MAKAMU WA RAIS AWATAKA WAKAZI WA KIZIMKAZI KUWA NA BIMA YA AFYA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewahimiza wakazi wa Kizimkazi kujiandikisha Bima ya Afya kwani ndio mfumo ambao utawawezesha kupata matibabu haraka na kwa gharama ndogo.


Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa Sherehe ya Siku ya Wakizimkazi ambapo siku hiyo wakazi hao hukutana na kupeana taarifa za maendeleo na kupanga mipango ya baadae kasha kula chakula cha asili pamoja na michezo ya asili.Mhe. Samia aliwaeleza wananchi hao kuwa hakutokuwa na mjomba atakayekuja kuwaletea maendeleo na alihimiza kwa kusema “Maendeleo ya Kizimkazi yataletwa na Wakizimkazi wenyewe”.


Katika Sherehe hizo Makamu wa Rais alifungua jengo la Ofisi ya Saccos ya Mkombozi lililopo Kizimkazi Dimbani na Kukagua maendeleo ya Ukumbi wa Skuli ya Sekondari Kizimkazi.Mchezo wa Kuvuta ,kusokota kamba, kukuna nazi na mbio za Ngalawa zilionekana kuvutia watu wengi.


Makamu wa Rais alihimiza wanamichezo kujitokeza kwa wingi mwakani kwani michezo hudumisha umoja na kuleta mshikamano katika jamii.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria ufunguzi wa jingo la Mkombozi Saccos lililpo Kizimkazi Dimbani wakati wa Sherehe za Siku ya Wakizimkazi


Viongozi na Wageni mbali mbali walijumuika kula chakula cha asili cha Wakizimkazi wakati wa shrehe ya Siku ya Wakizimkazi.

Mashindano ya kukuna nazi yawa kizutio wakati wa Sherehe za Siku ya Wakizimkazi.

Mashindano ya kusokota kamba

Vijana kutoka Kusini mwa Kizimkazi wakivuta kamba wakishindana na vijana wa kaskazini wakati wa sherehe za Siku ya Wakizimkazi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa Sherehe za Siku ya Wakizimkazi iliyofanyika kwenye uwanja wa Maulid, Kizimkazi, Wilaya ya Kusini mkoa wa Kusini, Unguja.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Bw. Sudi Simba ambaye alifika Kizimkazi kutambulisha huduma ya bima ya Afya ya Afya Wote wakati wa Sherehe za Siku ya Wakizimkazi iliyofanyika kwenye uwanja wa Maulid, Kizimkazi, Wilaya ya Kusini mkoa wa Kusini, Unguja.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia vipeperushi vyenye taarifa ya huduma ya bima ya Afya ya Afya Wote wakati wa Sherehe za Siku ya Wakizimkazi iliyofanyika kwenye uwanja wa Maulid, Kizimkazi, Wilaya ya Kusini mkoa wa Kusini, Unguja.

Wakazi wa Kizimkazi wakiangalia ngalawa 15 zikichuznz vikali ikiwa sehemu ya sherehe ya siku ya Wakizimkazi

Wananchi wakimpokea mshindi wa pili katika mashindano ya Ngalawa kijana Ahmed Yusufu Hassan ambaye ngalawa yake ameipa jina la Ndio Mambo

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa mkono wa pongezi kijana aliyeshinda kwenye mashindano ya Ngalawa Bw. Ali Khamisi Mgeni akiwa na chombo chenye jina la Sea Never Dry.

Post a Comment

0 Comments