Meneja
Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, kushoto
akimpatia hati ya kiwanja cha Vikuruti, mteja wao Ibrahim Yusuph Ismail,
nyumbani kwao Kariakoo jijini Dar es Salaam, leo mchana. Kwa wiki hii
tu Bayport imeamua kuwapelekea hati za viwanja wateja wao katika maeneo
yao ya makazi na maofisini kwao.
Na Mwandishi Wetu, Dar esSalaam
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, wateja wa Bayport
waliojipatia viwanja vya Bayport vilivyopo Vikuruti, Mlandizi, wilayani Kibaha
mkoani Pwani wameendelea kupewa hati zao, huku safari hii wakipewa hati kwenye
maeneo wanayopatikana ikiwamo majumbani na maofisini. Hatua za kuwapelekea hati hizo wateja wao ni kitendo cha
kuthamini uwapo wa wateja wao wanaoendelea kuiamini Bayport Financial Services
katika bidhaa zake za mikopo ya fedha, bila kusahau huduma ya mikopo ya viwanja
vyenye hati inayotolewa na taasisi hiyo, kwa kushirikiana na wadau wa ardhi
walioingia mikataba na Halmashauri unapopatikana mradi wa viwanja kwa ajili ya
watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi, wajasiriamali na Watanzania
kwa ujumla.
Meneja
Biashara wa Bayport Financial Services, Thabiti Mndeme, kushoto
akizungumza jambo wakati anamkabidhi hati yake ya kiwanja mteja wao
Neema Jameson Nawita, jijini Dar es Salaam leo mchana.
Akizungumza
wakati wa kutoa hati kwa wateja watatu leo jijini Dares Salaam, Meneja
Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, alisema jambo
kubwa la miradi ya viwanja kwenye taasisi yao ni kuona weteja wao
wanapata hati ili kuweka ubora wa huduma zao, ikiwa ni sehemu muafaka ya
kufuta migogoro ya ardhi kwa kununua viwanja vyenye hati. Alisema kwa
wiki mbili mfululizo wamekuwa wakiendelea kutoa hati kwa wateja wao,
huku kwa wiki hii tu, taasisi hiyo ikifika mbali kwa kujenga imani na
kwenda sambamba na wateja hao, wakaona umuhimu wa kuwathamini na
kuwataka wachague maeneo wanayoona wanaweza kupokea hati zao, iwe ni
maofisini kwao au kwenye maeneo ya makazi.
Mteja
wa Bayport na mkazi wa jiji la Dar es Salaam, Neema Jameson Nawita,
kulia akipokea hati yake ya kiwanja cha Vikuruti, wilayani Kibaha,
mkoani Pwani, aliyokabidhiwa leo na Taasisi ya Kifedha ya Bayport
Financial Services.
Mteja
wa Bayport na mkazi wa jiji la Dar es Salaam, Neema Jameson
Nawita,kulia akizungumza na waandishi baada ya kukabidhiwa hati yake ya
kiwanja cha Vikuruti, Mlandizi,wilayani Kibaha, mkoani Pwani. Kushoto ni
Thabit Mndeme, Meneja Biashara wa Bayport Financial Services.
Meneja
Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, kushoto
akimkabidhi hati ya kiwanja cha Vikuruti, Mlandizi, wilayani Kibaha
mkoani Pwani mteja wao Hassan Omary Hamis, jijini Dar es Salaam, leo
mchana.
Meneja
Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, kushoto
akizungumza jambo baada ya kukabidhi hati ya kiwanja kwa Hassan Omary
Hamis
Meneja
Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, akizungumza
jambo wakati anakabidhi hati za viwanja kwa wateja wao wa Bayport
Financial Services hawapo pichani leo jijini Dar es Salam.
“Huu
ni utaratibu tulioamua kwa wiki mbili hizi kwa wateja waliokuwa
wanapokea hati tuwafikishie kwenye maeneo yao ili waone taasisi yetu
inawathamini na kuwashukuru kwa sababu wamekuwa wakiendelea kuunga mkono
bidhaa zetu zote, ikiwamo huduma ya mikopo ya viwanja vya Vikuruti
tulivyoanzisha mwaka jana na mwaka huu tukianzisha huduma za viwanja
katika maeneo ya Bagamoyo, Chalinze, Kibaha, Kilwa na Kigamboni. “Huduma
hizi ni nzuri kwa Watanzania wote mahala popote walipokuwa wanaweza
kukopa au kununua viwanja hivi kwa njia pia ya fedha taslimu, ambapo kwa
(Kimara Ng’ombe) Bagamoyo mita moja ya mraba inauzwa Sh 10,000,
(Msakasa) Kilwa Sh 2000, (Boko Timiza) Kibaha Sh 9000, (Tundi Songani)
Kigamboni Sh 10,000 na (Kibiki na Mpera) Sh 4500, ambapo huduma zetu
zinapatikana pia kwenye matawi yote yaliyoenea sehemu mbalimbali za
Tanzania Bara,” Alisema Mndeme.
Naye Neema Jameson Nawita aliwashukuru Bayport kwa kumpatia hati yake
bila usumbufu wowote, akisema huduma zao za viwanja zinaonekana
kuandaliwa vyema huku zikiwa hazina usumbufu wowote katika kuandikishwa
hadi upewaji wa hati zao. “Nimefurahi kwa sababu nimefanikiwa kuwa
miongoni mwa Watanzania waliopewa hati za viwanja vya Vikuruti baada ya
kununua kiwanja hicho mwaka jana na nzuri zaidi nimepata bahati kubwa
kwa sababu nimeletewa hati hadi eneo la ofisi yangu,” Alisema.
Naye
mjasiriamali Ibrahim Yusuph Ismail aliipokea hati yake shangwe na
kusema kufanikiwa kununua kiwanja cha Vikuruti na kupewa hati yake bila
usumbufu ni hatua nzuri na mwendelezo wa kujiendeleza kwa kutumia
rasilimali bora ya ardhi.
Mteja
mwingine aliyezungumzia hatua hiyo ya upewaji hati ni Hassan Omary
Hamis, ambaye aliwataka Watanzania wote kuchangamkia fursa bora ya
uwekezaji wa ardhi kwa kujenga nyumba za makazi na za biashara ili
waongeze wigo wa kipato chao.
“Tusiogope
kuwekeza kwa sababu ni jambo la msingi ukizingatia kwamba zipo taasisi
zenye kiu ya maendeleo wakiwamo Bayport, maana si lazima mtu anunue kwa
pesa taslimu, ila anaweza kununua kiwanja kwa njia ya mkopo usiokuwa na
usumbufu na ukiwahusu watumishi wa umma, wafanyakazi wa kampuni binafsi
na wajasiriamali,” Alisema.
0 Comments