Let's Talk Business / Tuongee Biashara Pekee.

Habari Mpya

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, December 21, 2017

SHIRIKA LA POSTA NCHINI LAZINDUA NEMBO MPYA YA SHIRIKA HILO YENYE KAULI MBIU YA TWENZETU

Naibu Waziri Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa akizindua nembo mpya ya Shirika la Posta nchini ambayo imezinduliwa leo jijini Dar es Salaam katika Kuboresha huduma za shirika hilo kuwa la kisasa.

Naibu Waziri Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa, akimpongeza Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta nchini, Dr Haroun Kondo mara baada ya kuzindua nembo mpya ya shirika hilo jijini Dar es Salaam leo

Naibu Waziri Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa akishuka katika mabasi mapya ya Shirika la Posta nchini mara baada ya kuzindua huduma ya mabasi ya shirika hilo ambayo yatakuwa yanabeba abiria na vifurushi

Naibu Waziri Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa, akizungumza mara baada ya kuzindua Nembo mpya ya Shirika la Posta nchini

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta nchini, Dr Haroun Kondo akizungumza kabla yakumkaribisha mgeni rasmi kuzindua nembo mpya ya shirika la Posta nchini.

Mjumbe wa bodi ya Shirika la Posta nchini, Khadija Khamis Shabani akitoa neno la shukrani mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa nembo mpya ya shirika la Posta nchini

Muongozaji wa shughuli ya uzinduzi wa nembo mpya ya Shirika la Posta nchini, Pascal Mayala akizungumza wakati sherehe hizo zikikiendelea.

Naibu Waziri Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta nchini, Dr Haroun Kondo pamoja na Posta Mkuu Hassana Mwang'ombe wakiongozana kwenda kukagua magari

Sehemu ya wafanyakazi wa shirika la Posta nchini wakiwa katika hafla hiyo ya uzinduzi wa nembo mpya ya Shirika la Posta.

Msanii wa Muziki wa kughani kutoka Mjomba Band Mrisho Mpoto akiimba wakati wa uzinduzi wa nembo mpya ya Shirika la Posta Tanzania, Mbali na kuimba mpoto alitumia muda huo kuwaeleza Watanzania juu ya kuwa wazalendo kwa kutumia Barua kama chombo pekee ya kuonesha thamani kwa mtu unayempenda na kumjali, Mpoto amesema kuwa hapo zamani wahenga walitumia Barua kama chombo pekee cha kuonesha namna gani mtu anamjali mwenzie hasa nayakati zile wakiwa wanasoma shule za bweni .

Wasanii wa kundi la Mjomba Band wakitumbuiza wakati wa bendi hiyo ilipokuwa inaimba wakati wa uzinduzi wa nembo mpya ya Shirika la Posta nchini.

Mpiga Drums Maharufu nchini James Kibosho akikaanga chipsi pamoja na Mjomba Band jijini Dar es Salaam leo

Wanamuziki wakicharaza magitaa wakati wa Bendi ya Mrisho Mpoto ilipokuwa inatumbuiza wakati wa uzinduzi wa nembo mpya ya shirika la Posta nchini.

Mpiga kinanda Maarufu nchini Erasto Mashine akipiga kinanda wakati wa Bendi ya Mrisho Mpoto ilipotumbuiza wakati wa uzinduzi wa nembo mpya ya Shirika la Posta.
Msanii wa Muziki wa kughani Kutoka Mjomba Band Mrisho Mpoto akiimba na Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania

Post Top Ad

Your Ad Spot