Mwenyekiti
kamati ya soka la vijana katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Ayubu
Njenza (kushoto) akimkabidhi vifaa vya michezo katibu wa chama cha
mpira wa miguu Wilaya ya Kinondoni,Isaac Mazwile kwaajili ya mashindano
ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars, inayoanza
tarehe 24 Julai mkoani Mbeya. katikati ni Afisa Uhusiano Airtel,Jane
Matinde. Makabidhiano hayo yalifanyika leo jijini Dar-es-Salaam.
Mwenyekiti
kamati ya soka la vijana katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Ayubu
Njenza (kushoto) akimkabidhi vifaa vya michezo katibu wa chama cha
mpira wa miguu Wilaya ya Ilala Kanuti Daudi kwaajili ya mashindano ya
vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars katikati ni
Afisa Uhusiano Airtel Jane Matinde. Makabidhiano hayo yalifanyika leo
jijini Dar-es-Salaam.
Mwenyekiti
kamati ya soka la vijana katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Ayubu
Nyenza akiongea wakati kupokea vifaa vya michezo ya Airtel Rising Stars
kutoka kwa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel , Kulia Afisa Uhusiano
Airtel,Jane Matinde kushoto ni Afisa Maendeleo wa TFF bwana Jemadari.
Mwenyekiti
kamati ya soka la vijana katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Ayubu
(katikati kushoto), Afisa Uhusiano Airtel, Jane Matinde, katibu wa
chama cha mpira wa miguu Wilaya ya Kinondoni,Isaac Mazwile kulia na
Afisa Maendeleo wa TFF bwana Jemadari kwa pamoja wakionyesha vifaa vya
michezo vitakavyotumika wakati wa michuano ya Airtel Rising Stars.
Airtel jana ilikabithi vifaa kwa timu zote zitakazoshiriki michuano ya
Airtel Rising Stars kwa mwaka huu.
Afisa
Uhusiano Airtel, Jane Matinde akimkabithi vifaa vya michezo Mwenyekiti
kamati ya soka la vijana katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Ayubu
Nyenza kwaajili ya mashindano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya
Airtel Rising Stars, inayotegemea kutimu vumbi kuanzia Ijumaa, Julai 24,
2015 mkoani Mbeya.
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel leo imekabidhi jezi kwa timu za wasichana
na wavulana za U-17 zinazoshiriki michuano ya Airtel Rising Stars ambayo
inatarajiwa kuanza katika ngazi ya mkoa Ijumaa, Julai 24.
Mkoa
wa Dar es Salam unajumuisha mikoa ya kisoka ya Ilala, Kinondoni na
Temeke huku timu nyingine zikitoka mikoa ya Morogoro, Mbeya, Arusha na
Mwanza. Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa makabidhiano hayo
yaliyofanyika katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, jijini Dar es
Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya soka la Vijana ya TFF Ayoub
Nyenzi alisema kwamba maandalizi yote kwa ajili ya michuano hiyo ngazi
za mikoa yamekamilika.
“Ni
matarajio yetu kuwa tutashuhudia mechi zilizojaa ushindani na mvuto na
vilevile ningependa kuona mamlaka zinazohusika na usimamizi wa michuano
hiyo ngazi ya mkoa zikichagua wachezaji bora ambao wataunda timu za
kombaini za mikoa tayari kwa kushiriki fainali hizo ngazi ya taifa
zitazofanyika jijini Dar es Salaam baadaye mwezi Septemba”,alisema.
Mkoa
wa Mbeya utakuwa wa kwanza kuzindua mashindano yake Julai 24, ikifuatiwa
na mkoa wa Dar es Salaam Julai 27, Morogoro Agusti 1 na Arusha Agusti
9, huku Mwanza wakitarajia kufanya uzinduzi wao mnamo Agusti 15. Wageni
rasmi katika hafla za uzinduzi wa mikoa wanatarajiwa kuwa wakuu wa mikoa
husika.
Mikoa
yote shiriki inatarajiwa kuwa na timu za wavulana na wasichana isipokuwa
mkoa wa Arusha ambao unatoa timu ya wasichana pekee na Morogoro
inayoshirikisha wavulana tu. Huu ni mwaka wa tano mfululizo ambao
michuano hii imekuwa ikifanyika nchini, huku ikichangia kwa kiasi
kikubwa upatikanaji wa vipaji vyenye manufaa kwa Taifa.
Ofisa
Uhusiano wa Airtel Tanzania Jane Matinde, ameelezea nia ya dhati ya
kampuni yake kuendelea kudhamini programu za vijana huku akiomba sapoti
kutoka kwa TFF, Wizara inayoshughulikia masuala ya michezo pamoja na
wadau wengine wa mchezo wa soka.
Alisema
Airtel Rising Stars mwaka huu inaenda bega kwa bega na kampeni mpya ya
‘It’s Now’ huku nahodha wa Ivory Coast ambaye pia ni kiungo wa
Manchester City Yaya Toure akiongoza kampeni hiyo. Kampeni hii inalenga
kulea na kukuza vipaji barani Afrika kupitia nyanja mbalimbali kama vile
michezo, mtindo wa maisha na mziki lakini vilevile kuwapa mbinu
zitazaowawezesha kupata ufumbuzi wa masuala ya kiteknolojia na kuona
fursa zinazowazunguka.
Airtel
Rising Stars ni program ambayo ipo bara zima la Afrika maalum kwa ajili
kuwapa vijana fursa ya kuonesha vipaji vyao na kuwarahisishia makocha
kupata vijana ambao watawaendeleza vipaji vyao kwa manufaa ya baadaye.
0 Comments