Bayport yazindua huduma ya mikopo kwa njia ya mtandao

Msimamizi wa michezo ya kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Mrisho Milao kulia akipata maelekezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mauzo ya mtandao (Online) wa Bayport Financial Services, Zainabu Kalufya, katika uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo ya haraka kwa njia ya mtandao kwa www.kopabayport.co.tz, uzinduzi uliofanyika leo Makao Makuu ya Bayport, jijini Dar es Salaam. Picha kwa Hisani ya Bayport.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya Kifedhaya Bayport Financial Services, yenye Makao Makuu yake jijini Dar es Salaam, Tanzania, imezindua tovuti yake ya www.kopabayport.co.tz, itakayowezesha wateja wake kupata mikopo ya haraka na kwa njia rahisi.
Kwa kupitia tovuti hiyo, watu mbalimbali wanaweza kupata huduma za Bayport, sanjari na kupata mkopo ndani ya saa 24 baada ya kuidhinishwa, huku akijibiwa ombi lake la mkopo, ndani ya masaa mawili tangu alipojisajiri kwa mara ya kwanza.
Akizungumzia huduma hiyo mpya ya mikopo ya haraka kwa njia ya mtandao jijini Dar es Salaam leo mchana, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema kwamba huduma hiyo sasa itawawezesha wateja wao kukopa mahala popote atakapokuwa, tofauti na awali.

Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services kitengo cha Huduma kwa Wateja, wakiwajibika wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo ya haraka kwa njia ya mtandao onlinewww.kopabayport.co.tz, jijini Dar es Salaam leo.

Alisema kuwa lengo la uanzisha kwa tovuti hiyo ya www.kopabayport.co.tz ni kutokana na kuweka sera ya mikakati ya kuwapatia huduma hiyo watu wengi iliwaweze kukopa na kujikwamua kiuchumi, ikiwa ni maalum kwa watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni zilizoidhinishwa na Bayport.
“Bayport sasa imezidi kupiga hatua, kwa sababu mteja wetu hata kama akiwa nyumbani kwake, kwa kupitia huduma yetu hii anaweza kujisajiri na kukopeshwa anachokihitaji kutoka kwetu bila kupata usumbufu wa aina yoyote.
“Hayani mambo mazuri na naamini ni wakati wa wateja wetu na Watanzania wote kuendelea kuchangamkia huduma zetu za mikopo, ukizingatia ni Bayport pekee inayoweza kukupatia mkopo wa Chagua chochote Bayport italipia, Bima ya Elimu ya Uwapendao, mikopo ya fedha na mingineyo muhimu,” alisema Cheyo.
Naye Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Mrisho Millao, alisema utaratibu wa kukopa kwa njia ya Internet kutoka Bayport ni mzuri na utarahisisha upatikanaji wa huduma bora kwa wateja wao na Watanzania kwa ujumla.
“Nimeangalia ni mfumo mzuri na rahisi kwa mteja wa Bayport kupata mikopo ya haraka kwa njia ya mtandao huku ukiwa katika lugha mbili za Kiswahili na Kingereza,” alisema Millao.
Kwa mujibu wa Cheyo, hiyo ni njia rahisi na ya haraka mno inayomuwezesha kumpatia mkopo mteja wao, bila kusumbuka kwenda kwenye tawi kuanza taratibu za kujiunganisha kwenye huduma za mikopo ya taasisi yao.
Ili mtu aweze kuingia kwenye huduma hiyo, atalazimika kutumia simu yake ya mkononi yenye uwezo wa internet bila kusahau kompyuta, ikiwa hatua rahisi za kumpatia mkopo huo mteja, huku Cheyo akitumia muda huo kuwataka wateja wao na Watanzania kuiunga mkono Bayport ili kujikwamua kiuchumi kutokana na huduma zao za mikopo isiyokuwa na dhamana wala amana.

Post a Comment

0 Comments