MKURUGENZI MKUU WA PSPF, ADAM MAYINGU ATEMBELEA BANDA LA SIDO KUJIONEA SHUGHULI ZA VIWANDA, PIA ATEMBELEA MABANDA MENGINE YA WASHIRIKA


 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, (kushoto), na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Abdul Njaidi, wakitazama gari Kaparata kwenye banda la Shirika la Viwanda Vidogo vidogo SIDO kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Gari hilo limebuniwa na kutengenezwa na Mtanzania Jacob Luis, wa Kaparata Engineering.
 Mbunifu wa gari hilo, Jacob Luis, akihojiwa na mwandishi wa habari kuhusu ubunifu huo
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, ametembelea banda la Shirika la Viwanda Vidogovidogo SIDO kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, 2016 yanayoendelea pale viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Mayingu alitembelea banda hilo ili kujionea na kupata maelezo ya kina jinsi shirika hilo linavyoendeleza viwanda vidogovidogo ambavyo vinahitajika sana kwa sasa ukizingatia mkakati mkubwa wa serikali ya awamu ya Tano ambayo iemdhamiria kuifanya bTanzania kwua nchi ya viwanda na hivyo kupanua wigo wa ajira kwa Watanzania.
Mkurugenzi Mkuu huyo amabye alifuatana na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Abdul Njaidi, alipokelewa na Msimamizi Mkuu wa banda hilo, Kalumuna Benedicto, na alitembezwa maeneo mbalimbali na kujionea mashine mbalimbali zilizobuniwa na kutengenezwa na watanzania.
Pia alipata fursa ya kujionea gari lililobuniwa na kutengenezwa na Mtanzania Jacob Luis, wa Kaparata Engineering.
Gari hilo lina injini yenye ukubwa wa CC 900 na linatumia mafuta ya petrol, likitumia lita moja ya petrol kwa kilomita 15 na linabeba watu watano na mzigo wa kilo 500.
Kwa mujibu wa maelezo ya mbunifu Jacob Luis, gari hilo ni maalum kwa shughuli za shamba, kubeba maharusi, shughuli za kijeshi, polisi na zile za kiulinzi.
Mkurugenzi huyo pia alitembelea mabanda washirika wa PSPF, likiwemo lile linalokusanya wajasiriamali wanawake kutoka nchi nzima ikiwemo Zanzibar, hali kadhalika Mkurugenzi Mkuu huyo alitembelea Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya PPF, LAPF, GEPF NA PPF.
 Maelezo kuhusu gari Kaparata
 Mkurugenzi Mkuu Mayingu, akifuatana na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Abdul Njaidi, wakati akikagua mashine zilizokuwa zikionyeshwa kwenye banda hilo la SIDO
 Muangalizi Mkuu wa banda la SIDO, Kalumuna Benedicto, (kushoto), akimpatia maelezo, Mkurugenzi Mkuu Mayingu na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi kuhusu mashine hizi
  Muangalizi Mkuu wa banda la SIDO, Kalumuna Benedicto, (kushoto), akimpatia maelezo, Mkurugenzi Mkuu Mayingu na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi kuhusu mashine hizi
 Mayingu akizungumza jambo mbele ya wafanyakazi wa WCF, wakiongozwa na Afisa Uhusiano Mwandamizi, Fulgence Sebera, (watatu kulia) wakati akitembelea banda la Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF)
 Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, (kushoto), akimpatia maelezo ya kiutendaji ya Mfuko huo, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, alipotembelea banda la PPF akifuatana na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Abdul Njaidi
 Mkurugenzi Mkuu Mayingu, akitembelea banda la NSSF
 Mkurugenzi Mkuu Mayingu, akiangalia bidhaa zinazozalishwa na mjasiriamali huyu kutoka mkoani Dodoma
 Mkurugenzi Mkuu Mayingu akipata amelezo kutoka kwa mjasiriamali wa mkoa wa Manyara
 Mkurugenzi Mkuu wa PSPF akitembelea banda la LAPF
 Mayingu akitembelea banda la wajasiriamali kutoka Kigoma lililoko kwenye jengo la EOTF
Mkurugenzi Muu Mayingu (wapili kulia), akitembelea banda la GEPF kwenye jengo la Wizara ya Fedha na Mipango

Post a Comment

0 Comments