Mkurugenzi wa Muda wa Benki ya
NBC , Bw. Pius Tibazarwa akizungumza na wafanyakazi wa NBC katika
warsha ya siku moja kuzungumzia maendeleo na mikakati ya benki hiyo kwa
mwaka 2015. Warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi,
ilijumuisha wakurugenzi wote wa benki hiyo, wakuu wa vitengo na mameneja
wa matawi ya NBC nchi nzima.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Hazina cha Benki ya NBC, Barton Hamisi, akisisitiza
jambo wakati wa warsha ya siku moja kuzungumzia maendeleo na mikakati
ya benki hiyo kwa mwaka 2015. Warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es
Salaam juzi ilijumuisha wakurugenzi wote wa benki hiyo, wakuu wa vitengo
na mameneja wa matawi ya NBC nchi nzima.
Mkurugenzi
wa Mauzo ya Reja Reja wa NBC ,Musa Jallow akimkabidhi cheti cha mtoa
huduma bora wa mwaka 2014 Columba Kambi wa NBC Tawi la Dodoma katika
hafla ya kupongeza wafanyakazi bora katika kitengo cha mauzo
iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi.
Wakuu
wa vitengo mbalimbali vya Mauzo ya Reja Reja vya NBC Limited,
wakimkabidhi tuzo Kemibaro Omuteku (wa tatu kushoto) katika hafla ya
kupongeza wafanyakazi bora katika kitengo cha mauzo iliyofanyika jijini
Dar es Salaam juzi.
Mkurugenzi
wa Mauzo Wa NBC Musa Jallow, akimfunika shuka ya Kimasai Meneja wa
Tawi la Kahama Martin Nkanda baada ya kuibuka kuwa Meneja wa Tawi bora
wa mwaka 2014 katika hafla ya kupongeza wafanyakazi bora katika kitengo
cha mauzo iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi.
Meneja wa tawi la NBC la Muhimbili Fatma
Gulamsood (kulia) akipokea tuzo ya jumla katika ukusanyaji madeni kw
amwaka 2014. Akimkabidhi tuzo hiyo ni Andrew Massawe Mkuu wa Kitengo cha
Bidhaa za Kuwekeza na Wateja Wakubwa katika hafla ya kupongeza wafanyakazi bora katika kitengo cha mauzo iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano Mahusiano wa NBC Rukia Mtingwa akiongea na wafanyakazi wenzake (hawapo pichani) katika
warsha ya siku moja kuzungumzia maendeleo na mikakati ya benki hiyo kwa
mwaka 2015. Warsha hiyo ilijumuisha wakurugenzi wote wa benki hiyo,
wakuu wa vitengo na mameneja wa matawi ya NBC nchi nzima, akimsikiliza
kwa makini ni Eddi Mhina Meneja wa Mauzo kitengo cha Imani Banking cha
NBC.
Sehemu
ya wafanyakazi wa NBC wakipasha misuli kujiweka imara tayari kwa
mikakati ya 2015 katika kuendeleza benki yao wakati wa warsha ya siku
moja iliyojumuisha wakurugenzi wote wa benki hiyo, wakuu wa vitengo na
mameneja wa matawi ya NBC nchi nzima.
0 Comments