Afisa
Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (wa 3 kushoto) akimkabidhi
Kanizio Annatory (katikati) ambaye ni miongoni mwa vijana waliowezeshwa
na mpango wa Airtel Fursa “Tunakuwezesha” mashine na vifaa vya kuoshea
magari pamoja na sehemu ya kisasa ya kufanyia biashara, akishuhudiwa na
ndugu zake pamoja na wafanyakazi wa Airtel katika hafla iliyofanyika
kijiji cha Kamnazi mkoani Kagera.
Afisa
Uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (kwanza kulia) pamoja na
wafanyakazi wa Airtel wakimwonesha Kanizio Annatory (wa pili kushoto)
sehemu ya kisasa ya kuosha magari aliyowezeshwa na mpango wa Airtel
Fursa “Tunakuwezesha” baada ya kukabidhiwa mashine na vifaa vya kuosha
magari katika hafla iliyofanyika kijiji cha Kamnazi mkoani Kagera.
Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (4 kushoto) akimkabidhi
Kanizio Annatory (2 kulia) ambaye ni miongoni mwa vijana waliowezeshwa
na mpango wa Airtel Fursa “Tunakuwezesha” mashine na vifaa vya kuosha
gari pamoja na sehemu ya kisasa ya kufanyia biashara, akishuhudiwa na
dada yake Agnes Annatory (kulia) pamoja na wafanyakazi wa Airtel katika
hafla iliyofanyika kijiji cha Kamnazi mkoani Kagera.
Afisa
Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (wa 3 kushoto) akimkabidhi
Kanizio Annatory (katikati) ambaye ni miongoni mwa vijana waliowezeshwa
na mpango wa Airtel Fursa “Tunakuwezesha” mashine na vifaa vya kuoshea
magari pamoja na sehemu ya kisasa ya kufanyia biashara, akishuhudiwa na
ndugu zake pamoja na wafanyakazi wa Airtel katika hafla iliyofanyika
kijiji cha Kamnazi mkoani Kagera.
Mwanzoni
mwa wiki hii Airtel kupitia mpango wake wa Airtel Fursa iliweza
kufika katika kijiji cha Kumnazi wilayani Ngara mkoani Kagera na
kumfikia Kijana Kanizio Annatory anayejishughulisha na biashara ya
kuosha magari, kwa kumpatia vifaa na kufanyiwa ukarabati wa eneo lake la
kazi . Vijana wengi wanaamini maisha mazuri na fursa za kiuchumi
zinapatikana mjini, lakini kwa Kijana Kanizio kupita kwa barabara katika
kijiji hiki ni fursa adhimu kwake.
Airtel
Fursa umelenga katika kuwezesha vijana wajasiriamali hapa nchini kwa
kutoa msaada kwa vijana ambao wanaonyesha juhudi ya kujikomboa na
changamoto za maisha katika Jamii zinazowazunguka kwa kuwapatia vitendea
kazi na kutoa mafunzo ya biashara ya ujasiriamali. Airtel Fursa ni moja
ya sehemu ya utekelezaji wa wajibu wa Airtel katika kurudisha sehemu
ya faida wanayoipata kwa jamii ili kukidhi matakwa ya kiuchumi, na
kuunga mkono jitihada za serikali katika kubadilisha maisha ya wananchi.
Akiongea
wakati wa makabidhiano afisa uhusiano na matukio wa Airtel, Dangio
Kaniki alisema kuwezeshwa kwa kijana huyu kupitia Airtel fursa ni
ukombozi wa kiuchumi kwa familia yake na Jamii inayomzunguka. Kama
alivyokuwa amebainisha katika maombi yake kupitia mpango wa Airtel
Fursa, hatua hiyo imetafsiriwa kama kichocheo cha mapinduzi ya
kibiashara na fursa za kiuchumi kijijini hapa Kumnazi.
“Tunawahimiza
vijana kujitokeza kwa wingi na kuchangamkia fursa hizi pale
zinapojitokeza kwani baadhi ya vijana wamekuwa wakihamia mijini na
kuacha kazi ya uzalishaji mali kufanywa na wazee na wanawake na hivyo
kukwamisha maendeleo vijijini” aliongeza Dangio
Akizungumza
mara baada ya kupokea msaada huo, Kanizio amesema msaada huo ni
mkombozi wa maisha yake na familia huku dada yake Agnes Annatory
akiishukuru Airtel kwa kuwa mkombozi kwao.
Kanizio
alisema “ nawashukuru sana Airtel kwa kuweza kufanikisha ndoto zangu
kwa kuweza kunipatia vifaa hivi vya kisasa kwani nimekuwa nikipata ugumu
wa kupata wateja kwani sikuwa na vitendea kazi vya kutosha
vitakavyoweza kukidhi mahitaji ya wateja wangu, lakini sasa ninaamini
nitapata Wateja wengi sana na kuinua biashara yangu.
Mpaka sasa Airtel Fursa toka ianze imeweza kuwainua vijana wapata 2800kwa
kuwapatia vifaa mbali mbali kwa kuendeleza bishara zao na vile vile
kutoa mafunzo ya biashara katika mikoa mbali mbali hapa nchi, na katika
msimu huu wa pili Airtel Fursa imetenga kiasi cha shilingi bilioni moja
kwa ajili ya kubadlisha maisha ya vijana hawa.
0 Comments