Mtaalam
wa Kutoa Damu wa Kitengo cha Damu Salama, Kanda ya Mashariki, Daudi
Mkawa akimtoa damu Mfanyakazi wa Airtel Tanzania, Amitin Mbamba wakati
wa zoezi la kuchangia damu lililofanywa na wafanyakazi wa vitengo
mbalimbali vya Airtel, jijini Dar es Salaam jana. Kitengo cha Damu
Salama kina upungufu mkubwa wa damu ambapo kiasi cha ujazo wa unit
350,000 zinahitajika kwa ajili ya dharura za kitabibu kila mwaka.
Wafanyakazi
wa Airtel Tanzania (kutoka kushoto), Adam Suleiman na Frank Munale
wakitolewa damu kwa ajili ya kuchangia katika Kitengo cha Damu Salama,
Kanda ya Mashariki, wakati wa zoezi la kuchangia damu lililofanyika
katika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es Salaam jana. Kitengo cha Damu
Salama kina upungufu mkubwa wa damu ambapo kiasi cha ujazo wa unit
350,000 zinahitajika kwa ajili ya dharura za kitabibu kila mwaka.
Mtaalam
wa Kutoa Damu wa Kitengo cha Damu Salama, Kanda ya Mashariki, Judith
Goshashy akimpima shinikizo la damu Mkurugenzi wa Raslimali Watu wa
Airtel Tanzania, Patrick Foya wakati wa zoezi la kuchangia damu
lililofanywa na wafanyakazi wa vitengo mbalimbali vya Airtel, jijini Dar
es Salaam jana. Kitengo cha Damu Salama kina upungufu mkubwa wa damu
ambapo kiasi cha ujazo wa unit 350,000 zinahitajika kwa ajili ya dharura
za kitabibu kila mwaka.
Mnasihi
wa Kitengo cha Damu Salama, Kanda ya Mashariki, Julius Nkomwa akimtoa
damu Mkurugenzi wa Fedha wa Airtel Tanzania, Ketan Mehta wakati wa zoezi
la kuchangia damu lililofanywa na wafanyakazi wa vitengo mbalimbali vya
Airtel, jijini Dar es Salaam jana. Kitengo cha Damu Salama kina
upungufu mkubwa wa damu ambapo kiasi cha ujazo wa unit 350,000
zinahitajika kwa ajili ya dharura za kitabibu kila mwaka.
Airtel
Tanzania imeshirikiana na Kitengo cha damu salama cha taifa (National
Blood Transfusion Services) katika zoezi la kuchagia damu ili kupunguza
upungufu mkubwa nchini ambapo kiasi cha ujazo wa unit 350,000
zinahitajika kwaajilii ya dharura za kitabibu kila mwaka.
Zoezi
hilo la kuchangia damu limewashirikisha wafanyakazi wa Airtel kutoka
katika vitengo mbalimbali kujitolea na kujitokeza kuchangia damu ili
kusaidia jamii.
Akiongea
kwa niaba ya Airtel , Meneja huduma kwa jamii, Bi Hawa Bayumi alisema
“ Airtel tunaamini katika kugusa maisha ya watanzania kwa njia mbali
mbali huku tukishirikiana na wafanyakazi na wadau mbali mbali katika
kufanikisha hilo. Tumekuwa tukishirikiana na Kitengo cha kuchagia damu
kila mwaka kwa kuhusisha wafanyakazi na wadau mbali mbali kuchangia ili
kuongeza damu katika benki ya damu ya taifa kwa ajili ya mahitaji ya
dharura. Mwaka huu tunaendeleza utamaduni huu ili kuwawezesha matibabu
hususani kwa wanawake na watoto wanaohitaji msaada wa damu kupata huduma
hii kwa urahisi.
Tunawashukuru
wafanyakazi na wadau wetu mbalimbali kwa kujitolea na kushiriki katika
kuchangia kila mwaka na pia tunaahidi kuendelea kutoa elimu kwa jamii na
wafanyakazi wetu juu ya umuhumi wa kuchangia damu kwani kwa kufanya
hivyo tunaweza kuokoa maisha ya wengi wanaohitaji huduma hii kuipata kwa
haraka na urahisi.
Kwa
upande wake mwakilishi kutoka kitengo cha damu salam Judith Charles
alisema” Tunawashukuru wafanyakazi wa Airtel kwa kuonyesha mfano kwa
kujitokeza kuchangia damu leo, Natoa wito kwa watanzania kujenga tabia
ya kujitolea kuchangia damu kwani kwa kufanya hivyo kutatuwezesha kuwa
na units za kutosha kuhudumia wale wanaohitaji wakati wa dharura. Maisha
hayana uhakika inawezekana siku moja wewe ukawa ni mmoja kati ya wale
wanaohitaji, hivyo tunahimiza watanzania kujenga utamaduni wa kuchangia
damu.
Mpaka
sasa kitengo chetu kina tatizo la uhaba mkubwa wa damu hivyo natoa wito
kwa watanzania mmoja mmoja au kwa makundi kujitokeza kuchangia ili tuwe
na kiwango cha damu kinachokidhi mahitaji yanayokua kwa kasi kila siku.
0 Comments