Mkurugenzi
Mkuu wa shirika la Thamni Uhai Dk.Nguke Mwakatundu (kushoto) akitoa
taarifa ya utendaji na utekelezaji wa shughuli za shirika wakati wa
Hafla ya kukabidhi pikipiki 9 zenye thamani ya shilingi milioni 40 kwa
Mganga Mkuu wa mkoa Kigoma ambapo zitatumika kwenye vituo vya afya
mkoani Kigoma.
Mkurugenzi
Mkuu wa shirika la Thamini Uhai Dk.Nguke Mwakatundu (Wa Tatu kushoto)
akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kukabidhi kwa
serikali ya mkoa Kigoma pikipiki 9 zenye thamani ya shilingi milioni 40
ambazo zitatumika kwenye vituo vya afya mkoani humo.
Mganga
Mkuu wa mkoa Kigoma Paul Chaote (kati kati aliyesimama) akitoa hotuba
kwa niaba ya Katibu Tawala wa mkoa Kigoma Charles Palangyo wakati wa
Hafla ya shirika la Thamini Uhai kukabidhi kwa serikali ya mkoa Kigoma
jumla ya pikipiki tisa zenye thamani ya shilingi milioni 40 kwa ajili ya
matumzi kwenye vituo vya afya mkoani Kigoma,
Mkurugenzi
Mtendaji wa shirika la Thamini Uhai Dk.Nguke Mwakatundu (kulia)
akikabidhi moja ya pikipiki tisa zenye thamani ya shilingi milioni 40
Kwa Mganga Mkuu wa mkoa Kigoma Dk.Paul Chaote kwa niaba ya Katibu
tawala wa mkoa Kigoma Charles Palangyo ambao pikipiki hizo zitatumika
kwenye vituo vya afya mkoani humo.
Mganga
Mkuu wa mkoa Kigoma Paul Chaote (kushoto) akikabidhi funguo ya pikipiki
kwa Vitus Bukombe Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Ilagala (kati
kati) ikiwa ni moja ya pikipiki tisa zilizotolewa na shirika la Thamini
Uhai kwa vituo vya afya mkoani Kigoma kwa ajili ya kusaidia kampeni ya
kukabiliana na vifo vya mama wajawazito na watoto wakati wa kujifungua
anayeshuhudia kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Thamini Uhai
Dk.Nguke Mwakatundu.
Mkurugenzi
Mtendaji wa shirika la Thaimini Uhai Dk.Nguke Mwakatundu (wa pili kulia
mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na wageni waliohudhuria
hafla ya makabidhiano ya pikipi tisa zenye thamani ya shilingi milioni
40 zilizotlewa na shirika hilo kwa serikali ya mkoa Kigoma (wa pili
kushoto mstari wa mbele) Mganga Mkuu wa mkoa Kigoma,Dk.Paul Chaote. (Picha Zote na Fadhili Abdallah)
0 Comments