Dc Mshama aagiza Wakurugenzi kuhakikisha wanafuatilia watumishi wa afya waliojiriwa na mfuko wa PEPFAR kupitia THPS mkoani Pwani



Mkuu wa Wilaya Kibaha, Assumpter Mshama akizungumza katika mkutano wa wadau wa huduma za afya hususani ukimwi, uliofanyika mjini Bagamoyo ulioandaliwa shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Health Promotion Suppot (THPS). Mkuu wa Wilaya Kibaha Assumpter Mshama alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo.

Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Maggid Mwanga akizungumza jambo katika mkutano wa wadau wa huduma za afya hususani ukimwi, uliofanyika mjini Bagamoyo ulioandaliwa shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Health Promotion Suppot (THPS).

Mkurugenzi wa THPS Dk. Mbatia akimkabidhi zawadi Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama aliyekuwa mgeni rasmi kwenye mkutano huo na kumwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Everist Ndikilo

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama akimkabidhi zawadi Dk. Beatrice (RMO PWANI) iliyotolewa na wafanyakazi wa THPC kutokana na mchango wake katika mkutano wa wadau wa huduma za afya hususani ukimwi, uliofanyika mjini Bagamoyo ulioandaliwa shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Health Promotion Suppot (THPS).


Mgeni rasmi wa hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama akimkabidhi zawadi pamoja na cheti Batuli Mituro ya Muuguzi bora kutoka kituo cha Ikwiriri HC katika mkutano wa wadau wa huduma za afya hususani ukimwi, uliofanyika mjini Bagamoyo ulioandaliwa shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Health Promotion Suppot (THPS).


Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama akipatiwa maelezo juu ya upimaji wa saratani ya mlango wa kizazi kwa kina kutoka kwa mtaalamu wa THPS.

Mgeni rasmi Assumpter Mshama akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakuu wa wilaya wenzake wa mkoa wa Pwani pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa THPS

Baadhi ya wakuu wa wilaya wa Mkoa wa Pwani akibadilishana mawazo mara baada ya kumalizika kwa kutano huo




Wakurugenzi wameagizwa kuhakikisha wanafuatilia watumishi wa afya waliojiriwa kwa ufadhili wa mfuko wa dharura wa rais wa marekani ( PEPFAR) kupitia THPS katika vituo mbalimbali mkoani Pwani wanalipwa mishahara yao kwa wakati.


Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama alipokuwa mgeni rasmi akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo, katika mkutano wa wadau wa huduma za afya hususani ukimwi, uliofanyika mjini Bagamoyo ulioandaliwa shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Health Promotion Suppot (THPS).


Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama alilipongeza shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Health Promotion Suppot (THPS) katika juhudi wanazofanya katika sekta ya afya hususani mapambano dhidi ya ukimwi mkoani humo na kuwataka watumishi wa afya kuhakikisha wana wanatoa huduma ya vvu kila mahali katika vituo vya kutolea huduma za afya , mawodini, kliniki maalumu, kwenye mikusanyiko ya watu, na maeneo mengine maalumu ili malengo ya serikali ya 90 ya tatu yatimie ifikapo mwaka 2020 .


Mshama alisema serikali iliridhia maazimio ya shirika la umoja wa mataifa ya kupambana na ukimwi ya tisini ya tatu ambapo alifafanua azimio hilo ni ifikapo 2020 asilimia 90 ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi wawe wanatambua hali zao za maambukizi, asilimia 90 ya hao wawe wanatumia dawa na asilimia 90 ya walioko kwenye dawa wafubaze virusi kwa kiwango kinachotakiwa cha kopi 1000 za virusi kwa milimita moja ya damu.


Mapema akiongea katika mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji wa THPS Dk. Redempta Mbatia alisema shirika limekuwa likitoa huduma mbalimbali hususani katika sekta ya afya katika mapambano dhidi ya vvu katika mradi wake kwa kipindi cha miaka mitano Mkoani Pwani ikiwa ni pamoja nakuboresha miundo mbinu ya vituo vya afya, kununua vifaa tiba, kutoa mafunzo elekezi kwa watumishi pia kuhakikisha kila kituo kina dawa za kutosha.


“Tunatoza ruzuku kwa mkoa wa Pwani zaidi ya shilingi million 700 kwa mwaka, fedha hizi zinatakiwa zihudumie wananchi , zifanye mambo mbalimbali ikiwemo kulipa mishahara baadhi ya watumishi wa afya walioajiriwa kwa ufadhili wa PEPFA kupitia shirika letu, lakini pia tunatoa kiasi cha shilingi 10,000 kwa kila mtumishi atakayemgundua mteja wa VVU na kuhakikisha anamshika mkono kwa mkono na kumwandikisha kwenye huduma na tiba”, alisema Dk. Mbatia


Shirika laTHPS linapata ufadhili wake kutoka mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na ukimwi (PEPFAR) na hapa nchini shirika hilo limekuwa likiendesha miradi ya kutoa huduma za VVU katika mkoa wa Pwani, Mbeya, Kigoma na Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Pages