Kufuatia
anguko la shilingi ya Tanzania dhidi ya dola wafanyabiashara nchini
wametakiwa kuona kuwa ni fursa ya wao kijiinua kiuchumi katika biashara
zao ndani na nje ya nchi na kuachana na propaganda za wanasiasa ambapo
wanalalamikia anguko hilo.
Ambapo
hali hiyo imesababisha kupanda kwa bidhaa mbalimbali nchini hali
inayotajwa kuongeza ugumu wa maisha ya wananchi sambamba na
wafanyabiashara nchini ambao wananunua na kuagiza bizaa kutika nje ya
nchi.
Hayo
yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei
wakati akiongea na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya mkutano
mkuu wa ishirini wa wanahisa wa Benki ya Crdb unatarajia kufanyika
kesho jijini Arusha katika kituo cha mikutano cha Kimataifa AICC.
Hata
hivyo alisema kuwa hivi sasa Benki hiyo imeweza kupata faida ya
shilingi bilioni 95.6 sawa na asilimia 14 kwa mwaka 2014 ambapo limekuwa
ni ongezeko kubwa zaidi kutokea ambapo faida hiyo itawasaidia kuweza
kupatia wanahisa hao gawio la shilingi 15 kwa kila hisa na idadi ya
wanachama hao.
Ambapo
mizania imeongezeka kwa asilimia 17 katika lengo lao katika mwaka huu
ingawa soko limekuwa gumu kutokana na mfumuko wa bei uliopo sasa.
Dk.
Kimei aliongeza kuwa kutakuwepo na ajenda mbalimbali katika mkutano huo
mkuu ambapo moja ya ajenda ni kuangalia namna ya kukua zaidi na
kuongeza mtaji wao na kuboresha mfumo mzima wa Tehama ili kuweza
kukabiliana na wizi wa kupitia mtandao ili kuweza kuwahakikishia usalama
wa pesa za wateja wao.
Aidha
Banki hiyo inamkakati wa kuongeza mtaji wao ambapo wanatarajia kuongeza
zaidi ya billion 100 ili kuongeza aman za banki na mtaji wao ili
kuboresha huduma hizo na kukuza rasilimali za banki hiyo.
Dk.
Kimei aliongeza kuwa wanamkakati wa kupanua huduma zao katika nchi ya
Burundi na nchi jirani ili kuweza kuwarahishishia wateja wao pindi
wanapotoka na kutembelea nchi hiyo na kupata huduma ya miamala ya fedha.
Benki
hiyo hivi sasa wanamawakala zaidi ya 575 ya fahari huduma na
wanamashine ya zaidi ya 375 za kutolea pesa katika mikoa yote nchini ili
kuwarahisishia wateja wao kupata huduma za kibenki.
0 Comments