NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
BENKI
ya Walimu, (Mwalimu Commercial Bank Plc-MCB)), iko mbioni kuanzisha huduma ya
uwakala wa benki ambapo itashirikiana na mawakala wa sehemu mbalimbali nchini
ili kuhakikisha inafikisha huduma za kibenki kwa wananchi wote kwa urahisi, uhakika na unafuu.
Hayo
yamesemwa Juni 22, 2017, mkoani Morogoro na Mwneyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi
ya benki hiyo, Bw.Herman Mark Kessy, (pichani), kwenye Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Wanahisa
wa benki hiyo.
Aidha
Mwenyekiti huyo aliwaambia wajumbe wa mkutano huo kuwa, benki hiyo pia iko
katika mpango wa kutumia huduma za ATM
bila ya kadi (Cardless), huduma ambayo itasaidia sana wateja kutumia ATM hata
bila ya kuwa na kadi.
“Kupitia
huduma hii, wateja wataweza kupata pesa zao kupitia mawakala au kupakua programu
maalum kwenye simu zao za kiganjani zitakazowezesha kulipa huduma za maji,
umeme pia kutuma pesa kutoka kwenye akaunti zao kwenda kwenye huduma maalum ya
benki kwa njia ya simu.” Alifafanua.
Akizungumzia
hali ya taasisi za kifedha nchini, Bw.Kessy alisema, MCB iko imara licha ya
changamoto zilizojitokeza hivi karibuni kufuatia agizo la serikali kuelekeza
taasisi zake zote za serikali na umma kuhamisha na kupeleka fedha zote Benki
Kuu na hivyo wateja wakubwa wa serikali walifunga akaunti zao na kuhamishia
fedha zao BoT hali iliyosababisha ukwasi mkubwa.
“Lakini
sio hilo katika zoezi la serikali la uhakiki wa watumishi wa umma, ilibaini
watumishi hewa 19,000 na wakati zoezi hilo likiendelea kwa zaidi ya siku 90 urejeshaji
wa makato ulisitishwa, hivyo basi mabenki ikiwemo benki yetu hatukupata
marejesho ya mikopo kutoka kwa wafanyakazi walioathiriwa na zoezi hilo na pia
kukosa mapato yatokanayo na riba ya mikopo hiyo.” Alisema.
Mwenyekiti
huyo wa bodi aliwaambia wajumbe wa mkutano huo kuwa changamoto nyingine ni
sheria inayotaka mabenki ili yaweze kufanya miamala ya fedha za kigeni nje ya
nchi zinatakiwa kua na benki washirika ili kupitisha miamala hiyo.
“Kutokana
na sheria hiyo, benki za Marekani zimeweka utaratibu mgumu kuhusu ushirikiano na
mabenki ya nje, hivyo benki ndogo na za kati zimeshindwa kutimiza masharti ya
kupata benki mshirika (Correspondence Banking), kutokana na hilo benki nyingi
ndogo na za kati zimepoteza biashara na wateja.” Alifafanua Bw. Kessy.
Hata
hivyo Bw. Kessy alisema pamoja na misukosuko hiyo, benki ya MCB imeendelea
kufanya vizuri katika kuongeza wateja licha ya kuwa ngeni kwenye soko, ambapo
hadi kufikia Juni, 2017 wateja wenye
akaunti za akiba wamefikia 28,576 zenye thamani ya shilingi bilioni 5.3 huku
idadi ya wateja wa mikopo ikifika 228 wenye thamani ya shilingi bilioni 3.1 na
kwamba benki imeweza kuwafikia wateja katika sehemu mbalimbali za nchi.
Kuhusu
mahusiano ya kibiashara na wanahisa waanzilishi wa benki hiyo, Bw. Kessy
alisema, benki iemendelea kuimarisha uhusino wake na Chama cha walimu, pamoja
na Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Umma (PSPF).
“Mahusinao
haya yamewezesha kuwapa wachangiaji wa Chama Cha Walimu, (CWT), mikopo yenye
riba nafuu, vilevile tuko katika mkakati wa kushirikiana na PSPF kutoa mikopo
ya riba nafuu kwa wanachama wake, hii yote ni katika kuwasaidia watumishi wa
Umma kujikwamua kiuchumi na kuwa na maisha bora,” alisema.
Katika
mkutano huo wa siku moja wajumbe watapokea taarifa na kuzijadili ambazo ni
pamoja na taarifa ya fedha kwa kipindi cha mwaka 2016, kupitisha majina ya
wakurugenzi wa bodi yaliyopendekezwa, kujadili na kupitisha posho za
wakurugenzi, kujadili na kupitisha wakaguzi wan je wa benki kwa mwaka 2017 na
pia kujadili na kupitisha mabadiliko yanayopendekezwa ya kubadilisha makala ya
muundo, (MEMARTs) za kampuni.
Wajumbe wa mkutano huo wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa
Afisa Mtednaji Mkuu wa MCB, Ronald Manongi akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huo
Wajumbe wakifuatilia kwa utulivu mkutano huo
Bw. Manongi
Mkuu wa kitengo cha Hazina MCB, Nunu R. Saghal (kushoto), akijadiliana jambo na Mkuu wa kitengo cha fedha cha benki hiyo, Selemani Kijori
|
Ambrose
Mshula mjumbe wa bodi ya wakurugenzi MCB, (aliyesimama), akizungumza
kwenye mkutano huo. Wengien kutoka kushoto, ni Mshauri wa ksiheria wa
benki, Upendo Ngaponda, Afisa Mtendaji Mkuu wa MCB, Ronald Manongi,
Mkurugenzi wa bodi ya benki, Said Kambi, Mwenyekiti wabodi ya
wakurugenzi, Herman Kessy, George Fumbuka mwangalizi wa hisa na
Mkurugenzi wa kampuni ya kimataifa ya ukaguzi wa mahesabu
Ernst&Young, Deokan Mkenda
|
|
Mshauri wa kisheria wa MCB, Upendo Ngaponda akizungumzia |
Katibu wa CWT Manispaa ya Morogoro, Abubakar Rashid, (kushoto), na Mkuu wa kitengo cha ukuzaji biashara na masoko benki ya MCB, Valence Lutenganya, wakitazama kitu kwenye kompyuta
Mjumbe akijisajili
Maafisa wa juu wa benki ya MCB, kutoka kushoto, Charles Shedrack, Frederick Rwabukambara, Valence Lutenganya, na Selemani Kijori, wakijadiliana jambo
Afisa Mtendaji Mkuu wa MCB, Ronald Manongi, (kushoto), akisalimiana na mwakilishi wa Mfuko wa Afya ya Jamii, (NHIF) Yasin Mwakababu. NHIF ni mmoja wa wanahisa wakubwa wa benki
Msaidizi wa Afisa Mtendaji Mkuu wa MCB, Furaha Johnson, (kushoto), akiongozana na mmoja wa wakurugenzi wa benki hiyo, Dkt. Fidea Luhwano Mgina
Wajumbe wakichukua makabrasha tayari kwa mkutano
Wajumbe wakichukua makabrasha tayari kwa mkutano
Wajumbe wakiwa kwenye mkutano na wengine wakipitia taarifa mbalimbali
Mjumbe akipitia taarifa
Wajumbe wakijisajili
Mjumbe akielekea ukumbini
Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Walimu
(Mwalimu Commercial Bank Plc-MCB), Bw.Herman Mark Kessy, (katikati),
akiongozana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Walimu Tanzaia, Bw.Yahya
Msulwa,(Kushoto) na Aifisa Mtendaji Mkuu wa MCB, Bw.Ronald Manongi..
0 Comments