Meneja
Uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari kusiana
na huduma mpya ya linda simu ya Airtel Simu Bima itakayowasaidia wateja wote
wanaotumia Simu za Smartphone kuziwekea Bima simu zao na kulipia kupitia huduma
ya Airtel Money, kulia ni Meneja wa Airtel Money Bw, Moses Alphonce na kushoto
ni Muwakilishi wa shirika la Bima la UAP bw, Charles Matondane.
Meneja
Masoko wa kampuni ya Bima ya UAP bw, Raymond Komanga akielezea jinsi mfumo wa
malipo wa Airtel SimuBima unavyofanya kazi kwa kushirikiana kampuni yake mara baada ya uzinduzi wa huduma hiyo
ya kulinda simu za smartphone kupitia bima ijulikanayo kama Airtel SimuBima,
katikati ni Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando na Meneja wa Airtel Money
bw, Moses Alphonce (kulia) huduma ya AirtelSimuBima itawawezesha wateja wa
Airtel pamoja na watumiaji wote wa Smartphone nchini kuepuka hasara pale simu
inapopotea au kuibiwa.
Toka
kulia ni meneja wa Airtel Money bw, Moses Alphonce akiwa na Meneja Uhusiano wa
Airtel Jackson Mmbando wakionyesha jinsi huduma yao ya kulipia simu za
smartphone Bima ijulikanayo kama “Linda simu
na Airtel Simu Bima” Inavyofanya kazi. Kupitia huduma hiyo sasa wateja wote
wanaotumia Smarphone nchni wataweza kuziwekea Bima zao simu kulipia kupitia huduma ya Airtel Money na
endapo simu hiyo itaibwa au kupotea mteja atalipwa ndani ya siku tano. kushoto
anaefuatilia uzinduzi huo ni muwakilishi wa kampuni ya bima ya UAP Tanzaninia bw
Charles Matondane ambao wao watakuwa wakiwalipa wateja.
Na Mwandishi Wetu,
· Wateja wa mitandao mingine pia wataweza kusajili simu zao na bima hiyo na kulipia kwa Airtel money
· Airtel Simu Bima kufidia simu za wateja wake zilizopotea au kuibwa
Kampuni
ya simu za mkononi Airtel kwa kushirikiana na kampuni ya Bima ya UAP
leo wamezindua huduma kabambe itakayowasaidia wateja wote wanaotumia
Simu za Smartphone kuziwekea Bima simu zao na kulipia kupitia huduma ya
Airtel Money.
Huduma hiyo mpya nchini kwa watumiaji wa smartphone itajulikana kama “Airtel SimuBima”
ambapo itawawezesha wateja wa Airtel pamoja na watumiaji wote wa
Smartphone nchini kuepuka hasara pale simu inapopotea au kuibiwa.
Akiongea
wakati wa uzinduzi huo Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson
Mmbandoalisema “Leo Airtel tumeongeza sababu nyingine kwa wateja wetu
kuendelea kufurahia huduma zetu, sasa wateja wote wenye simu orijino za
smartphone wataweza kusajiliwa na huduma ya ‘Airtel SimuBima’ ambapo mteja
mmoja anataweza kusajili hadi simu mbili katika mfumo huu. Ikitokea
mteja ameibiwa simu yake au kuipoteza basi kupitia huduma hii ya ‘Airtel SimuBima’ tutampatia
mteja huyo pesa ili aweze kununua simu nyingine atakayotaka na kisha
simu iliyopotea itazimwa moja kwa moja isiweze kutumika tena”.
“Mteja wa Airtel ataweza kufaidi huduma ya “Airtel SimuBima”
mara baada ya kupakuwa aplikesheni ya simuBima kutoka kwenye Playstore
na kusajili taarifa za smartphone yake ikiwemo IMEI namba pamoja na
gharama ya simu yake na papohapo atapata ujumbe utakaomwambia gharama
ya Bima ya simu hiyo kwa mwaka ambayo ataamua kuilipa yote au kuwa
anailipa kwa kila mwezi” aliongeza Mmbando
“Airtel Tanzania tunaamini kuwa ushirika wetu na shirika la bima la UAP kupitia ‘Airtel SimuBima’ utasaidia
kuhamasisha watumiaji wa simu za mkononi kununua simu orijino ili
waweze kufurahia huduma hii pamoja na huduma zingine za Airtel za
kimtandao kama vile Airtel TV, Kujisomea masomo ya VETA –VSOMO kupitia
mtandao pamoja na kufaidi aplikesheni mbalimbali za airtel zenye
kusaidia wateja katika mambo ya kiuchumi na kijamii” alieleza Mmbando
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa UAP Bw, Raymond Komanga alisema
“tunawahakikishia wateja wote wa Airtel watakaosajili namba zao katika
huduma ya Airtel SimuBima kwamba tutawalipa madai yao haraka sana pale
wanapopatwa na tatizo la kupoteza simu au kuibiwa simu zilizowekewa Bima
ndani ya siku tano tu tokea pale wanapotoa taarifa kituo cha polisi na
kutujulisha sisi, tutalipa simu za hadi shilingi milioni moja na laki
tano, lakini wateja waelewe kuwa bima yetu haitakuwa ikilipa simu
kuvunjika au
Komanga aliendelea kuelezea kuwa “Ikitokea simu ya mteja iliyosajiliwa na “Airtel SimuBima”
imepotea au kuibiwa mteja atatakiwa kutoa taarifa mapema sana na kupata
taarifa ya polisi kuhusiana na upotevu huo au wizi ili kuweza
kukamilisha malipo yake. Swala hili linatakiwa kufanywa na wateja wote
waliojisali na kulipia bima ya mwezi au ya mwaka mzima kupitia Airtel
SimuBima”
Wateja wa “Airtel SimuBima”
wataweza kudai malipo yao kwa kutumia simu nyingine ya smartphone na
kuingia katika Aplikesheni ya Airtel SimuBima kisha kufuata maelekezo ya
malipo. Vilevile mteja anaweza kutumia kompyuta na kuingia katika
ukurasa wa ‘Airtel SimuBima’ na kukamilisha taarifa za madai.
“Ukitaka kulipia huduma hii ya ‘Airtel SimuBima’ piga *150*60# kisha chagua malipo, na uchague SimuBima, papohapo malipo yatatufikia sisi moja kwa moja”. Bw, Komanga alisema.
0 Comments