wataitumia wiki hii kuboresha zaidi, 
ikiwamo kufanyia kazi maoni ya wateja.
Ineke
 amesema kwamba, kutokana na kauli mbiu ya Serikali ya Awamu ya Tano, 
chini ya Rais John Magufuli, ya kuigeuza Tanzania kuwa ya viwanda, benki
 yake iko tayari kuendana na kasi ya mchakato huo, ambao unategemea sana
 ubora huduma za kibenki.
Ineke
 ameongeza , benki yake imekuwa kinara nchini sio tu katika utoaji wa 
huduma bora kwa wateja, bali pia huduma bora za kijamii kwa ujumla, 
ambako imekuwa ikichangia katika sekta zote, zikiwemo za afya na elimu.
Aidha,
 katika kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani, NMB imepanga 
kufanya ziara katika Kituo cha Kulelea Wazee kilichopo Kigamboni jijini 
Dar es Salaam, ambako pamoja na mambo mengine, watatoa msaada na 
kuhudumu kwa wazee waliopo kambi hiyo.
Ineke
 amewataka wateja wa NMB kuwa sehemu ya maendeleo ya benki hiyo kwa 
kutoa maoni yatakayoongeza kasi ya huduma bora, huku akiahidi kuyafanyia
 kazi maoni yote ya maboresho yatakayotolewa na wateja wao nchini kote.
 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya NMB Inike Bussemaker
 akimkabidhi Godliver Mwendo cheti cha mfanyakazi bora wa benki hiyo 
katika uzinduzi a wiki ya huduma kwa mteja tawi la Msasani Jijini Dar es
 salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya NMB Inike Bussemaker(katikati)
 akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa tawi la NMB Msasani 
katika uzinduzi wa wiki ya huduma kwa mteja Jijini Dar es salaam.
Meneja
 wa kanda ya Kinondoni Vicky Bishubo akielezea namna benki ya NMB 
imeweza kuwafikia wananchi na wateja wao kwa uharaka na madhumini yao ya
 kuendelea kutoa huduma bora katika Wiki ya Huduma kwa wateja 
iliyozindulia. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya NMB Inike Bussemaker
 akizungumza na wateja waliofika asubuhi katika tawi la NMB Msasani na 
kuwaelezea malengo yao ya kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya NMB Inike Bussemaker akiwa na  sambamba na  Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Kipolisi Kinondoni SACP Suzane Kaganda katika kuchukua chakula.
 Wateja wa benki ya NMB wakiwa wanachukua chakula.

Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya NMB Inike Bussemaker
 akiwa anasalimia na Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Kipolisi Kinondoni SACP 
Suzane Kaganda leo katika uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja NMB 
Msasani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya NMB Inike Bussemaker wakizungumza jambo na  Kamanda
 wa Polisi  Mkoa wa Kipolisi Kinondoni SACP Suzane Kaganda katika 
uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja leo Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya NMB Inike Bussemaker
 akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa tawi la NMB Msasani 
katika uzinduzi wa wiki ya huduma kwa mteja Jijini Dar es salaam.
 
0 Comments