BENKI YA CRDB YAKUTANA NA WAFANYABIASHARA WADOGO NA WA KATI MWANZA





Na Binagi Media Group.


Benki ya CRDB leo imekutana na wafanyabiashara wadogo na wa kati mkoani Mwanza na kuwahakikishia kwamba itaendelea kutoa huduma bora ikiwemo mikopo ili kukuza mitaji yao.


Akisoma hotuba ya Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Dkt.Charles Kimei, Mkurugenzi wa CRDB tawi la Mwanza, Wambura Calystus amewahakikishia wafanyabiashara hao kwamba huduma za mikopo zitatolewa kwa wakati wote katika benki hiyo kwa kuzingatia kanuni za kibenki nchini.


Amesema benki hiyo imeendelea kutanua na kuboresha huduma zake ikiwemo uwepo wa Matawi 20, vituo vya kutolea huduma 50, ATM 135, mawakala wa Fahari huduma zaidi ya 649 katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.


Aidha amesema kwa mkoa wa Mwanza benki ya CRDB ina matawi manne, vituo vya huduma 13 pamoja na Mawakala wa Fahari Huduma zaidi ya 105 na hivyo kusaidia kuwafikia wateja wake kwa urahisi.


Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria mkutano huo, Agapiti Malya pamoja na Doroth Baltazari wameipongeza benki hiyo kwa namna ilivyowawezesha kwa njia ya mikopo na kuinua biashara zao ambapo wameomba benki hiyo kuendelea kuboresha zaidi huduma zake ili kuwanufaisha wafanyabiashara wengi zaidi.



Baadhi ya wafanyabiashara (wajasiriamali) wadogo na wa kati walioshiriki mkutano ulioandaliwa na benki ya CRDB mkoani Mwanza kwa ajili ya kujadili pamoja masuala mbalimbali ya kibenki ili kusaidia kuboresha huduma zinazotolewa na benki hiyo.



Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Mkoani Mwanza, Wambura Calystus akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huu, hii leo Jijini Mwanza

Meneja Mwandamizi wa benki ya CRDB, kwa wateja wadogo na wa kati, Elibariki Masuka akizungumza kwenye mkutano huo Jijini Mwanza

Meneja Biashara benki ya CRDB, Danford Muyango akizungumza kwenye mkutano huo

Mmoja wa watoa mada kutoka benki ya CRDB akiwasilisha mada kwenye mkutano huo

Mmoja wa watoa mada kutoka benki ya CRDB akiwasilisha mada kwenye mkutano huo

Mmoja wa watoa mada kutoka benki ya CRDB akiwasilisha mada kwenye mkutano huo

Washiriki wa mkutano huo wakifuatilia mada kwenye mkutano huo

Benki ya CRDB imeendelea kuwahakikishia wajasiriamali kwamba itaendelea kushirikiana nao kwa kuwapatia mikono yenye riba nafuu ili kukuza biashara zao

Mjasiriamali Doroth Baltazari ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Chabati Pop Food, akiwaonyesha baadhi ya wanahabari bidhaa anazotengeneza.

No comments:

Post a Comment

Pages