Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema (Kushoto) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya “Mwanamke na Uongozi” iliyoandaliwa na Uongozi wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (DARUSO) na kupata udhamini kutoka kwa Kampuni ya mawasiliano ya Zantel akisalimiana na baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Nkurumah kwa ajili ya kuadhimisha hafla hiyo. Katikati ni Mkufunzi Mkuu na Msambazaji wa huduma za Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Kulwa Mbena.
Meneja Mauzo wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Jensen Msechu(wa pili kulia) akifafanua kuhusu huduma na ofa mbalimbali za Kampuni hiyo kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam wakati wa hafla ya “Mwanamke na Uongozi” iliyoandaliwa na Uongozi wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (DARUSO) kwa udhamini wa Zantel. Hafla hiyo ilifanyika siku ya jumamosi katika ukumbi wa Nkurumah uliopo chuoni hapo. Kulia ni Mkufunzi Mkuu na Msambazaji wa huduma za Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Kulwa Mbena.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sophia Mjema akiwaongoza wanafunzi na baadhi ya wakufunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam kucheza nyimbo ya “Strength of a woman” ya Mwanamuziki Shaggy ambayo ina maudhui ya kuwainua wanawake wakati wa hafla ya “Mwanamke na Uongozi” iliyoandaliwa na Uongozi wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (DARUSO) kwa udhamini wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel. Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Nkurumah wa Chuo hicho mwishoni mwa juma.
Mkufunzi Mkuu na Msambazaji wa huduma za Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel, Kulwa Mbena akizungumza wakati wa hafla ya “Mwanamke na Uongozi” iliyoandaliwa na Uongozi wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (DARUSO) chini ya udhamini wa Kampuni ya Zantel. Hafla hiyo ilifanyika siku ya jumamosi katika ukumbi wa Nkurumah uliopo chuoni hapo.
Mkurugenzi wa Kitengo cha masuala ya jinsia wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dr. Eugenia Kafanabo akizungumza wakati wa hafla ya “Mwanamke na Uongozi” iliyoandaliwa na Uongozi wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (DARUSO) kwa udhamini wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel. Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Nkurumah wa Chuo hicho mwishoni mwa juma.
Baadhi ya wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari ya Zanaki wakifuatilia hafla ya “Mwanamke na Uongozi” iliyoandaliwa na Uongozi wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (DARUSO) kwa udhamini wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel. Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Nkurumah wa Chuo hicho mwishoni mwa juma.
0 Comments