TRA YAVIFUNGIA VITUO VYA MAFUTA VISIVYOTUMIA MASHINE ZA KIELEKTRONIKI JIJINI DAR ES SALAAM


Cathbert Kajuna-Kajunason Blog

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imevifungia vituo zaidi ya 10 jijini Dar es Salaam kwa kosa la kuendesha biashara bila mashine ya Kielektroniki.


Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa zoezi la kufungia vituo mbalimbali, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere amesema kuwa kwa sasa zoezi hilo linaendelea nchi nzima ili kuumbua vituo vyote vinavyokwepa kulipa kodi.


"Tuliwapa muda wafunge mashine hizo mpaka mwaka jana 2016 mwishoni lakini mpaka sasa hawajatekeleza agizo hilo hivyo hatuna budi kuvifunga hivyo vituo mpaka pale watakapotekeleza matakwa ya serikali," amesema Kamshna Kichere.


Kwa upande wa Kamishna wa Mapato ya ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya amesema wakati umefika kwa wafanyabiashara kufuata makubaliano wanayokuwa wakiwafanya na TRA ili kuepuka usumbufu unaojitokeza kwa sasa. Ameongeza kuwa sheria kali zitachukuliwa kwa wafanyabiashara wote ambao vituo vyao vya mafuta vimefungwa na wakakaidi. Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere (mwenye miwani kulia) akimuhoji msimamizi wa kituo cha GBP cha Sinza Mori jijini Dar es Salaam mara baada ya kufika kwa ajili ya zoezi la kukifungia kituo hicho kwa kukosa kuwa na mashine za kielektroniki. Wengine ni wafanyakazi wa TRA walioambatana nae.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere (aliyenyoosha mkono) akiwahimiza vijana wake wafunge kituo hicho.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere (kushoto) akiwa na Kamishna wa Mapato ya ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Elijah Mwandumbya (kulia) wakitoa msisitizo.

Kituo cha GBP kikiwa kimeshafungwa.


Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere akikagua mashine za kituo cha PUMA kilichopo Mwenge jijini Dar es Salaam ambapo alikuta mashine zake za kielektroniki zipo salama.

Kituo cha KOBIL kilichopo karibu na TCRA, Sinza kikiwa kimefungwa.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere (mwenye tai nyekundu) akimuhoji meneja wa kituo cha OIL COM kilichopo Mwenge mkabala na Vinyago jijini Dar es Salaama kabla hajakifunga.

Kituo cha OIL COM kilichopo Mwenge mkabala na Vinyago jijini Dar es Salaamakikiwa kimefungwa.

Mfanyakazi wa TRA akifunga kituo cha OIL COM Ubungo jijini Dar es Salaam.

Kituo cha OIL COM Ubungo jijini Dar es Salaam kikiwa kimefungwa. Kituo cha TSN - Mwenge kikiwa kimefungwa.

Kituo cha OIL COM Njia Panda ya Mabibo jijini Dar es Salaam kikiwa kimefungwa.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere akihakikisha jinsi mashine za kituo cha LAKE OIL kilichopo njia panda ya Mabibo jijini Dar es Salaam kabla hakijafungwa.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Edward Kichere akimkabidhi risiti mteja aliyefika kuweka mafuta kituoni hapo.

Post a Comment

0 Comments