ACACIA YAFANYA TAMASHA LA AJIRA KUWAPA FURSA WAFANYAKAZI WALIOACHISHWA KAZI MIGODI YA BUZWAGI NA BULYANHULU




Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Acacia kupitia migodi ya dhahabu ya Buzwagi na Bulyanhulu imefanya tamasha la ajira kwa kuwakutanisha waliokuwa wafanyakazi wa migodi hiyo na makampuni zaidi ya 20 kwa ajili kubalishana mawazo na kupeana mawasiliano na taarifa ili wafanyakazi hao wapate kazi.

Tamasha hilo limefanyika leo Jumatano Desemba 20,2017 katika ukumbi wa Umoja uliopo katika mgodi wa Buzwagi uliopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkufunzi katika Idara ya Saikolojia ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dk Chris Mauki.

Akizungumza wakati wa tamasha hilo,Meneja wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu Benedict Busunzu alisema lengo la tamasha la ajira lilioandaliwa na Acacia ni kuwaonesha fursa za ajira waliokuwa wafanyakazi wa kampuni ya Acacia kwa kuwakutanisha na makampuni mbalimbali katika kipindi cha kuelekea kufunga migodi hiyo.

“Tumekutana hapa ili kuonesha fursa za ajira kwa wafanyakazi wetu waliobobea katika kazi za migodini, kuna maisha mengine baada ya mgodi,tumealika kampuni ambayo yanachukua mawasiliano na CV na kama kuna nafasi za ajira basi watapatia ili maisha yaendelee nje ya mgodi”,aliongeza Busunzu.

“Tulialika makampuni zaidi ya 40, 15 yalikubali kushiriki,na 11 leo yamehudhuria,lakini pia wafanyakazi zaidi ya 260 wamehudhuria kwa ajili ya kuonana na makampuni haya,Acacia inaamini tamasha hili litakuwa na mafanikio makubwa tuliyotarajia”,alieleza.

Aidha Busunzu alisema kupitia program yao ‘No Harm 2020’ yenye miradi 10,wamekuwa wakitoa elimu na mafunzo mbalimbali kwa wafanyakazi wao kuhusu namna ya kuishi baada ya kumaliza muda ajira mgodini ambapo wafanyakazi 800 katika mgodi wa Bulyanhulu na 600 katika mgodi wa Buzwagi wamepatiwa mafunzo ya ujasiriamali na ajira.

Kwa upande mgeni rasmi Dk Chris Mauki ambaye ni Mkufunzi katika Idara ya Saikolojia ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam aliipongeza Acacia kwa kuwaandaa wafanyakazi wake kwa kuwapatia mafunzo ya namna ya kuishi baada ya migodi kufungwa huku akiwataka kukubali mabadiliko na kuthubutu kufanya kazi nyingine badala ya kukata tamaa.

“Mnayo nafasi ya kufanya biashara,kuajiriwa,kujiajiri na kuajiri wengine, ,mnachotakiwa kufanya ni kujitambua,kukubali mabadiliko,kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha,muishi maisha ya kuokoa muda,kuweni na mahusiano mema na watu wanaowazunguka na hapo ndipo mtakubaliana nami kuwa kuna maisha baada ya mgodi”,aliongeza Dk. Mauki.

Nao washiriki wa tamasha hilo waliishukuru Acacia kuwakutanisha na makampuni hayo kwani wamewapa urahisi wa kutafuta kazi kwa kukutana na waajiri moja kwa moja na kuwapatia taarifa zao (CV).

Nayo makampuni hayo yalisema Acacia ina wafanyakazi wazoefu na waliobobea katika kazi za migodini hivyo yanaamini yatapata wafanyakazi wazuri watakaowatumia kwenye makampuni yao.

“Acacia ni kampuni kubwa ya kimataifa, hii ni sehemu nzuri ya kupata wataalamu wanaojua kazi vizuri”,alisema Kaimu Meneja rasilimali watu kutoka shirika la Madini la taifa- STAMICO Lameck Kabeho na Jolene Ngaluko Mtalo kutoka Wakala wa ajira. –CV People Africa.

Naye Meneja wa Huduma na Mahusiano wa Acacia, Elias Kasitila alisema mpaka sasa wafanyakazi 3000 wameachishwa kazi katika migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu na zoezi la kupunguza wafanyakazi bado linaendelea katika mgodi wa Buzwagi hivyo idadi itaongezeka.

Kasitila aliyataja makampuni yaliyoshiriki katika tamasha hilo kuwa ni Twiga Cement,Mantrac Tanzania Ltd,Northern Engineering,SAO Hill,Shanta Gold mine,IMED,LINDAM,CV People,Junior Construction,Sandvick na STAMICO.

Mgeni rasmi Mkufunzi katika Idara ya Saikolojia ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dk Chris Mauki akizungumza katika Tamasha la Ajira lililoandaliwa na Kampuni ya Uchimbaji madini ya dhahabu ya Acacia lililofanyika leo Jumatano Desemba 20,2017 katika mgodi wa Buzwagi na kukutanisha pamoja makampuni zaidi ya 10 na wafanyakazi zaidi ya 260 walioachishwa kazi katika mgodi wa Buzwagi na Bulyanhulu wakati Acacia ikielekea kufunga migodi hiyo.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog



Dk Chris Mauki akizungumza katika Tamasha hilo la Ajira.Kulia ni Meneja wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu Benedict Busunzu.
Meneja wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu Benedict Busunzu akielezea lengo la kufanya tamasha la ajira lililokutanisha pamoja makampuni na wafanyakazi wa Acacia ili kupeana fursa za ajira. Kulia Meneja Uendelevu mgodi wa Buzwagi George Mganza,kushoto ni Dk. Chris Mauki.

Meneja wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu Benedict Busunzu akiwasisitiza waliokuwa wafanyakazi wa Acacia kutumia fursa ya tamasha hilo kutafuta maisha nje ya migodi.

Washiriki wa tamasha la ajira wakimsikiliza Meneja wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu Benedict Busunzu

Meneja wa migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu Benedict Busunzu akielezea namna Acacia inavyoendelea kutoa elimu ya ajira na ujasiriamali kwa wafanyakazi wake ili kujiandaa kuanza maisha mengine nje ya migodi.Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Huduma na Mahusiano wa Acacia, Elias Kasitila. Wa kwanza kulia ni Meneja Msaidizi wa Ulinzi katika mgodi wa Buzwagi Allan Bunyan akifuatiwa na Meneja Ulinzi katika mgodi wa Buzwagi Gordon Surgeon

Washiriki wa tamasha la ajira wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea

Meneja wa Huduma na Mahusiano wa Acacia, Elias Kasitila akielezea kuhusu tamasha la ajira ambapo alisema zaidi ya makampuni 40 yalialikwa kushiriki tamasha hilo, makampuni 15 yakakubali kushiriki na leo makampuni 11 yamekutana na wafanyakazi wa Acacia zaidi ya 260 walioachishwa kazi katika migodi hiyo.

Kasitila alisema mpaka sasa wafanyakazi 3000 wameachishwa kazi katika migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu hivyo wanafanya jitihada za kuhakikisha wafanyakazi hao wanapata fursa za ajira sehemu zingine ili maisha yaendelee

Mtaalamu wa Mawasiliano Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi Mary Lupamba akitoa maelekezo kwa washiriki wa tamasha hilo la ajira

Tamasha linaendelea

Washiriki wa tamasha hilo wakiwa eneo la tukio

Tamasha linaendelea

Washiriki wa tamasha wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea



Tamasha linaendelea





Tamasha linaendelea





Washiriki wa tamasha hilo wakiwa eneo la tukio





Waliokuwa wafanyakazi katika migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu wakiwa katika ukumbi wa Umoja katika mgodi wa Buzwagi kwa ajili ya kutembelea vibanda vya makampuni yaliyoshiriki katika tamasha la ajira kwa ajili ya kupata mawasiliano na kutoa taarifa zao (CV) kutafuta fursa za ajira





Waliokuwa wafanyakazi katika migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu wakiwa katika banda la shirika la Madini la taifa- STAMICO,wakisikiliza maelezo kutoka Kaimu Meneja rasilimali watu wa shirika hilo,Lameck Kabeho





Waliokuwa wafanyakazi wa Acacia wakiwa katika banda la Shanta Gold Mine kutafuta fursa za ajira





Hapa ni katika banda la kampuni ya Sandvik,kulia ni aliyekuwa mfanyakazi wa Acacia akiuliza jambo





Mfanyakazi wa Mantrac Tanzania Ltd akimsikiliza kwa makini mmoja wa waliokuwa wafanyakazi wa Acacia





Hapa ni katika banda la LINDAM huduma kwa waliokuwa wafanyakazi wa Acacia inaendelea


Ndani ya ukumbi wa Umoja washiriki wa Tamasha la ajira wakibadilishana mawazo



Kulia Mfanyakazi wa CV People,Jolene Ngaluko akimsikiliza kwa makini mmoja wa waliokuwa wafanyakazi wa Acacia aliyeamua kupeleka CV yake kwa ajili ya kutafuta fursa za ajira
Wafanyakazi wa CV Peole Africa wakiendelea kukusanya CV kwa kuziweka kwenye Laptop



Waliokuwa wafanyakazi wa Acacia wakiangalia CV walizokuja nazo kwenye tamasha la ajira kwa ajili ya kuzikabidhi kwenye makampuni



Waliokuwa wafanyakazi wa Acacia wakibadilishana mawazo



Meneja Msaidizi wa Ulinzi katika mgodi wa Buzwagi Allan Bunyan (kulia) na Meneja Ulinzi katika mgodi wa Buzwagi Gordon Surgeon wakifurahia jambo katika ukumbi wa Umoja wakati wa Tamasha la ajira



Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

No comments:

Post a Comment

Pages