Zaidi ya shilingi Bilioni 20/- kuendelea kushindaniwa katika promosheni ya JayMillions

Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa(katikati)akiongea na waandishi wa habari hivi karibuni (hawapo pichani)wakati wa uzinduzi wa Promosheni ya JayMillions,Wengine katika picha kushoto ni Balozi wa Promosheni hiyo Hilary Daud”Zembwela” na kulia ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.

Uwezo Magendege, 22, ni mshindi wa kwanza wa zawadi nono ya siku ya pesa taslimu Sh. 100m/- za promosheni iliyozinduliwa siku 19 zilizopita na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania.
Hadi kufikia leo ni Sh. 126m/- pekee zilizokwisha kuchukuliwa na Uwezo, washindi wengine wawili – Hyness Petro Kanumba from Rukwa and James Mangu (Mwanza) – wa Sh. 10m/- na sita – Chiliphod Wanjala (Mwanza), Janeth Ngannyange (Njombe), Evarista A (Mwanza), Stanley Bagashe (Shinyanga), Ramadhani H. Maulid (Dodoma) and  Lucas M (Shinyanga) – wa Sh. 1m/-. Kiasi cha zaidi ya Sh. 5bn/- (ambazo ni sawasawa na magari madogo 428 ya muundo wa mgongo wa kobe) zingeweza kunyakuliwa na wateja iwapo wangetuma neno “JAY” kwenda 15544 kucheki kama wameshinda.
Uwezo ni mkazi wa wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa. Mnamo Alhamis Januari 29, 2015, Uwezo alipokea simu ambayo ilipelekea maisha yake kubadilika milele alipotaarifiwa kuwa amejishindia Sh. 100m/- kutoka katika mamilioni ya shilingi yanayogawiwa kupitia promosheni ya JayMillions ya Vodacom Tanzania kwa siku hiyo.
“Nawasihi wateja wote wa Vodacom wasiache kucheki kila siku kujua kama wameshinda. Mimi ndoto zangu zinatimia kupitia promosheni hii maana tangu kuanzishwa kwa JayMillions nimekuwa nikicheki kila siku. Pamoja na kupata ujumbe kwamba sijashinda mara kila mara, sikuacha kucheza. Siku ile nilipoamua kutuma “AUTO” kwenda 15544 ndipo nilipopata ujumbe papo hapo kwamba nimeshinda,” alielezea Uwezo, akiwa na furaha tele.
Uwezo anategemea kutumia sehemu ya pesa alizoshinda kujilipia ada ya shule ambapo amepanga kujiunga na mkondo wa biashara katika elimu ya juu. Amepanga pia kuwekeza sehemu ya mapato haya katika mradi wa upandaji miti. Kwake yeye mradi huu si tu sehemu ya kujipatia kipato bali utakuwa ni kumbukumbu ya bahati hii aliyopata kwa vizazi vyake vijavyo.
Promosheni ya JayMillions ni ya kipekee nchini ambapo kila siku wateja wote wa Vodacom huingizwa kwenye droo halafu wateja 111 huchaguliwa ambapo wanaweza kujishindia zawadi za pesa taslimu iwapo watacheki.
Kila siku mteja mmoja wa Vodacom anaweza kujinyakulia kitita cha Sh. 100m/-, wateja 10 kujishindia Sh. 10m/- na wateja 100 kujishindia Sh. 1m/-. Wateja 10,000 wanaweza kujishindia muda wa maongezi wenye thamani ya Sh. 1000/- kila siku. Kujua kama wameshinda, wateja wa Vodacom wanapaswa kucheki kila siku kwa kutuma neno “JAY” kwenda 15544.
“Tunaendelea kuwasisitizia wateja wetu wacheki kila siku ili kujua kama namba zao zimeshinda. Kama Uwezo asingetuma ujumbe siku ile angeendelea tu na maisha yake kama yalivyokuwa bila kujua kama namba yake ilichaguliwa kushinda. Hadi hivi sasa tuna washindi 9 wa zawadi za pesa taslimu Sh. 126m/- lakini kila siku wateja 111 wanachaguliwa kushinda. Bado kuna Sh. 24.3bn/- za kushindaniwa kwa siku 81 zilizosalia kwenye promosheni hii hivyo endeleeni kutuma “JAY” kwenda 15544 kila siku,” alisema Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa.
Baada ya kutuma neno “JAY” kwenda 15544, mteja atapokea ujumbe kumjulisha kama ameshinda au la. Kama hajashinda atashauriwa kujaribu tena siku inayofuata. Kila ujumbe mfupi unagharimu Sh.300/- lakini tofauti na promosheni zilizopita, JayMillions haina maswali mengi, wala chemsha bongo. Kila mteja ana nafasi ya kushinda.

No comments:

Post a Comment

Pages