
 
Mkuu
 wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (wa pili kulia) akikata keki 
kuashiria uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja wa TTCL leo kwenye duka 
la huduma kwa wateja na bidhaa za TTCL lililopo Makao Makuu ya kampuni 
hiyo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni
 ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Waziri Kindamba pamoja na Mkuu wa 
Kitengo cha Biashara TTCL Kanda ya Dar es Salaam, Bi. Jane Mwakalebela 
(kulia) wakishuhudia tukio hilo. Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri 
Waziri Kindamba (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda 
(kushoto) wakigonganisha glasi za mvinyo mara baada ya mkuu huyo wa mkoa
 kuzinduwa Wiki ya Huduma kwa Wateja wa TTCL leo kwenye duka la huduma 
kwa wateja na bidhaa za TTCL lililopo Makao Makuu ya kampuni hiyo jijini
 Dar es Salaam.
 Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri 
Waziri Kindamba (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda 
(kushoto) wakigonganisha glasi za mvinyo mara baada ya mkuu huyo wa mkoa
 kuzinduwa Wiki ya Huduma kwa Wateja wa TTCL leo kwenye duka la huduma 
kwa wateja na bidhaa za TTCL lililopo Makao Makuu ya kampuni hiyo jijini
 Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimlisha keki Kaimu Afisa 
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Waziri Kindamba
 kwenye uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja wa TTCL leo.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimlisha keki Kaimu Afisa 
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Waziri Kindamba
 kwenye uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja wa TTCL leo. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimlisha keki Afisa Mkuu 
wa Masoko na Mauzo wa Kampuni hiyo, Bw. Peter Ngota kwenye uzinduzi wa 
Wiki ya Huduma kwa Wateja wa TTCL leo.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimlisha keki Afisa Mkuu 
wa Masoko na Mauzo wa Kampuni hiyo, Bw. Peter Ngota kwenye uzinduzi wa 
Wiki ya Huduma kwa Wateja wa TTCL leo. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimlisha keki mmoja wa 
wateja wa kampuni ya TTCL kwenye hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa
 Wateja wa TTCL leo.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimlisha keki mmoja wa 
wateja wa kampuni ya TTCL kwenye hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa
 Wateja wa TTCL leo. 
MKUU
 wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amezitaka taasisi na mashirika 
ya umma yaliopo chini ya mkoa wake kuiunga mkono Kampuni ya Simu ya 
kizalendo Tanzania (TTCL) kwa kuanza kuzitumia bidhaa za kampuni hiyo 
hasa kwenye shughuli za mawasiliano ili kuonesha uzalendo kwa vitendo. 
Makonda
 ametoa kauli hiyo leo Makao Makuu ya TTCL jijini Dar es Salaam 
alipokuwa akizinduwa Wiki ya Huduma kwa Wateja wa kampuni ya TTCL, huku 
akiahidi kuzishawishi taasisi na mashirika ya umma yanayofanya kazi 
chini ya utawala wake kuhakikisha wanatumia huduma za TTCL ili kuiunga 
mkono kampuni hiyo ya kizalendo ya mawasiliano. 
Alisema
 Serikali imeonesha nia njema ya kuirejesha TTCL katika hali nzuri baada
 ya kuirejesha kwa asilimia 100 chini ya umiliki wake, hivyo kuyataka 
mashirika na taasisi za umma kuunga mkono juhudi za Rais wa Tanzania, 
Dk. John Pombe Magufuli kuirejesha kampuni hiyo chini ya umiliki wa 
serikali kwa asilimia 100. 
Alisema
 yete kama kiongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam atahakikisha ofisi zote za 
umma zilizopo chini ya mkoa wake zitatumia huduma za TTCL na endapo 
watendaji wa TTCL sinazosita kutumia watoe taarifa ili yeye ahoji ni 
kwanini wanapinga agizo hilo. 
Aidha
 Mkuu wa Mkoa huyo alisitaka baadhi ya taasisi za umma wadaiwa sugu wa 
TTCL walipe madeni yao mara moja na zile zinazokaidi zifikizwe kwenye 
mkono wa sheria (mahakamani) kwa ajiri ya taratibu za kisheria. Alisema 
kampuni itafanya vizuri kihuduma endapo wateja wanaopewa huduma wanalipa
 kwa wakati ili iweze kuboresha huduma zake kwa wateja wote.  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipiga picha na mwenyeji 
wake huku akionesha alama ya mabadiliko inayotumiwa na TTCL.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipiga picha na mwenyeji 
wake huku akionesha alama ya mabadiliko inayotumiwa na TTCL. 
Kwa
 upande wake, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba 
akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa Makonda alisema Kampuni 
ya Simu Tanzani iliianza mchakato wa kuleta mabadiliko ndani ya kampuni 
hiyo tangu mwaka 2014, mpango uliopewa jina la 'TTCL Business 
Transformation Project' ambao ulilenga kuongeza tija na ufanisi katika 
uzalishaji na uwajibikaji ili kutoa huduma bora kwa Wananchi na Wateja 
wetu wote wa ndani na nje ya Tanzania. 
Aliyataja
 miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi chote cha mabadiliko 
ya kibiashara ni pamoja na kuirejesha Kampuni ya TTCL kumilikiwa na 
Serikali kwa asilimia 100 baada ya kuondoka kwa aliekuwa mbia mwenza, 
kupatikana kwa Masafa yanayowezesha kutolewa kwa huduma za 3G/4G na 
utekelezaji wa miradi mbali mbali ya kuboresha huduma. Kindamba 
aliongeza mafanikio mengine ni kupatikana kwa fedha kutoka kwenye vyanzo
 mbalimbali ikiwemo Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB), Kupatikana fedha 
kutoka Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ambazo zinatumika kwa ajili
 ya kupeleka mawasiliano vijijini na Ujenzi na ukarabati wa miundombinu 
ya mtandao wa Mawasiliano, mitambo chakavu, kusimika mitambo ya GSM-2G, 
UMTS- 3G na LTE- 4G. "...pia katika eneo la Biashara; Tumeendelea na 
juhudi za kutangaza na kuitambulisha huduma ya 3G/4G katika jiji la Dar 
es salaam, bidhaa nzuri ambazo zinakidhi mahitaji ya wateja zimekuwa 
chachu ya wananchi kuanza kuvutiwa na bidhaa za TTCL.
 TTCL
 tunatoa huduma ya T-TV ambayo wateja wanapata fursa ya kutazama 
matangazo ya vituo mbalimbali vya Luninga kupitia simu zao za Smartphone
 na tablet. 
Pia,
 TTCL imefanikiwa kuunganisha Hospitali Kuu za Mkoa wa Dar es salaam 
katika Mkongo wa TTCL, hivyo kutengeneza mazingira mazuri kwa taasisi 
hizo kuendesha huduma za afya kwa kutumia teknolojia yaani Afya-Mtandao 
(E-Health)," alisema Kindamba. 
Aidha
 alisema wiki ya Huduma kwa Wateja, TTCL inalenga kutambua na kuthamini 
mchango wa wateja, ambao wamekuwa chachu ya ukuaji wa Kampuni, huku 
kampuni ikijipanga kuwatembelea wateja wake, kuzungumza nao na kuomba 
ushauri wao ili tuweze kutoa huduma bora na endelevu ambazo zitaongeza 
tija katika kazi zao. 
"...Tumejipanga
 vyema kufanya kazi kwa ufanisi, tunatekeleza kwa vitendo falsafa ya 
Serikali yetu ya awamu ya tano ya Hapa Kazi Tu. Tutatumia rasilimali 
zetu vizuri ili Kampuni itoe mchango stahiki mageuzi yanayoendelea ya 
kuifanya nchi yetu kupiga hatua kuelekea kuwa nchi ya Uchumi wa Kati, 
Nchi ya Uchumi wa Viwanda. 
Katika
 kufikia lengo hili, huduma za Mawasiliano ni muhimu sana, na napenda 
kukuhakikishia kwamba, kwa kutumia huduma za TTCL, lengo hili 
litafikiwa," Alisema.  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (wa pili kulia) akimpa tuzo
 mmoja wa wafanyakazi bora wa kampuni hiyo kwenye duka la huduma kwa 
wateja na bidhaa za TTCL lililopo Makao Makuu ya kampuni hiyo jijini Dar
 es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (wa pili kulia) akimpa tuzo
 mmoja wa wafanyakazi bora wa kampuni hiyo kwenye duka la huduma kwa 
wateja na bidhaa za TTCL lililopo Makao Makuu ya kampuni hiyo jijini Dar
 es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipiga picha na 
wafanyakazi bora wa TTCL waliozawadiwa kwenye uzinduzi wa wiki ya huduma
 kwa wateja.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipiga picha na 
wafanyakazi bora wa TTCL waliozawadiwa kwenye uzinduzi wa wiki ya huduma
 kwa wateja. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipiga picha na baadhi ya 
viongozi waandamizi wa TTCL kwenye uzinduzi wa wiki ya huduma kwa 
wateja.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipiga picha na baadhi ya 
viongozi waandamizi wa TTCL kwenye uzinduzi wa wiki ya huduma kwa 
wateja. Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemus Mushi akitoa ratiba fupi ya hafla hiyo kabla ya uzinduzi.
 Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemus Mushi akitoa ratiba fupi ya hafla hiyo kabla ya uzinduzi. 
 
0 Comments