Meneja
Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati)akifafanua
jambo kuhusiana na mshindi wa shilingi Milioni 100/-kupitia promosheni
ya JayMillions inayoendeshwa na kampuni hiyo ambapo Mkazi wa kilolo
mkoani Iringa Bi.Uwezo Magedenge aliibuka na ushindi wa kitita hicho
katika droo ya 14 iliyochezeshwa jijini Dar es Salaam leo,Wengine ni
Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha Tanzania Mrisho Millao(Kushoto) na
Afisa wa kampuni hiyo Pristin Lyatonga.Ili mteja kujua kama ameshinda
anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
Mkazi
wa Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Uwezo Magendenye (22) , leo ameibuka
mshindi wa kwanza wa shilingi milioni 100 katika droo ya kumi na nne ya
promosheni ya Jaymilioni inayoendeshwa na kampuni ya mawasiliano ya
Vodacom Tanzania.
Magedenge
binti mwenye umri wa miaka 22 ambaye ni mhudumu wa mapokezi katika
nyumba ya wageni ya Luganga Lodge iliyopo wilayani Kilolo amesema kuwa
amepokea taarifa hizi kwa furaha akiwa kazini na amefurahia ushindi huu
ambao anaamini utabadilisha maisha yake kwa kiasi kikubwa.
“Katika
maisha yangu nimeishapitia mambo mengi nahangaika na maisha hadi
kufikia hapa nilipo nikiwa mhudumu kwenye nyumba ya wageni.Kwa ushindi
huu naamini nitafungua shughuli zangu za biashara ikiwemo kuanzisha
biashara ya maduka ya M-Pesa pia kufungua nyumba yangu ya kulala wageni
na kusaidia ndugu zangu ambao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za
maisha”.Alisema.
“.Nashukuru
Vodacom kwa kuleta promosheni hii ambayo naamini itabadilisha maisha
yangu na namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniona na kusikiliza sala zangu .
Aliongeza
kuwa kwa muda mrefu amekuwa akishiriki kwenye promosheni mbalimbali na
hajawahi kufanikiwa kwa ushindi huu anaamini kuwa promosheni hizi
hususani za Vodacom ni za kweli na amewataka wateja wote kushiriki ili
kutopoteza bahati zao za kujishindia mamilioni ya fedha na kubadilisha
maisha yao.
Akiongea
muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi, Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom
Tanzania,Rene Meza amempongeza mshindi na kuwahimiza wateja wote
kuchangamkia promosheni hii kwa kuhakikisha wametuma neno JAY kwenda
namba 15544 ili kutopoteza nafasi zao za kushinda pia alisema kuwa njia
nyingine ya kushinda ni kutuma neno AUTO kwenda namba 15544 iwapo simu
haina fedha ambapo mteja akiweka fedha anakatwa shilingi 300/-.
Naye
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania alisema kuwa tangu
promosheni hii ianze mapema mwezi huu tayari wateja 2
wamekwishajishindia milioni 10 na wateja watano wameishajishindia
shilingi milioni moja kila mmoja na maelfu wengine tayari wamejishindia
muda wa maongezi.
“Promosheni
hii itadumu kwa muda wa siku mia moja hivyo leo ni droo ya kumi na nne
hivyo bado kuna mabilioni ya fedha yamewasubiri watanzania,wanachopaswa
kufanya ni kuhakikisha kila siku wameangalia kama namba zao zimeibuka na
ushindi kwenye droo ya siku kwa kutuma neno Jay kwenda namba 15544.
0 Comments