Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania,Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati
wa kutangaza majina ya washiriki walioingia 5 bora katika mashindano ya
Airtel Trace Music Stars.Kulia ni Meneja Masoko wa Airtel,Anethy Muga.
Meneja
Masoko wa Airtel Tanzania,Anethy Muga akiongea na waandishi wa habari
(hawapo pichani) wakati wa kutangaza majina ya washiriki walioingia 5
bora katika mashindano ya Airtel Trace Music Stars.Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania,Jackson Mmbando.
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania,Jackson
Mmbando (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wanne
waliongia hatua ya 5 bora katika mashindano ya kuvumbua vipaji vya
muziki ya Airtel Trace Music Strars . fainali za mashindano hayo
zinategemea kufanyika mwanzoni mwa mwezi wa pili.kulia ni Meneja Masoko
wa Airtel Tanzania,Anethy Muga.
Kampuni
ya simu ya mkononi ya Airtel Tanzania leo imetangaza washiriki
walioingia tano bora katika shindano la Airtel Trace Music star,shindano
lenye lengo la kusaka na kuibua vibaji kwa wanamuziki chipukizi.
Akiongea
na waandishi wa habari,Meneja Masoko wa Airtel,Aneth Muga alisema" leo
tunayofuraha kubwa kutangaza majina ya washiriki waliofanya vizuri
katika mashindano haya na kupata nafasi ya kuingia katika hatua ya tano
bora na kuweza kumpata mmoja kati yao atakaeibuka na ushindi wa
kuiwakilisha nchi yetu katika mashindano ya Airtel Trace Afrika".
Akiendelea
kufafanua Aneth alisema "Washiriki hawa watano ni kati ya wengi
waliothubutu kuonyesha uwezo wao wa kushiriki kwa kupiga simu, kuimba na
kutuma nyimbo zao na hatimae majaji wamesikiliza vipaji vyao kama
walivyoimba na kuwachagua kuingia tano bora (top 5), sasa kura nyingi
toka kwa watanzania ndio itakayomuwezesha mmoja wao kupata ushindi wa
kwanza wa Airtel Trace Tanzania.
Mashindano
haya yanalengo la kuinua vibaji vya muziki kwa vijana wetu kuzifikia
ndoto zao na kuwawezesha kuonyesha vipaji vyao ndani na nje ya nchi.
Airtel tunajisikia furaha kuwa sehemu ya mafanikio yao na sehemu ya
kuinua vipaji vya wanamuziki chipukizi kwa kupitia mashindano haya ya
Airtel Trace Music Stars. Napenda kuwapongeza na kuwatia hamasa wale
wote walioshiriki na pia hawa waliofanya vizuri na kufika katika hatua
hii muhimu ya mashindano haya.
Akitangaza
majina ya walioibuka kwenye tano bora Meneja Uhusiano wa Airtel,
Jackson Mmbando alisema " tunawashukuru watanzania na wanamuziki
chipukizi kwa kushiriki katika shindano hili na mpaka sasa tunao vijana
wengi waliojaribu kuonyesha uwezo wao wa kuimba, lakini kama
mnavyofahamu haya ni mashindao hivyo napenda kuwaleta kwenu wale
waliofanya vizuri zaidi na kuingia katika hatua hii ya mchuano mkali.
waliobahatika
kuingia tano bora ni pamoja na Nalimi Mayunga mwenye namba ya ushiriki
(YUN), Christopher Kihwele (TOJ), Tracy Eminence (MHR), Beautus Henry
(BOB) na Rose Mbuya (ROS)
Natoa
wito kwa watanzania , wadau mbalimbali na wapenzi wa muziki kuwapigia
kura washiriki hawa kwa kupiga kutuma sms yenye jina la fumbo la
mshiriki kwenda kwenye namba 15594
Hii ni
nafasi ya pekee kwa watanzania kuonyesha uwezo na vipaji vyao katika
anga za Afrika hivyo ni matumaini yetu kuwa washiriki hawa watajifua
vyema ili kufanya vizuri katika mashindano ya Afrika pindi mshindi
atakapo patikana.
Akiongea
mara baada ya kutangaza kuwa moja ya tano bora Christopher Kiwhele
alisema" najisikia furaha sana kupata nafasi hii ya kuwa moja ya tano
bora, kwakweli kwangu ni kama ndoto, siamini kama nimeweza kufudhu ma
kufika katika hatua hii kubwa, na amini ntaendelea kufanya vizuri kwani
naendelea kujiandaa vyema, nimetamani sana kuwa mwimbaji nyota na
mwimbaji anayenivutia zaidi ni Ed sheeran naamini kupitia mashindano
haya ntafika mbali na kutumiza ndoto zangu. Nawaomba watanzania watuunge
mkono na kutupigia kura ili kuendelea kufanya vizuri na hatimae
kuwakilisha nchi yetu vyema katika mashindano ya Afrika.
Washiriki
tano bora wa Airtel Trace music Star sasa wako kambini ambapo wanapata
mafunzo yatakayoendelea hadi fainali inayotegeme kufanyika tarehe 7
mwenzi wa pili 2015 jijini Dar es saalam.
0 Comments