Naibu
Waziri Sayansi na Teknolojia January Makamba akizungumza wakati wa
uzinduzi wa kampuni ya na kampuni ya Copyrights Management East Africa
Limited (CMEA).
Afisa
Mtendaji Mkuu wa CMEA, Paul Matthysse akisisitiza jambo wakati wa
uzinduzi wa kampuni hiyo yenye lengo la kuwakwamua wanamuziki katika
umaskini. CMEA pia itawawezeha pia watayarishaji wa muziki na wasanii
wengine pamoja na vyombo vya habari kupata kufahami takwimu sahihi za
nymbo zilizochezwa kwa siku, wiki, mwezi na kwa mwaka.
Mwanamuziki
Mkongwe nchini, John Kitime akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampuni
ya inayojishughulisha na Hakimiliki za kazi za wasanii katika nchi za
Afrika Mashariki ijulikanayo kwa jina la Copyrights Management East
Africa Limited (CMEA).
Meneja
Mradi wa kampuni ya Copyrights Management East Africa Limited (CMEA)
ambayo inasimamia haki miliki za kazi za wasanii wa ukanda wa nchi ya
Afrika Mashariki, Abdi Zagar akielezea jinsi kampuni yao inavyofanya
kazi wakati wa uzinduzi wa kampuni hiyo.
Naibu
Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba akisalimiana na Afisa
Mteandji Mkuu wa Chama Cha Hakimiliki Tanzania, Doreen Sinare wakati w
uzinduzi wa kampuni ya inayojishughulisha na Hakimiliki za kazi za
wasanii katika nchi za Afrika Mashariki ijulikanayo kwa jina la
Copyrights Management East Africa Limited (CMEA). Katikati ni Katibu
Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata), Godfrey Mngereza.
Afisa
Mteandji Mkuu wa Chama Cha Hakimiliki Tanzania, Doreen Sinare wakati w
uzinduzi wa kampuni ya inayojishughulisha na Hakimiliki za kazi za
wasanii katika nchi za Afrika Mashariki ijulikanayo kwa jina la
Copyrights Management East Africa Limited (CMEA).
Naibu
Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba akiwa katika “red
carpet’ wakati wa uzinduzi wa kampuni ya inayojishughulisha na
Hakimiliki za kazi za wasanii katika nchi za Afrika Mashariki
ijulikanayo kwa jina la Copyrights Management East Africa Limited
(CMEA).
Banana
Zorro wa B-Band akiwa na Mwenzake wakati wa uzinduzi wa kampuni ya
inayojishughulisha na Hakimiliki za kazi za wasanii katika nchi za
Afrika Mashariki ijulikanayo kwa jina la Copyrights Management East
Africa Limited (CMEA).
Na Mwandishi Wetu
Naibu
Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba amewataka wanamuziki
nchini kuachana na kutegemea kupata shoo za majukwaani na kupata
umaarufu usiokuwa na tija kwa kujiunga na kampuni ya Copyrights
Management East Africa Limited (CMEA) ambayo inasimamia haki miliki za
kazi za wasanii wa ukanda wa nchi ya Afrika Mashariki.
Naibu
Waziri Makamba alisema hayo wakati wa uzinduzi rasmi wa kampuni ya CMEA
ambayo ipo chini ya mtayarishaji wa muziki maarufu, Paul Matthysse
(P-Funk) ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa kamuni hiyo.
Makamba
alisema kuwa wanamuziki wengi nchini wanapata umaarufu mkubwa wa bila
kipato kutokana na kazi zao bora kwani hawafaidiki na utunzi wa nyimbo
zao zinazopigwa kwenye televisheni na vituo vya redio mbalimbali.
Alisema
kuwa matokeo yake wanapotea katika fani hiyo na kuwa maskini maarufu na
faida kubwa kwao ni kupata sifa kwa warembo mbalimbali ambao huwakimbia
pale wanaposhuka katika fani.
“Mimi
najua muziki na wanamuziki, hakuna mtu anayeweza kunidanganya,
wanamuziki wanapata tabu katika utunzi na baadaye kutafuta fedha za
kurekodi kwa kukopa au kwa kuombaomba, baadaye watafute fedha za kuwapa
madj wa redio na wa vipindi vya televisheni ili wimbo wake uchezwe na
kupata shoo mbalimali kwa kipato kidogo,” alisema Makamba.
Alisema
kutokana na hali ilivyo, mwanamuziki anaishia kukuapata shoo kwa ujira
mdogo na akipotea katika fani, anakuwa maskini maarufu.
“CMEA
ni sululisho kwenu, kampuni hi itafanyakazi pamoja na Chama Cha
Hakimiliki Tanzania (Cosota) kuweza kujua wimbo wako au video yako
imechezwa mara ngapi redioni au kwenye televisheni na unastahili kulipwa
shilingi ngapi,” alisema.
Alisema kuwa hata baada ya kuacha muziki, utaendelea kupata fedha
‘pensheni’ kutokana na wimbo au video yako kuchezwa redioni na kwenye
televisheni.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa CMEA, Paul Matthysse alisema kuwa mbali ya wanamuziki,
kampuni yao itawawezeha pia watayarishaji wa muziki na wasanii wengine
pamoja na vyombo vya habari kupata kufahami takwimu sahihi za nymbo
zilizochezwa kwa siku, wiki, mwezi na kwa mwaka.
Matthysse
alisema kuwa kampuni yao imewekeza mitambo ya kisasa inayowezesha
kuchapisha na kuhakiki nyimbo pindi zinapochezwa hewani na televisheni
na redio na kutoa ripoti za aina mbalimbali zinazohitajika kutumika kwa
malengo maalum.
“Pia
tunapokea na kuhifadhi nyimbo kwenye mitambo maalum kwa matumizi ya
uhakiki, na kudhibiti kiasi cha mirabaha ambacho Cosota kupitia vyombo
vya habari inatakiwa kuwalipa wasanii kulingana na idadi kamili ya
urushwaji wa kazi zao,” alisema Matthysse.
0 Comments