Benki ya NBC yadhamini mkutano wa chama cha African Society for Bioinformatics and Computational Biology(ASBCB)


Mfanyakazi wa Benki ya NBC kitengo cha mauzo, Erica Mwaipasi (kulia) akizungumza na baadhi ya washiriki wa mkutano wa siku tatu wa Chama cha Watumiaji wa Elimu ya Kompyuta katika Sayansi inayohusu Utafiti wa Uhai na Viumbe hai Afrika (ASBCB) uliofanyika jijini Dar es Salaam. NBC ilikuwa mmoja wa wadhamini wa mkutano huo ambao pamoja na mambo mengine ulijadili jinsi elimu hiyo inavyoweza kusaidia ufumbuzi wa tiba ya magonjwa mbalimbali ya binadamu.
Maofisa wa Benki ya NBC Kitengo cha Mauzo, Erica Mwaipasi (kulia) na Prosper Massano (katikati) wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Vision Investments, Ally Nchahaga katika mkutano wa siku tatu wa Chama cha Watumiaji wa Elimu ya Kompyuta katika Sayansi inayohusu Utafiti wa Uhai na Viumbe hai Afrika (ASBCB) uliofanyika jijini Dar es Salaam juzi. NBC ilikuwa mmoja wa wadhamini wa mkutano huo ambao pamoja na mambo mengine ulijadili jinsi elimu hiyo inavyoweza kusaidia ufumbuzi wa tiba ya magonjwa mbalimbali ya binadamu.
Mfanyakazi wa Benki ya NBC kitengo cha mauzo, Prospper Massano (katikati) akizungumza na Promise Mwakale katika mkutano wa siku tatu wa Chama cha Watumiaji wa Elimu ya Kompyuta katika Sayansi inayohusu Utafiti wa Uhai na Viumbe hai Afrika (ASBCB) uliofanyika jijini Dar es Salaam. NBC ilikuwa mmoja wa wadhamini wa mkutano huo ambao pamoja na mambo mengine ulijadili jinsi elimu hiyo inavyoweza kusaidia ufumbuzi wa tiba ya magonjwa mbalimbali ya binadamu. Kulia ni Erica Mwaipasi wa NBC.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali wakati wa mkutano huo jijini Dar es Salaam.
Mtakwimu kutoka Taasisi ya taifa ya utafiti wa magonjwa ya binadamu Tanzania (NIMR), Dk Bruno Mmbando akielezea umuhimu wa takwimu katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za magonjwa wakati wa mkutano huo.

Post a Comment

0 Comments