Benki ya NBC Idara ya Uendeshaji wafanya mkutano kuweka mikakati ya kuendeleza benki


Kaimu Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Jimmy Myalize (kushoto) akikabidhi zawadi kwa mfanyakazi aliyeitumikia benki hiyo kwa kipindi kirefu cha miaka 27, Said Kilala wakati wa mkutano wa idara ya uendeshaji ya benki hiyo (COO) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha NBC, Ngwitika Mwakahesya.
Kaimu Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Jimmy Myalize (kushoto) akikabidhi zawadi kwa mshindi wa jumla katika vipengele vyote wa shindano la kumtafuta mfanyakazi mahiri katika idara hiyo, Mwanaisha Ayosi wakati wa mkutano wa idara ya uendeshaji ya benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha NBC, Ngwitika Mwakahesya.
Kaimu Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Jimmy Myalize (kushoto) akikabidhi cheti kwa mmoja wa washindi wa shindano la kutafuta wafanyakazi mahiri katika idara hiyo, Emmanuel Simon wakati wa mkutano wa Idara ya Uendeshaji ya benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Everline Ugomba kutoka ofisi ya COO.
Kaimu Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Jimmy Myalize (kulia) akizungumza wakati wa mkutano wa idara ya uendeshaji ya benki hiyo (COO) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katika mkutano huo wafanyakazi hao waliweza kuweka mikakati mbalimbali ya kufanikisha maendeleo ya benki hiyo.
Kaimu Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Jimmy Myalize (wa nne kushoto waliosimama) akipozi kwa picha na washindi na washiriki wa shindano la kutafuta watumishi mahiri katika vipengele vya Respect, Integrity, Service Excellence, Stewardship wakati wa mkutano wao jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

No comments:

Post a Comment

Pages