Afisa
Mkuu wa Fedha wa benki ya Exim Tanzania Bw. Selemani Ponda
(katikati)akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam jana wakati akitoa taarifa ya mapato ya benki hiyo katika
kipindi cha robo mwaka kilichoisha mwezi Juni mwaka huu. Wengine ni Naibu Afisa
Mkuu wa Fedha wa benki hiyo Bw. Issa Hamisi (wa kwanza kushoto) na
Meneja Mwanadamizi wa utafiti na uchambuzi wa biashara wa benki hiyo Bw.
Joseph Mrawa (wa kwanza kulia)
Afisa
Mkuu wa Fedha wa benki ya Exim Tanzania Bw. Selemani Ponda (wa kwanza
kulia)akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam jana wakati akitoa taarifa ya mapato ya benki hiyo katika
kipindi cha robo mwaka kilichoisha mwezi Juni mwaka huu. Wengine ni Naibu Afisa Mkuu wa Fedha wa benki hiyo Bw. Issa Hamisi (katikati) na Mkaguzi Mkuu wa ndani wa hesabu za benki hiyo Bw. George Binde
Benki
ya Exim Tanzania imefanikiwa kujipatia faida ya sh. bilioni 12.79
(kabla ya kodi) katika kipindi cha robo mwaka kilichoisha mwezi Juni
mwaka huu, takwimu zinazoonyesha ongezeko la faida kwa asilimia 69
katika benki hiyo.
“Ongezeko
hilo ni kubwa ikilinganishwa na faida yash.bilioni 7.56 tuliyoiopata
katika robo mwaka iliyotangulia na hivyo basi tunajisikia fahari
kutangaza faida hii mbele yenu,’’ alibainisha Afisa Fedha Mkuu wa benki
hiyo Bw. Selemani Ponda alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam jana.
Kwa
mujibu wa Bw Ponda faida hiyo pia ni sawa ongezeko la asilimia 28
ikilinganishwa na faida ya kiasi cha sh. bilioni 13.96 katika kipindi
cha miezi sita kwa mwaka uliopita.
“Katika
robo mwaka hii iliyoisha mwezi Juni, jumla ya mapato kwenye faida
itokanayo na riba ilikuwa kwa asilimia 26 hadi kufikia sh. bilioni 17.9
ongezeko lilichangiwa na gharama nafuu ya amana zetu sambamba na
usimamizi bora wa fedha,’’ alibainisha.
Zaidi
Bw. Ponda alisema katika kipindi hicho faida isiyotokana na riba
ilikuwa kwa asilimia 43 hadi kufikia kiasi cha sh. bilioni 12.3 kutoka
sh. bilioni 8.6 iliyorekodiwa katika mwaka uliopita.
Benki
hiyo pia ilikuwa na mapato mgao kutokana na uwekezaji wenye ukubwa
kiasi cha sh. bilioni 2.3 ikilinganishwa na kiasi cha sh. bilioni 2
kilichorekodiwa katika kipindi kama hicho mwaka jana.
"Nguvu
ya ukuaji wa mapato inaoyesha mafanikio ya Benki.. Tunaendelea
kuboresha ufanisi katika uendeshaji na utoaji wa huduma zetu ili
kuwaridhisha zaidi wateja wetu. Kwa ripoti hii matokeo yanaonyesha
kwamba Exim tumeonyesha utendaji bora hasa kwa kuhusisha rasilimali watu
na technolojia iliyo bora zaidi "aliongeza.
0 Comments