SAMSUNG S7 ITAKUWEPO SOKONI MAPEMA MWAKA HUU



 Samsung GALAXY S 7
 Samsung
Samsung

Na Mwandishi Wetu , Dar Es Salaam,

Kampuni ya simu ya Samsung imevuka mipaka kwa mara nyingine tena kwa ujio wa simu za galaxy smartphone. Msimu huu, sio tu kwamba Samsung inazindua simu mpya bali inazindua mfumo mpya wa kufikiri nini hasa simu inaweza kufanya kwa jinsi tunavyoichukulia teknolojia yetu. Kwa Tanzania, Samsung inawapa watumiaji wake sababu za msingi za kuweka oda ya simu mpya ya Galaxy S7.

Simu za Galaxy S7 na S7 Edge zitakufanya ufikiri tena uwezo na vitu gani simu inaweza kufanya. Kufuatia S6 kushinda karibu tuzo zote za simu bora za smartphone kwa mwaka 2015, mwezi March kampuni ya Samsung imedhamiria kuzindua simu iliyokuwa ikisubiriwa sana katika matoleo ya galaxy. S7, simu iliyosheneni program mpya zaidi kuliko toleo lolote la Galaxy inayokuja na kasha imara, kioo chenye inchi 5.5 chenye skrini yenye mwonekano bora. Samsung Galaxy S7 ni simu ya kwanza yenye teknolojia ya kiwango cha juu cha picha (dual-pixel) na pia yenye uwezo wa kupiga picha ya mbali. Inakupa fursa ya kupiga picha  kwa zote kwa kiwango cha ubora wa juu katika sehemu zenye mwanga mdogo/giza. Simu zetu huwa tunaenda nazo kila mahali isipokuwa sehemu zenye maji. Samsung S7 imefungua ulimwengu wa kutumia simu yako ukiwa unanyeshewa na mvua au kwenye bwawa la maji. Kwa betri inayodumu muda mrefu, Samsung S7 inakupa uwezo wa kuitumia muda wa siku nzima na zaidi ya hapo.

“Tunaamini katika ulimwengu wenye mafanikio, spidi, na furaha zaidi. Tunajitahidi kufikia lengo hilo kwa ujio wa Galaxy S7 na Galaxy S7 edge kwa kuzingatia dizani murua yenye utendaji wa hali ya juu wa kukupa  ujuzi bora wa matumizi ya simu” alisema DJ Koh, Raisi wa mawasiliano na biashara wa kampuni ya simu za Samsung. “Tunawawezesha watumiaji kwa teknolojia ili kuwasaidia kujifunza mengi katika maisha na tutaendelea kusukuma gurudumu hili kwa lolote litakalowezekana.”
”Maisha ya watumiaji simu nchini Tanzania yanabadilika kwa haraka, mahitaji na matarajio yao ya kutumia simu zenye ubora wa hali ya juu yanaongezeka. Mfumo wa kuopereti ndio sababu pekee pale unapojadili simu mpya na za kisasa kwa sababu unamadhara makubwa katika ufanyaji kazi wa simu katika matumizi, na urahisi wake wa uendeaji. Wigo wa program katika simu ya Samsung Galay S7 unakupa uwezo wa usio na kifani wa matumizi ya simu kwa watumiaji wote”. Aliyasema hayo Rayton Kwembe meneja bidhaa kutoka kampuni ya Samsung Tanzania.

Simu za “smartphone” ni kwa ajili kufurahia habari na taarifa wakati bado unawasiliana. Mtu anaweza kuangalia filamu, kucheza michezo ya kwenye simu, na kuangalia picha kwa kupitia skrini ya simu yako hivyo unahitaji simu yenye mwonekano mzuri na mkubwa. Kioo cha simu kikubwa na angavu cha Galaxy S7 kina lengo la kuwapa burudani watanzania.
Nafasi ndogo ya kuhifadhi kumbukumbu na usalama umekuwa ni ishu kubwa kwa watanzania na watumiaji wa simu, kwa ujio wa S7 kutakuwa hamna tena matatizo kama hayo na uwepo wa kuweka kidole kama nywila itatatua changamoto ya usalama. Betri inayokaa muda mrefu na spidi ya ufanyaji kazi ni zawadi kutoka S7.
Simu nyingi nyingi za kawaida huwa zinakuwa na uwezo wa kawaida katika matumizi ya intaneti, intaneti inakuwa ngumu kuitumia kwa sababu ya skrini ndogo ya simu na kava pia. Kwa simu yenye nguvu katika utendaji na program inayoendana na simu, S7 itatumika kuwezesha kazi zote za kimtandao.

Kuanzia tarehe 4 mwezi March, kampuni ya simu ya Samsung itakuwa inafanya maonyesho ya Galaxy S7 katika maduka ya Samsung Mlimani City, City Mall, na Jm Mall pamoja na maduka ya Vodacom ya Mliman City na Samora avenue. Kuweka oda kunaweza pia kufanyika kwa kupiga simu namba 0766960517 au kupitia tovuti http://www.samsung.com/africa_en/home/. Maonyesho hayo ya Samsung yatahusisha kifaa chao kipya cha Gear VR- kinachokupa uwezo wa kuona vitu halisi, kitakachotumika kama bendera katika toleo hili kama ilivyokuwa kwa Gakaxy S6, S6 edge, S6 edge+ na Note 5 kwa ajili ya kuonyesha picha halisi. Gear VR inampa mtumiaji aliyevaa kifaa hicho usoni ujuzi wa tofauti ukilinganisha na anayeangalia moja kwa moja kwenye Tv kwa sababu maudhui yote ya unachoangalia yanachukuliwa na simu yako.

Maduka hayo yatakuwa yanachukua oda za samsung galaxy S7 wale wote watakao weka oda watapatiwa spika ndogo za masikioni za Samsung zinazotumia Bluetooth ambazo huwa zinajulikana kwa wengi kwa jina la Samsung level U. spika hizi zina vifaa vya kisasa vya kuwekwa shingoni ili kushikilia vizuri spika hizo ndogo masikioni. Zenye ukubwa wa 12mm spika hizo zitakupa sauti yenye kiwango cha hali ya juu. Kipaza sauti kisicho na mwangwi na chenye ubora wakati wa kuongea na simu. Kwa ajili ya kuweka oda ya simu iliyosubiriwa muda mrefu ya Samsung galaxy S7, bei ya rejareja ni Tzs 1.68m (pamoja na vat) na S7 edge kwa Tzs 1.89m (pamoja na vat).
Kampuni ya Samsung imeingia ubia na Vodacom katika kifurushi cha intaneti kwa ajili ya ujio na promosheni za Samsung Galaxy S7 ambapo watanzania watafurahia 10 GB za intaneti bure kwa kila Samsung S7.

Kuhusu Kampuni ya vifaa vya Samsung.
Kampuni ya vifaa vya Samsung ni kiongozi ulimwenguni katika teknolojia, kufungua fursa mpya kwa watu wote kila mahali. Kwa kupitia teknolojia ya hali ya juu na ugunduzi mbalimbali, kampuni ya Samsung inahamasisha ulimwengu na kuleta matumaini ya mabadiliko katika mitazamo na teknolojia zinazolenga katika televisheni, simu, vifaa vya kuvaa, kamera vifaa vya umeme, mtandao, vifaa vya afya na LED. Samsung imeajiri zaidi ya wafanyakazi 319,000 katika nchi 84 na inafanya mauzo ya mwaka dola bilioni 216.7 kujifunza zaidi tembelea www.samsung.com.

Post a Comment

0 Comments