BENKI YA CBA YAZINDUA HUDUMA MPYA YA KUWAFUATA WATEJA WAKE WALIPO




Mkurugenzi wa Bank ya biashara Africa CBA Gift Shoko akizungumza hivi karibuni jijini Arusha katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya kuwahudumia wateja kibinafsi (private banking) kwa kuwafuata wateja wake walipo tofauti na mfumo uliozoeleka wa wateja kufuata bank(Habari Picha na Pamela Mollel blog)

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi CBA N.Kitomari akizungumza katika uzinduzi huo hivi karibuni jijini Arusha katika hafla ya uzinduzi wa huduma mpya kwa
wateja binafsi (private banking) kwa kuwafuata wateja wake walipo tofauti na mfumo uliozoeleka wa wateja kufuata bank



Julius Konyani Mkuu wa kitengo cha wateja binafsikatika benki ya CBA akizungumza jambo katika hafla ya uzinduzi wa hudum mpya kwa wateja binafsi (private banking) kwa kuwafuata wateja wake walipo tofauti na mfumo uliozoeleka wa wateja kufuata bank



Mkurugenzi wa Bank ya biashara Africa CBA Gift Shoko akimkabidhi moja ya wateja wa benki hiyo zawadi


Huduma mpya
ya kuwahudumia wateja kibinafsi (private banking) kwa kuwafuata wateja wake walipo tofauti na mfumo uliozoeleka wa wateja kufuata bank ikiwa imazinduliwa rasmi




Julius Konyani Mkuu wa kitengo cha wateja binafsi akimkabidhi zawadi moja ya wateja wa benki hiyo katika uzinduzi wa huduma mpya ya kuwahudumia wateja kibinafsi (private banking) kwa kuwafuata wateja wake walipo tofauti na mfumo uliozoeleka wa wateja kufuata bank




Mkurugenzi wa Bank ya biashara Africa CBA Gift Shoko kulia akiteta jambo na Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi CBA N.Kitomari

Kushoto ni mkuu wa kitengo ,anayeshughulikia maswala ya benki na uuzaji kwa watu binafsi,anayefatia ni Solomon Kawiche mkuu wa kitengo cha masoko CBA,alevalia shati la kitenge ni mkuu wa kitengo cha sheria CBA ,Wapili kulia ni Julius Konyani Mkuu wa kitengo cha wateja binafsi na Mussa Kitambi Mkuu wa kitengo cha mashirika na makampuni wakiwa katika picha ya pamoja

Kulia ni mkuu wa idara ya masoko kampuni ya Smile Mkoani Arusha Veronica Martine pamoja Queen Siraki wa Benki ya CBA

Waalikwa wakichukua baadhi ya matukio yaliyokuwa yakijiri katika uzinduzi huo

Waalikwa wakiwa katika nyuso za furaha



Wadau wakipata msosi ulioandaliwa na benki ya CBA



Mc maarufu jijini Arusha ambaye ndiye alikuwa mwongozaji wa shughuli hiyo ya uzinduzi akisisitiza jambo





Bank ya biashara Africa CBA imeanzisha huduma ya kuwahudumia wateja kibinafsi (private banking) kwa kuwafuata wateja wake walipo tofauti na mfumo uliozoeleka wa wateja kufuata bank.


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo hivi karibuni jijini Arusha mkurugenzi wa Bank hiyo Gift Shoko alisema lengo la kianzisha huduma hiyo ni kutoa fursa kwa watu wote kuchangia pato la taifa.


"Hivi sasa kuna watu wanakosa muda wa kwenda Bank kupanga foleni kutokana na majukumu mbalimbali, hivyo kuwepo kwa huduma hii kutawarahisishia kupata huduma bila kwenda Bank" alisema Shoko na kuongeza


"Ni fursa kwa taasisi na mashirika mbali mbali kuchangamkia huduma hii kwani itaambatana na kuduma kama kupewa vyumba vya kufanyia mikutano, kupewa msaada wa kisheria, kupata matibabu ya nje ya nchi na mteja kupewa mtu maalimu wa kumhudumia"


Kwa upande wake Solomon Kawiche mkuu wa kitengo cha masoko CBA alisema huduma hiyo itakuwa kwenye mikoa ya Arusha, Mwanza na Dar es salaam licha ya kuwa na matawi Mbeya, Kigoma, Mtwara, Moshi na Tunduma.


Bank hiyo iliyoanza miaka ya 60 ambayo ipo Tanzania, Kenya na Uganda, yenye makao makuu mjini Nairobi hivi karibuni inatarajia kuanzaisha tawi Ivory cost kwa lengo la kujitanua zaidi kibiashara.

No comments:

Post a Comment

Pages