USIKU WA OLD IS GOLD KILA JUMAPILI SAFARI CARNIVAL


Usiku wa Old is Gold taarab  kila Jumapili ndani ya Safari Carnival
Na Andrew Chale
USIKU wa Old is Gold taarab  unatarajiwa kurindima ndani ya ukumbi wa Safari Carnival, Mikochezni B, kwa wadau kupata burudani ya muziki wa mwambao wa kizamani.
Kwa mujibu wa waandaji wa usiku huo, Mkurugenzi wa Fabak Fashions, Asia Idarous Khamsin  alieleza kuwa  ni kila Jumapili  ndani ya ukumbi huo utakuwa na burudani ya kipekee kwa nyimbo za mwambao pamoja na ‘surprise’ mbalimbali kwa watakaofika hapo.
“Kila jumapili  kwa kiingilio cha sh 5,000 tu. Wapenzi wa muziki wa mwambao  watashuhudia shoo ya Usiku wa Old is Gold ndani ya Safari Carnival” Alisema Asia Idarous
Aliongeza kuwa, mbali na burudani ya taarab za zamani  pia kutakuwa na ‘Surprise’ mbalimbali" kwa wadau watakaojitokeza kwenye usiku huo.
Aidha,  Asia Idarous alisema usiku huo, pia umedhaminiwa na  Safari Carnival, Fabak fashions, Clouds fm, Gone Media, Maji Poa, Michuzi Media Group na wengineo.

No comments:

Post a Comment

Pages