NMB YAKABIDHI MSAADA WA MADAWATI HAI


Meneja wa benki ya NMB tawi la Hai, Medadi Malisa (kulia) akimkabidhi mwalimu mkuu wa shule hiyo Teodora Mlayi huku akishuhudiwa na mgeni rasmi Zuhura Chikira ambaye ni katibu tawala wa wilaya ya Hai.
Meneja wa Benki ya NMB wilaya ya hai Medadi malisa Kushoto akiwa amekaa kwenye madawati yaliyotolewa msaada na benki hiyo kwa shule ya msingi kambi ya Raha, kulia kwake ni Afisa Elimu wa wilaya hiyo Deogracia Mapunda akifuatiwa na katibu tawala Zuhura Chikira na mwenyekiti wa shule hiyo.

 Na Woinde Shizza,Hai

 BENKI ya NMB kanda ya Kaskazini imetoa msaada wa madawati 50 wenye thamani ya sh. milioni 5 katika shule za msingi Kambi ya Raha,iliyomo wilayani humo,huku msaada huo ukitokana na faida inayopata benki hiyo.

 Akiongea jana baada ya kukabidhi msaada huo,meneja wa benki hiyo tawi la Hai mkoa Kilimanjaro, Medadi Malisa alisema benki hiyo imeamua kutoa msaada huo kulingana na uhitaji wa shule hiyo baada ya kupokea maombi kutoka kwa viongozi wa shule hiyo.

 Alisema Benki ya NMB imekuwa ikipokea maombi mengi ya uhitaji wa msaada kwa jamii lakini kwa kuzingatia na umuhimu wa eneo husika ndio maana imefikia uwamuzi wa kutoa madwati katika shule hiyo baada ya kutambua kuwa kuna haja ya kusaidia wanafunzi hao.

 ‘’ Benki ya NMB imeamua kutoa msaada wa madawati 50 kutokana na uhitaji wa shule husika napenda niwahakikishie kuwa benki yenu imetenga zaidi ya shilingi bilioni 1 kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya wananchi ikiwemo kusaidia sekta ya Afya, Elimu na michezo,’’alisema Malisa.

 Aliongeza kuwa kuwa,benki hiyo iliamua kutoa msaada wa madawati hayo ya wanafunzi ili kuweza kutoa motisha kwa wanafunzi hao kuweza kusoma kwa bidii kwa madai kuwa kutokuwepo kwa vitendea kazi mashuleni ni moja ya sababu zinazopelekea wanafunzi wengi kufeli.

 "Msaada huu wa madawati umetokana na faida kidogo ambazo benki inapata hivyo tumeona katika faida hizo ni jambo jema kutoa msaada wa aina hii kwa ajili ya kuweza kuendeleza watoto kielimu kwani wao ndiyo Taifa la kesho," alisema Malisa.

 Kwa upande wa Katibu tawala wa Wilaya ya Hai Zuhura Chikira, ambaye alimwakilkisha mkuu wa wilaya ya Hai aliipongeza benki ya NMB kwa kutoa msaada huo na kuwataka wadau wengine wa elimu kuiga mfano wa benki hiyo kwa kutoa mchango kama huo ili kupunguza ya madawati wilayani huo.

 Alisema wilaya ya Hai inakabiiwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya upungufu wa madawati hata hivyo alisema taitizo hilo lipo kwa baadhi ya shule za msingi na wilaya ipo kwenye mkakati wa kukabiliana nalo. Aliwataka wadau wengine wa elimu kuiga mfano wa benki ya NMB,kwa kuisaidia serikali kupunguza changamoto zilizopo kwenye shule mbalimbali hapa nchini hasa za msingi ambako ndiko tatizo kubwa lilipo.

No comments:

Post a Comment

Pages