Balozi wa Jaymillions Ahimiza Wateja Kuangalia kama Namba zao Zimeshinda Kila Siku

Balozi wa Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hilary Daud”Zembwela” (kulia) akisalimiana na Mshindi wa kwanza wa shilingi milioni 100 kupitia promosheni hiyo mkazi wa Kilolo mkoani Iringa Uwezo Magedenge (22)mara alipomtembelea hotelini kwake alipofikia jijini Dar es Salaam kabla ya kukabidhiwa kitita chake wiki iliyopita na kurudi mkoani Iringa.
Mshindi wa kwanza wa shilingi milioni 100 kupitia promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania ,Uwezo Magedenge (22) ambaye ni mkazi wa Kilolo mkoani Iringa,akiteta jambo na Balozi wa Promosheni hiyo Hilary Daud”Zembwela” alipotembewa hotelini kwake na Balozi huyo kabla ya kukabidhiwa kitita chake wiki iliyopita.

Balozi wa promosheni ya Jaymilioni inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hillary Daud ”Zembwela”maarufu kwa jina la Zembwela  wiki hii alikuwa kivutio kwa wananchi wengi alipotembelea eneo maarufu la  maduka la Mlimani City lililopo jijini Dar es Salaam ambapo alitoa ofa ya kuwalipia  baadhi ya wateja waliokuwa wananunua mahitaji ikiwemo pia kuwagawia fedha baadhi ya wananchi waliokuwa katika eneo hilo.

Ziara hiyo ilileta msisimko mkubwa wa wananchi waliokuwa eneo hilo ambapo  baadhi yao walilazimika kuacha shughuli zao kumwangalia balozi huyo na wengine kuomba kupiga naye picha ikiwemo waliompiga picha kwa kutumia simu zao zao mkononi.

Zembwela alitumia fursa hiyo kuwaeleza wananchi kuwa wanaotumia mtandao wa Vodacom wahakikishe kila siku  wameangalia kama namba zao zimeshinda mamilioni ya fedha kwa kutuma neno JAY kwenda namba 15544 na aliwataka wale ambao hawako kwenye mtandao wa Vodacom wajiunge nao ili  washiriki kwenye promosheni hii kubwa iliyolenga kubadilisha maisha ya watanzania wengi kuwa mamilionea.

“Leo nimewafuata huku kuwagawia mapesa kwa maana naona wengi wenu bado hamjachangamkia fursa hii kwa kuangalia iwapo  namba zenu zimeshinda kila siku,bado tunayo mabilioni ya fedha kwa ajili yenu hivyo changamkia fursa hii muweze kujishindia mamilioni ya fedha katika kipindi hiki cha promosheni.Kila siku kuna mshindi 1 wa shilingi  milioni 100,000,washindi 10 wa milioni 10 na washindi 100 wa shilingi milioni 1 hivyo kazi kwenu na Vodacom.Alisema.

Naye Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu aliwahimiza Watanzania na wateja wote kuchangamkia promosheni hii kwa kuhakikisha wametuma neno JAY kwenda namba 15544 ili kutopoteza nafasi zao za kushinda pia alisema kuwa njia nyingine ya kushinda ni kutuma neno AUTO kwenda namba 15544 iwapo simu haina fedha ambapo  mteja akiweka fedha anakatwa shilingi 300/-

  Alisema kuwa tangu promosheni hii ianze mapema mwezi uliopita  mteja mmoja ameishajishindia milioni 100,  wateja 2  wamekwishajishindia milioni 10 na wateja kumi na moja wameisha jishindia shilingi milioni moja kila mmoja  na  maelfu wengine tayari wamejishindia muda wa maongezi.

Wateja wa Vodacom ambao tayari wamejipatia mamilioni ya fedha kupitia promosheni hii ni Uwezo Magedenge mfanyakazi nyumba ya wageni  wilayani Kilolo mkoani Iringa ambaye amejishindia milioni 100. Waliojishindia milioni kumi kila mmoja wao Hynes Petro Kanumba mkulima kutoka Inyonga mkoani Rukwa na James Mangu mfanyabiashara  kutoka wilayani Magu.

Washindi wa milioni moja  ni Chiphold Wanjara mjasiriamali wa Kutoka Mwanza ,Janeth Nganyange wa Njombe,Evarista Minja mwanafunzi kutoka Mwanza,Stanley Bagashe Mwalimu  wa Shinyanga,Ramadhani Maulid Mkulima kutoka Dodoma, ,Lucas Masegese wa Shinyanga,Ayub Makonde mfanyabiashara wa Mbeya,Hyasinti Mlowe Fundi gereji kutoka Njombe,Florian Gwayu mchapishaji kutoka Arusha,Modesta Millanzi mjasiriamali kutoka Peramiho mkoani Ruvuma na Nobert Minungu mwanafunzi kutoka Mbwanga mkoani Dodoma.

“Promosheni hii itadumu kwa muda wa siku mia moja hivyo  juma  hili inaingia katika wiki ya nne na bado kuna mabilioni ya fedha yamewasubiri watanzania,wanachopaswa kufanya ni kuhakikisha  kila siku wameangalia kama namba zao zimeibuka na ushindi kwenye droo ya siku kwa kutuma neno Jay kwenda namba 15544.”Alisema

Post a Comment

0 Comments