AIRTEL YAZINDUA KADI YA MALIPO YA AIRTEL MONEY "TAP TAP"




Airtel Tanzania yazindua kadi ya malipo ya 'Airtel Money Tap Tap'
 •         Airtel yawa kampuni ya kwanza kutoa huduma ya kufanya
malipo kwa kupitia kadi inayouunganishwa na akaunti ya Airtel Money ya
mteja 
Dar es Salaam, Jumatatu 12 Octoba 2015,  Airtel Tanzania leo
imezindua  huduma ya kwanza , ya kipekee na kibunifu yenye technologia
ya kisasa ijulikanayo kama “Tap Tap”  itakayomuwezesha mtumiaji wa
huduma ya Airtel Money kufanya malipo kwa njia rahisi na,salama
kupitia kadi hiyo.
Huduma hii itawewazesha wateja na jamii kwa ujumla kutumia maendeleo
ya technologia kuleta urahisi katika kuendesha maisha yao. “Tap Tap”
itawawezesha wateja wa Airtel Money kufanya miamala kwa haraka na
urahisi kwa kugusisha kadi zao ambazo zimeunganishwa na akaunti ya
Airtel money wakati wowote wanapotaka kulipia huduma mbalimbali.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Afisa Uhusiano wa Airtel
Bi Jane Matinde alisema” Leo kwa mara nyingine tena Airtel tunachua
hatua thabiti katika kuboresha maisha ya mamilioni ya wateja wetu
kupitia uzinduzi wa huduma hii ya Tap Tap.  
Kadi hii ni rahisi
kutumia, ili kufanya malipo mteja atagusisha kadi yake kwenye kifaa
cha muuzaji na moja kwa moja kufanya malipo kwa kuweka namba yako ya 
siri, wateja wetu wataweza kulipia huduma mbalimbali katika vituo vya
mafuta , maduka ya dawa, baa, saloni, maduka ya rejareja, wataweza
kununua muda wa maongezi  kwa mawakala wa Airtel Money. Kupitia kadi
hii tunawawezesha watanzania kuwa na usalama na pesa zao na kuondoa
haja ya mteja kutembea na pesa wakati  wote. vilevile Mteja
atakapopoteza au kuibiwa kadi hela zake zitakuwa bado ni  salama”

Aliongeza kwa kusema , huduma ya “Tap Tap”  inadhihirisha dhamira yetu
ya kuboresha matumizi ya huduma za kifedha kupitia simu za mkononi na
kutengeneza njia mpya ya kufanya malipo katika technologia ya simu za
mkononi  na kuwaondolea wateja wetu athari zitakazowapata kwa kutembea 
na pesa nyingi mfukoni

 “ Tunaamini technologia hii mpya katika huduma za  kifedha kupitia
simu za mkononi italeta njia mbadala wa kufanya malipo na pia kusaidia
katika kuendelea kukuza na kutanua huduma za kifedha nchini.”.
“Ni matumaini yetu kuwa wakazi katika maeneo ya Mbagala, Temeke,
Tandika, Ubungo ambapo huduma hii imezinduliwa kwaoleo watafurahia
faida zinazotokana na huduma hii ikiwa ni pamoja na kuboresha maisha
yao kupita technologia hii ya kisasa” aliongeza Matinde
 Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu ya Mkononi ya Airtel Tanzania , Bi.
Jane Matinde akionyesha kadi mpya ya malipo inayotumia huduma ya Airtel 
Money iliyopewa jina la Airtel Money ‘ Tap Tap’ katika hafla ya uzinduzi 
rasmi wa kadi hiyo uliofanyika mbagala nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana. Airtel inakuwa kampuni ya kwanza ya simu nchini kuanzisha huduma kama hiyo ambapo mteja anaweza kuitumia kufanyia malipo mbalimbali hata kama simu yake haipo hewani.
 Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu ya Mkononi ya Airtel Tanzania , Bi.
Jane Matinde (wa pili kushoto) na Ofisa wa kitengo cha Airtel Money,
Stephen Kimea, wakiwapa baadhi ya wateja, Shabani Mneta (kulia) na
Penina Mneta,  kadi za Airtel Money ‘Tap Tap’  mara baada ya
kuunganishwa  katika hafla ya 
uzinduzi rasmi wa kadi hiyo ya malipo  inayotumia huduma ya Aritel Money 
katika kufanyia malipo mbalimbali. Uzinduzi huo ulifanyika mbagala zakhem 
nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana. Airtel inakuwa kampuni ya kwanza 
ya simu nchini kuanzisha huduma kama hiyo.
 Ofisa wa kitengo cha Airtel Money, Stephen Kimea (wa pili kulia)
akielezea faida na matumizi ya  kadi ya malipo ya airtel money ‘Tap Tap’
katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kadi hiyo  inayotumia huduma ya Aitel
Money katika kufanyia malipo mbalimbali. Uzinduzi huo ulifanyika mbagala 
zakhem nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana. Airtel inakuwa kampuni ya 
kwanza ya simu nchini kuanzisha huduma kama hiyo. Kulia ni  Meneja Uhusiano 
wa kampuni hiyo, Jane Matinde (kulia).
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la Tip Top Connection,
Hamadi Seneda ‘Madee’ akiimba katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kadi ya
malipo ya airtel money ‘Tap Tap’ inayotumia huduma ya Airtel Money katika 
kufanyia malipo mbalimbali. Uzinduzi huo ulifanyika mbagala zakhem nje 
kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana. Airtel inakuwa kampuni ya kwanza ya 
simu nchini kuanzisha huduma kama hiyo.
 Mkali wa miondoko ya kizazi kipya, Emmanuel Simwinga '*Izzo Business*'
akiimba moja ya nyimbo zake zilizompatia umaarufu ya ‘naongea na rizwani’ 
katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kadi ya malipo ya QAirtel Money ‘Tap Tap’ 
inayotumia huduma ya Airtel Money katika kufanyia malipo mbalimbali. Uzinduzi huo ulifanyika mbagala zakhem nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana. Airtel inakuwa kampuni ya kwanza ya simu nchini kuanzisha huduma kama hiyo.
  Baadhi ya wateja wa Airtel wakIonyesha kadi zao mpya za Airtel Money
‘Tap Tap; katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kadi ya malipo ya Airtel Money
‘Tap Tap’ inayotumia huduma ya Aitel Money katika kufanyia malipo
mbalimbali. Uzinduzi huo ulifanyika mbagala zakhem nje kidogo ya Jiji la
Dar es Salaam jana. Unaweza kufanya manunuzi katika maduka na katika maeneo 
mengine kwa kutumia kadi hiyo hata kama simu yako haipo hewani.

  Baadhi ya wakazi wa mbagala na maeneo mengine waliofurika katika
Uwanja wa Mbagala zakhem katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kadi ya malipo 
ya Airtel Money ‘Tap Tap’ inayotumia huduma ya Aitel Money katika kufanyia 
malipo mbalimbali jijini Dar es Salaam jana.
 Mkali wa mitaa ya mbagala, Hamidu Ali ‘prof gentleman’ akifanya vitu
vyake wakati wa  uzinduzi rasmi wa kadi ya malipo ya Airtel Money ‘Tap Tap’ inayotumia huduma ya Airtel Money katika kufanyia malipo mbalimbali jijini  
Dar es Salaam jana

No comments:

Post a Comment

Pages