Kitengo cha Dharura TANESCO chatakiwa kuongeza ubunifu


Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini, Profesa James Mdoe amekitaka Kitengo cha Dharura cha Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kufanya kazi kwa ubunifu ili kukabiliana na malalamiko ambayo yamekuwa yakitolewa na wananchi mara kwa mara.

Profesa Mdoe aliyasema hayo mara baada ya kufanya ziara katika banda la Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake katika Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yaliyofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwa malalamiko ya wananchi juu ya ucheleweshaji wa huduma unaofanywa na kituo cha dharura cha TANESCO yamepelekea wananchi kuwa na taswira hasi juu ya shirika hilo.

“Ninawataka kuwa wabunifu katika utendaji kazi wenu, kwa kutoa huduma kwa haraka kwa kuwa nyinyi ndio mliobeba taswira ya shirika,”alisema Profesa Mdoe.

Wakati huo huo akizungumzia sekta ya madini nchini, Profesa Mdoe alisema kuwa Serikali imejipanga katika kuwawezesha wachimbaji wadogo wa madini kwa kuwa wana mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

Alisema kupitia Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali za Madini (SMMRP), Serikali imekuwa ikitoa ruzuku kwa wachimbaji wadogo wa madini wanaokidhi vigezo.

Alitaja vigezo hivyo kuwa ni pamoja na kuwa na leseni za uchimbaji madini, kuonesha kuwa wanaendesha shughuli za uchimbaji madini pamoja na ulipaji wa kodi serikalini.

Alisisitiza kuwa Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), ipo tayari kuwasaidia wachimbaji wadogo kwa kuwapatia vifaa na mafunzo ili kukuza uzalishaji wa madini nchini na hivyo sekta hiyo kuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi
Mtaalam kutoka Kampuni ya Kuendeleza Nishati ya Jotoardhi Tanzania (TGDC), Mhandisi Nyaso Makwaya (kulia) akielezea shughuli za kampuni hiyo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Prof. James Mdoe (wa pili kutoka kushoto) mara alipotembelea banda la TGDC.
Mtaalam kutoka Idara ya Madini, Wizara ya Nishati na Madini Philip Mathayo (kushoto) akitoa maelezo juu ya sera ya madini kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Prof. James Mdoe (wa pili kutoka kulia) mara baada ya kuwasili kwenye banda la Wizara kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mtaalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Marwa Petro (kushoto) akielezea sera ya nishati kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Prof. James Mdoe (wa pili kutoka kulia) mara baada ya kuwasili kwenye banda la Wizara kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kulia kabisa ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara, Asteria Muhozya.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Prof. James Mdoe ( wa kwanza kulia) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kupata maelezo kutoka kwenye banda hilo.
Afisa Uhusiano wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Yasin Silayo (kushoto) akielezea majukumu ya shirika hilo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Prof. James Mdoe (kulia).
Afisa Mawasiliano kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA) Mhandisi Yisambi Shiwa (kulia) akielezea majukumu ya wakala huo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Prof. James Mdoe (kushoto) mara alipotembelea banda la wakala huo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Prof. James Mdoe (kushoto) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika banda la Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini Tanzania (STAMICO) Zena Kongoi (kulia) akielezea mikakati ya shirika hilo katika kuwasaidia wachimbaji wadogo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Prof. James Mdoe (kushoto)
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Prof. James Mdoe (katikati) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kutembelea banda la Wizara ya Nishati na Madini na taasisi zake.
Meneja Uendelezaji Masoko na Teknolojia kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Advera Mwijage (kulia) akimwonesha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Prof. James Mdoe (katikati) matumizi ya majiko sanifu katika kupikia mara alipotembelea banda la REA. Kushoto kabisa ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Asteria Muhozya.
Mtaalam kutoka kampuni ya Arti Energy ambayo ni mdau wa Walala wa Nishati Vijijini (REA), Abdallah Seushi (kulia) akielezea bidhaa zinazosambazwa na kampuni hiyo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Prof. James Mdoe (kushoto) mara alipotembelea banda la REA.
Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Ally Mluge (kulia) akielezea muundo wa shirika hilo kwa kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Prof. James Mdoe (kushoto) mara alipotembelea banda la TPDC.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini Prof. James Mdoe akiangalia kombe la ushindi wa kwanza kwenye kundi la makampuni ya gesi na mafuta la Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) kwenye banda lake.

Post a Comment

0 Comments