KAMPUNI YA ORYX GAS YAJIVUNIA KUWA RAFIKI WA MAZINGIRA

Na Emmanuel Masaka,Dar.

KAMPUNI ya mama katika usambazaji na uuzaji wa gesi ya ORYX nchini ijulikanayo kama ORYX ENERGIES LTD imekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha nishati mbadala inatumika badala ya mkaa ambao umeonekana kuwa wa gharama sana.

Akizungumza katika kuadhimisha Wiki ya mazingira leo viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam Mkuu wa Kitengo cha Mauzo kampuni ya gesi ya ORYX Jeffrey Nasser amesema kuwa ORYX GAS amekuwa rafiki mkubwa wa mazingira pale walipoamua kuletea nishati mbadala ya ges.

"Na haikuishia hapo tu bali tuliwawezesha wananchi wengi sana nchi nzima kuipata kwa gharama ndogo na hata yale maeneo ya wananchi wa hali ya chini tumewawezesha kupata gesi yetu. Na Tunaamini tumeokoa miti mingi ambayo ingekatwa kwa matumizi ya kupikia,"amesema.

Amefafanua kwa ORYX GAS kwa nyakati tofauti wamekuwa wadau muhimu katika kuunga mkono jitihada za Serikali katika kutunza mazingira, na kwa muda mrefu wamekuwa na kampeni yao ya ORYX GAS "Rafiki wa Mazingira".

Hivyo amesema katika kuadhimisha Wiki ya mazingira wameamua kuchukua fursa kujiunga na wadau wengine kushirikiana katika kuelimisha wananchi umuhimu wa kutunza mazingira kwa kuwapa nishati mbadala ya gesi ya kupikia kwa gharama nafuu sana ukilinganisha na nishati ya mkaa ambayo inachochea uharibifu wa miti na mazingira kwa ujumla.

"Lengo letu ni kuhakikisha watu wote wanatumia nishati ya gesi, kampuni ya ORYX imewekeza kwa kiwango kikubwa kwenye maghara ya uhifadhi na mitambo ya kujaza gesi nchi nzima.Hatutarajii kusikia tena uhaba wa gesi ya kupikia nchini na hatutarajii kabisa watumiaji wa gesi wanarejea kwenye mkaa na kuni kwa kukosa nishati hii ya gesi hapa nchini,"amesema.

Pia Jeffrey amesema kuwa Mkaa ni gharama hasa kwa wakazi wa mijini na kuongeza hivi sasa gunia la mkaa kwa wakazi wa Dar es salam limefikia Sh.70,000 na wengi wanalalamika kuwa mkaa haumalizi mwezi.

"Sisi tunawapa mtungi wa gesi wa kilo 15 ambao kwa familia ya watu saba wanaotumia gesi pekee huweza kutumia kati ya siku 30 hadi 40. Mbali na faida za gharama ndogo,gesi yetu pia ni salama kwa afya ya mtumiaji na usafi wa mazingira ambapo tusingeanza usambazaji mkubwa wananchi wangepaswa kuweka bajeti nyingine za matibabu ya madhara ya moshi mwilini na ukarabati wa nyumba ambazo huchafuka sana kutokana na matumizi ya kuni na mkaa,"amesema

Amesema kampuni yao ya ORYX imetoa shukurani kwa wananchi kwa muitikio mkubwa wa matumizi ya gesi kila siku inayoenda. "Muitikio mkubwa umeonekana hasa pale ongezeko la watumiaji wengi wapya nchi nzima wakinunua mitungi mipya ya gesi ya ORYX kwa matumizi yao,"amefafanua.

Mkuu wa Kitengo cha Mauzo ORYX GAS,Jeffrey Nasser akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) juu yakuelimisha wananchi umuhimu wa kutunza mazingira kwa kuwapa nishati mbadala ya gesi ya kupikia kwa gharama nafuu ukilinganisha na nishati ya mkaa ambayo inachochea uharibifu wa miti na mazingira.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (Kulia) akimzikiliza Menejacha wa Maendeleo ya Biashara Oryx Gas,Mohamed Mohamed ambabo akifafanua juu ya kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kutunza mazingira kwa kuwapa nishati mbadala ya gesi ya kupikia kwa gharama nafuu ukilinganisha na nishati ya mkaa ambayo inachochea uharibifu wa miti na mazingira,leo jijini Dar as Salaam katika kilele cha maadhimosho ya wiki ya mazingira Duniani.

Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamii

No comments:

Post a Comment

Pages