Let's Talk Business / Tuongee Biashara Pekee.

Habari Mpya

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, March 30, 2018

Milioni 260 za Tatumzuka kunyakuliwa katika ‘Jackpot’ ya Pasaka


Tatu Mzuka, mchezo wa namba unaongoza hapa nchini unawapa fursa Watanzania kushinda kitita cha Shilingi milioni 260 katika droo itakayofanyika jumapili ya pasaka na kuonyeshwa moja kwa moja saa 3:30 usiku

Taifa linapojiandaa na sherehe za Pasaka, Tatumzuka imeungana na wateja wake kwa kutangaza fursa ya kushinda kitita cha shilingi 260 ambacho lazima kitolewe jumapili ya Pasaka.

Kitita hicho kinono cha milioni 260 ambacho hakijawahi kutolewa kwa mtu katika historia ya nchi hii sasa kitatolewa kwa mshindi mmoja atakayebahatika kwenye ‘PasakaMzukaJackpot’ siku ya tarehe 31/3/2018.

Bwana Sebastian Maganga, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa Tatumzuka, ameuelezea umma namna ilivyo rahisi kuingia katika droo. “Wiki hii ukiwa na shilingi 500 tu, kwa kutumia; Mpesa, Tigo pesa au Airtel Money, ingiza namba ya kampuni ambayo ni 555111, kisha weka namba zako tatu za bahati na hapo utakuwa umeingia rasmi kwenye droo ya milioni 260 za PasakaMzukaJackpot” alielezea Maganga

Hicho sio kitu pekee ambacho Tatumzuka inatoa msimu huu wa sikukuu, pia una nafasi ya kushinda milioni 10 kila siku na milioni 6 kila saa.“Ukinunua tiketi moja ya shilingi 500, Tatumzuka inakupa nafasi ya kuingia katika droo 3 tofauti na hivyo kukuongezea nafasi za kushinda tofauti na michezo mingine ya namba” Maganga alisisitiza

Tatu Mzuka pia imetumia fursa hiyo kuwatambulisha washindi wa wiki iliyopita ambao walitokana na droo ya 34 ya Tatumzuka jackpot.Bi Hanifa kutoka Magomeni, Dar es Salaam alijishindia milioni 5. Bwana Juma Mkombozi kutoka Magomeni, Kagera alijishindia milioni 7. Bwana Prosper Munuo kutoka Bunju A alijinyakulia milioni 5 na Magreth Nkwabi wa Kahama, Shinyanga alipata milioni 3.

Washindi wote wakiwa wenye furaha baada ya ushindi walisisitiza kwamba wataendelea kucheza kujaribu bahati zao kwenye dau la kihistoria la milioni 260 jumapili hii.‘Droo hii ya kihistoria itaonyeshwa moja kwa moja kupitia ITV, Clouds TV na TV1 jumapili hii saa 3:30 usiku’ Bwana Maganga aliufafanulia umma.

Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Sebastian Maganga akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo jijini Dar akielezea kuhusu Tatumzuka kuungana na wateja wake kwa kutangaza fursa ya kushinda kitita cha shilingi 260 ambacho lazima kitolewe jumapili ya Pasaka.

Mmoja ya washindi akikabidhiwa mfano wa Hundi yake yenye thamani ya shilingi milioni tano na la Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Sebastian Maganga.

Washindi wa Tatu Mzuka Jackpot wa wiki iliyopita kwa pamoja wakifurahi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot