Imekuwa ni kitu cha kawaida kwa
wapendanao kusherehekea na kufurahi pamoja siku ya Valentine tar
14.02.2015 kila mwaka, sio kwamba nyakati nyingine wapendanao hawana
nafasi za kuonyesha mapenzi yao, la hasha, utofauti ni kwamba siku hii
inakuwa na hamasa na bashasha zaidi, na wengi kujitokeza kuonyesha kitu
cha tofauti kwa wapenzi wao. Inawezekana sana ukasherehekea, ukafurahia,
kula na kunywa na mwisho wa siku mahusiano yako na mpenzi wako
yakabakia vile vile yalivyokuwa, hapa tunakuja na fursa njema kwako,
kuyaruhusu mahusiano yako kupevuka na kukua zaidi kwa kujifunza mambo
yatakayoboresha kuhusiana kwenu wakati huo huo mkila, mkinywa na
kufurahi. Tunakuletea VALENTINE LOVERS' DINNER & TALK itakayofanyika
siku ya Jumamosi tar 14.2.2015 pale Mbezi Garden Hotel, Mbezi Beach
kuanzia saa moja jioni. Kwa moyo mkunjufu kabisa napenda kuwaweka mbele
yako partners waliosimama pamoja kuhakikisha tukio hili linakufikia.
Shukrani za pekee sana ziwafikie
Christom Solution ni kampuni
inayojishuhulisha na kuandaa, kupanga na kuratibisha matukio ya kijamii,
kiserikali na shuhuli za makampuni "Corporate events". Christom
solution wanajishuhulisha pia na ushauri wa kisaikolojia "Counselling
therapy" pamoja na mafundisho na mazungumzo ya halaiki katika
kuhamasisha na kutia moyo "Public, inspirational and motivational
talks". Kwa kupata huduma zao wasiliana nao kwa namba 0713 407182 au
chrismauki57@gmail.com
Sherehe yetu ni blog maarufu sana hapa
nchini kwa sasa inayokuwezesha kupata kila unachohitaji kuhusu styles
za shuhuli kama maharusi, sendoff, kitchen poarties na nyingine nyingi,
za ndani ya nchi na nje ya nchi. Baadhi ya picha unazoziona ndani ya
www.chrismauki.com ni vionjo tu, picha nyingi zaidi utakutana nazo
kwenye www.shereheyetu.com. Hawa wanashiriki pia katika kulitangaza
tukio hili la wapendanao
Siku hiyo wapendanao waliodumu katika
mahusiano kwa muda mrefu zaidi na wale ambao ndio wapya zaidi kwenye
mahusiano watatuwakilisha kukata keki maalumu iliyotolewa kwa hisani
kubwa ya Angela Cakes. Katika shuhuli mbali mbali, kwa mahitaji ya keki
za aina zote wasiliana na Angela Cakes kwa 0782 297408.
Usisahau kabisa kwamba siku ya
wapendanao ndio ile miziki na nyimbo za taratiiibu za mapenzi na jumbe
za kuhamasisha mahusiano zitayafikia masikio yako kupitia spika murua
kutoka Respect DJ's. Hawa wanasimama thabiti kuhakikisha mahitaji yako
yote ya muziki na PA System yanakamilika. Sikuhiyo DJ mix zote na Sound
system itamilikiwa na Respect DJ's. Red carpet pia ita nakshiwa na
vijana wa Respect DJ's. Shukrani za dhati zikufikie mpiganaji wangu
Abdul Kimanga.
Mambo ya kupendeza na kutoka fresh na
kitanashati yana
wenyewe. Nakuletea mbele yako wenye shuhuli hii ya kuhakikisha
unatokelezea na unasimama smart pale kati. Ni RM Collections. Hawa
wanahusika zaidi na uuzaji wa suti za kiume, viatu, miwani za ukweli na
za kisasa kabisa kutoka nchi mbalimbali, wana nguo za kike pia, wana
blazers "makoti ya juu ya wanaume", hizi ni za ukweli sanaaaa, wana tai
za rangi na material tofauti. Wanapatikana Migombani street kwenye kona
ukitokea Hospitali ya Kairuki kama unapita njia ya kutokea Shoppers
Plaza, au njia ya kwenda Ursino street. Ukitokea Shoppers duka lipo
kushoto hapo hapo kwenye kona na ukitokea Kairuki hospital duka lipo
kulia kwako kwenye kona utaona bango kubwa juu ya duka RM Collections.
Wacheki kwa namba 0767 224 504. RM Collection watasimamia kiuthabiti
zoezi la kuhakikisha mzungumzaji wa valentine talk anapendeza kuanzia
chini hadi juu. Shukrani za dhati na za kipekee ziwafikie RM Collections
0 Comments