VODACOM NA MONEYGRAM WASAINI MKATABA WA MAKUBALIANO WA KUTOA HUDUMA ZA KIFEDHA


 Ofisa Mkuu wa Idara ya huduma za biashara za M-Pesa wa Vodacom Tanzania,Jacques Voogt akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa hafla ya Uzinduzi  wa makubaliano ya ushirikiano wa kutoa huduma ya kutuma na kupokea fedha kwa njia ya M-pesa na Moneygram (Moneygram M-Pesa)ambayo itawanufaisha wateja wanaoishi Nje ya nchi kutuma fedha na kuingia moja kwa moja kwa jamaa zao waliopo nchini.Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.
003.Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo ya Kitaifa wa Benki kuu ya Tanzania(BoT)Bernard Dadi(katikati) na Makamu wa Rais wa Moneygram Afrika,Herve Chomel(kulia)wakimshuhudia Ofisa Mkuu wa Idara ya huduma za biashara za M-Pesa wa Vodacom Tanzania,Jacques Voogt(kushoto)akisaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa kutoa huduma ya kutuma na kupokea fedha kwa njia ya M-pesa na Moneygram(Monegram M-Pesa)ambayo itawanufaisha wateja wanaoishi Nje ya nchi kwa kutuma fedha na kupokea  moja kwa moja kwa jamaa zao waliopo nchini, Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo ya Kitaifa wa Benki kuu ya Tanzania(BoT)Bernard Dadi(katikati) akiwashuhudia Ofisa Mkuu wa Idara ya huduma za biashara za M-Pesa wa Vodacom Tanzania,Jacques Voogt(kushoto) na Makamu wa Rais wa Moneygram Afrika,Herve Chomel(kulia)wakipongezana mara baada ya kusaini  mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa  kutoa huduma ya kutuma na kupokea fedha kwa njia ya M-pesa na Moneygram(Moneygram M-Pesa)ambayo yatawanufaisha wateja wanaoishi Nje ya nchi kwa kutuma fedha na kupokea  moja kwa moja kwa jamaa zao waliopo nchini, Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Moneygram Afrika,Herve Chomel(kushoto) na Ofisa Mkuu wa Idara ya huduma za biashara za M-Pesa wa Vodacom Tanzania,Jacques Voogt,wakiteta jambo wakati  wa hafla ya Uzinduzi  wa makubaliano yaushirikiano wa  kutoa huduma ya kutuma na kupokea fedha kwa njia ya M-pesa na Moneygram (Moneygram M-Pesa)ambayo itawanufaisha wateja wanaoishi Nje ya nchi kutuma fedha na kuingia moja kwa moja kwa jamaa zao waliopo nchini.Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam.


  Mkurugenzi wa Mifumo ya Malipo ya Kitaifa wa Benki kuu ya Tanzania(BoT)Bernard Dadi(kulia) akijibu maswali kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa ushirikiano wa kutoa huduma ya za kutuma na kupokea fedha kupitia njia ya M-pesa na Moneygram(Monegram M-Pesa)kati ya Vodacom Tanzania na  Moneygram huduma hizo zitawanufaisha wateja wanaoishi Nje ya nchi kwa kutuma fedha na kupokea  moja kwa moja kwa jamaa zao waliopo nchini, Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam. ,Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa Moneygram Afrika,Herve Chomel na  Ofisa Mkuu wa Idara ya huduma za biashara za M-Pesa wa Vodacom Tanzania,Jacques Voogt.
Makubaliano mapya yanawawezesha wateja kupokea pesa moja kwa moja kwenye akaunti za M-Pesa nchini Tanzania.

DAR ES SALAAM (Agosti 25, 2015) —Kampuni ya MoneyGram inayotoa huduma za kutuma pesa duniani na kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania zimetangaza kwamba wateja wa Vodacom sasa wanaweza kupokea pesa moja kwa moja kwenye akaunti zao za M-Pesa. Kwa sasa, kuna watumiaji wa huduma ya M-Pesa zaidi ya milioni saba nchini Tanzania ambao hufanya miamala ya zaidi ya trilioni mbili kila mwezi.

Ushirikiano huo mpya utawawezesha Watanzania wanaoishi nje ya nchi kutuma fedha moja kwa moja kwa ndugu na jamaa zao hapa nchini ambao ni wateja wa M-Pesa kwa njia rahisi, inayofaa, salama na haraka zaidi. Hatua hiyo itafungua uwezekano wa kukuza utumaji pesa kwenda Tanzania, ambao kwa sasa ni umefikia dola za Marekani bilioni 1.2.

Uzinduzi huo ulifanyika wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, ambapo pia ulihudhuriwa na Herve Chomel, Makamu wa Rais wa MoneyGram Upande wa Mauzo Kanda ya Afrika na Jacques Voogt, Ofisa Mkuu wa wa Idara ya biashara ya huduma za M-Pesa wa Vodacom Tanzania.

“Kampuni ya MoneyGram inafurahi sana kufanyakazi na Vodacom kutoa huduma ya haraka, uhakika na salama  kwa mamilioni ya wateja watakaotuma na kupokea pesa,” alisema Chomel. “Vodacom M-Pesa tayari imesaidia kuongeza huduma za utumaji pesa kwa gharama nafuu kwa mamilioni ya watu wa makundi mbalimbali nchini Tanzania na ushirikiano huu mpya utawawezesha zaidi watu walio vijijini na mijini kupokea pesa kutoka kwa marafiki na jamaa zao wanaoishi nje ya nchi.”
Aliongeza kusema, “MoneyGram inaendelea kukua Afrika yote kutokana na uhusiano mzuri ilionao na kampuni za mtandao wa simu, mabenki, ofisi za posta, watoahuduma za rejareja ili kuwapa kipaumbele zaidi wateja wetu. Kwa sasa, MoneyGram inatoa huduma zake kwa zaidi ya nchi 200 huku ikiwa na mtandao wa za mawakala zaidi ya 350,000 kote duniani ambapo 25,000 wanatoka Afrika.”

“Uhusiano huu mpya na MoneyGram unatuwezesha kuingiza nchini dola za Marekani bilioni 1.2 kwa wateja wetu kila mwaka, anasema Voogt. “Utawarahisishia zaidi na kuwezesha familia na marafiki kupokea pesa kupitia M-Pesa. Hii ni njia mojawapo tunakwenda mbali zaidi kwa ajili ya wateja wetu.”




Wateja wa M-Pesa nchini Tanzania wanaweza kupokea pesa kutoka MoneyGram moja kwa moja kwenye akaunti za simu zao kutoka kwa wateja katika nchi zaidi ya 120 kwa saa 24 kwa siku, siku 7 kwa wiki na siku 365 kwa mwaka kulingana na mfumo uliopo. Wateja wanaoishi nchini Marekani wanaweza kutuma pesa kwenda kwenye akaunti za M-Pesa kwa haraka na usalama zaidi  kutoka kwa wakala wa MoneyGram au MoneyGram kwa njia ya mtandao.

No comments:

Post a Comment

Pages