Mkurugenzi
wa masoko wa Airtel bw. Levi Nyakundi (kushoto) akimkabidhi mmoja kati
ya washindi wa promosheni ya Yatosha Zaidi bi. Mwajabu Omary katika
makabidhiano yaliyofanyika katika ofisi za makao makuu ya Airtel
Tanzania. Anayeshuhudia (katikati) Mkurugenzi wa wa kitengo cha
Mawasiliano bi Beatrice Singano Mallaya .Airtel imekabidhi magari matatu
katika hafla hiyo.
KAMPUNI
Ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania asubuhi imekabidhi magari kwa
washindi watatu wa kwanza wa promoseni ya Yatosha Zaidi.
Hafla
hiyo fupi ya kuvutia ilifanyika Makao Makuu ya Airtel jijini Dar es
Salaam na kushuhudiwa na waandishi wa habari, wafanyakazi wa Airtel na
wageni waalikwa kadhaa.
Mkurugenzi
wa Masoko wa Airtel Levi Nyakundi aliwaomba washindi kuendelea kutumia
mtandao wa Airtel kwani kwa sasa wao ni sehemu ya familia ya kampuni
hiyo.
Washindi
hao ni mkazi wa mkoani Pwani, Ramadhan Dilunga (53) ambaye ni mkulima,
mwalimu mstaafu na anayeishi Mtwara, Namtapika Kilumba (60) na
mfanyabiashara mkazi wa Dar es Salaam, Mwajabu Churian (27).
Akizungumza
kwenye hafla hiyo, Mkurugenzi Mawasiliano Bi Beatrice Singa Mallya
alisema: “Tukio hili la leo linaweza kuchukuliwa kama mwanzo wa mipango
mingi iliyopo kwenye kampuni yetu. Kuna mambo mengi yanakuja na
madhumuni yetu makubwa ni kushiriki katika kubadilisha na kuboresha
maisha ya Watanzania kadhaa wenye bahati.
“Tunaridhishwa
na kufurahia uungwaji mkono tunaoupata kutoka kwa wateja wetu, vyombo
vya habari na pia serikalini, ieleweke kwamba Airtel ipo na itaendelea
kuwapo nchini.”
Akizungumza
kwa niaba ya washindi wenzanke Mwajabu Omary alisema: “Tunachoahidi kwa
uongozi wa Airtel na wafanyakazi wake ni kwamba, tutaendelea kuunga
mkono huduma zinazotolewa na Airtel. Kwa ushindi wetu huu si ndugu na
jamaa zetu pekee ndio watatiwa moyo wa ushiriki kwenye promesheni ya
Airtel Yatosha Zaidi, bali pia Watanzania wote.”
Wiki
moja iliyopita, Airtel Tanzania ilizindua promosheni ya Airtel Yatosha
Zaidi Promotion kwa kutenga magari 60 mapya aina ya Toyota IST kama
zawadi kwa washindi. Kila siku kwa siku 60 gari moja litatolewa kwa
mteja atakayeshinda.
Wikiendi
iliyopita, washinda hawa waliozawadiwa magari leo walitangazwa baada ya
droo kufanyika. Droo hiyo ilishuhudiwa na mwakilishi kutoka Bodi ya
Michezo ya Kubahatisha huku Balozi wa Airtel Yatosha, msanii wa filamu,
Elizabeth Michael maarufu zaidi kama Lulu, akiwatangaza washindi.
0 Comments